Misemo hii ya Kiingereza inanipa wakati mgumu kuitumia....

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
23,914
23,075
Misemo yenyewe ni hii niliyobold red

Person1:Thank you for your help.
A) Person2: You are welcome.

Person1: I got A in Maths
B) Person2: Good for you.



Msemo
A, nafikiri kumjibu hivyo person1, inamaanisha unataka aendelee kuwa na shida ili arudi tena umsaidie. Kwa nini usitafutwe msemo ambao utamwimiza person1 atafute njia mbadala ya kutatua shida/tatizo lake mwenyewe muda mwingine?

Msemo B, Ukimjibu person1, nafikiri unakuwa unaonyesha kutopendezewa kwake kupata hiyo A ktk maths. Kwa nini usitumike msemo wa I am happy for you.

Dokezo: kiingereza changu cha kuungaunga/sio cha kitaalamu.Hivyo wakati mnanisaidia kunifafanulia misemo hii zingatia hili dokezo.

Nawasilisha WanaJF wa lugha.
 
Nadhani wote Mmeisharudi kutoka Igunga, naombei msaada wenu wa misemo hiyo hapo juu.
 
Samahani kwa kuchelewa...
Hiyo ya kwanza maana yake: nimefurahi kukusaidia na kama utakua na shida tena usisite kuja kwangu nitakusaidia tena. Huwezi kumwambia mtu nimekusaidia ila ukiwa na shida tena tatua mwenyewe... kama ukitaka unaweza kutumia neno "pleasure" badala ya "you are welcome".
Ya pili nayo unasema: ni vizuri sana kama ilikua hivo. kweli hata mimi naona ni kama unasema ni vizuri kwako ila sio vizuri kwangu. hapa pia unaweza kusema "lucky you!" au more simply "congrats!, well done".
 
Uwe mwangalifu pia kwa sababu siku hizi watu wameanza sana kutumia misemo (idioms) za Kimarekani ambazo katika Kiingereza chetu cha Malkia tulikuwa hatukitumii sana; hata Waingereza wenyewe wakati mwingine wanapta shida na wameanza kumezwa na misemo hii ya Kimarekani. Hilo ni angalizo tu.

nilirudi kwenye maswali yako:

1: "You are welcome" ni mmoja wa majibu ambayo kwa bahati mbaya sana umepotezwa maana katika Kiswahili. Nimesikia watu mara nyingi wakiambia "asante" wanajibu "karibu"! Neno "karibu" tunavyolitumia sisi halitafsiri kwa usahihi neno la "You are welcome" inapotumiwa katika kiingereza kujibu shukrani ya mtu. Msemo unaokaribiana na huo ni kule kuitikia kwa Wasukuma "Wabeja kulumba" yaani - na ukienda Mwanza na sehemu nyingine watu bado wanaitikia hivyo - asante kushukuru. Yaani, mtu anatambua na kuonesha kufurahiwa na wewe kushukuru.

Kwa hiyo mtu akikujibu "You are welcome" hamaanishi anakukaribisha - jinsi inavyosikika kwa mzungumzaji wa Kiswahili. Anamaanisha ameridhika umeshukuru. Haihusiani na kumwambia mtu "karibu".

"Good for you" ni sawasawa kimaana na pendekezo lako "I'm happy for you" na wengine wanatumia maneno hayo kwa kubadilishana. Lakini "Good for You" wakati mwingine inatumiwa kama kejeli. Ni vizuri kusikiliza "tone" ya mtu anayesema.
 
Tafadhali ujue kwamba maneno ninayoyataja chini hutumiwa kama tafsiri ya kutosha la "you are welcome"

Haidhuru

Yote mamoja tu
Potelea mbali
Si neno
Hapana neno
Usifikiri
Bila samahani
Si kitu
Kwa furaha!
Ni furaha yangu

"Good for you" ndio ina maana ya "hongera" au wakati mwingine unaweza ukawa msemo wa kidhihaki.

 
Back
Top Bottom