Misemo kwenye khanga. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misemo kwenye khanga.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Viol, May 11, 2012.

 1. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Mwenye wivu ajinyonge
  hii ni kawaida yetu sijui nyie malimbukeni
  mimi ndo shina wengine wote matawi
  utamaliza gesi kwa kupika mifupa
  Mtu mzima ovyo!
  Jicho hilo mimi nina wangu
  mtaa wa pili mtanikoma..
  asie kujua nani kama wewe ni mmbea
  Yako unayakalia yawezio midomo juu
  kama unataka kumjua mume mwenzio mwache mkeo
  chokochoko za jirani hazinitoi ndani..
  tusikosane tufikirie watoto
  Mtamaliza kuni kwa kukaanga mawe
  Ushuzi dawa yake mate
  huruma ninayo bahati sina
  wewe peleleza na wala hutaniweza
  wembamba wa reli treni inapita

  ongezea mengine
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  hunilishi, hunivishi na wala hunibabaishi
   
 3. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,856
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  vikao kaeni, umbea acheni!
   
 4. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Mshukuru Mungu kwa kila jambo.
   
 5. SIM

  SIM JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 1,639
  Likes Received: 791
  Trophy Points: 280
  Vua gamba vaa gwanda.
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  nani kama mama.....
  asante mama kwa malezi bora.....
   
 7. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Sa Sweetie hizo Khanga utapoanza kuninunulia ndo ntajua maneno yake.
   
 8. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Fitina na pelelezi ni sumu ya penzi
  Dhuluma si njema
  Mama nipe radhi kuishi na watu kazi
  CCM NO.1
  Penye udhia penyeza rupia
   
 9. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  ..................................... (hiki ni kitenge jamani, hakina maneno..eti!? :lol:)
   
 10. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,749
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Miaka 50 ya Uhuru
   
 11. S

  Starn JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 400
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huo sio msemo
   
 12. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,994
  Trophy Points: 280
  Tenda wema mara mia,adui akijua, umeumia.

  Kama unaweza mtie kama mumeo umzuie.

  Mbuzi kala mkeka,wambea mtakalia nini?.

  Usisafirie nyota ya mwenzio.

  Utamu wa wali matandu,uzuri wa kiuno chach*ndu.

  Raha ya nanga baharini,mtoni utatoka na tope.

  Mjinga akierevuka,mwerevu uko matatani.

  Utamu wa mtwangio kutwanga,raha ya wanaume,mapanga nshhaaaa....!!!
  Niendelee....?
   
 13. Junior. Cux

  Junior. Cux JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 5,305
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  nimekukubali madame.. dahh, Uzuri wa kiuno chachandu.!!!
   
 14. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,994
  Trophy Points: 280
  Umeona e Junior. Cux?
  Wakwako anazivaa au ndo keshaingia Town wamtafutia cheni...?!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Msolid1990

  Msolid1990 Senior Member

  #15
  May 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nguvu mpya kasi mpya ari mpya na spid za ajabu.
   
 16. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Madame B raha ya nanga baharini...nimekukubali endelea

  Sikuhadae rangi,tamu ya chai sukari
  Chakumbimbi ukimuona muogope
  Sijafunzwa kula ndizi sukari
  Macho yanacheka, moyo unalia
  unalo limekuganda
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  1.Mpaka Kieleweke
  2.Hapa kazi tu kula kwenu
  3.Kula CCM Kura CHADEMA
   
 18. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Asante mama kwa Malezi yako Mema
   
 19. Junior. Cux

  Junior. Cux JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 5,305
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  yani wish angejua navozitamani lakini ye kakomaa na gold ooh silver... Ndo mana 2naenda kuzitaftia nje.!!! Am sure sir B anafaidi sana..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,994
  Trophy Points: 280
  Naendelea...!!
  Utamaliza visigino kwa safari za umbea.

  Aruuuuu.

  Hausimiki,hausimami.

  Tondola nidambe,dambila humohumo.
   
Loading...