Misamaha ya kodi na mgawo wa umeme vya kwamisha TRA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misamaha ya kodi na mgawo wa umeme vya kwamisha TRA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jun 29, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,806
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Misamaha ya kodi na mgawo wa umeme vyakwamisha TRA
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Tuesday, 28 June 2011 20:26
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Mussa Juma, Arusha
  Mwananchi

  MISAMAHA mikubwa ya kodi na mgawo wa umeme unaoendelea nchini, ni miongoni mwa vikwazo vinavyosababisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kushindwa kukusanya kodi kwa kiwango kikubwa.Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitillya, aliyasema hayo juzi wakati wa kusaini makubaliano ya kusaidiwa na Mamlaka ya Mapato Norway (NRA), kuboresha ukusanyaji mapato.

  Kitillya alisema bado misamaha ya kodi ambayo inatolewa kwa kampuni na taassisi mbalimbali ni mikubwa, hivyo kuathiri ukusanyaji mapato.Alisema hivi sasa misamaha ya kodi imefikia asilimia 2.5 ya pato la Taifa (GDP), tofauti na nchi za Kenya na Uganda ambako ni asilimia moja ya pato lao.

  Pia, Kitillya alisema tatizo la mgawo wa umeme na kutokusanywa kodi ipasavyo kwenye kampuni kubwa kama za madini, gesi na mafuta inachangia mapato kuwa kidogo tofauti na nchi nyingine.

  Alisema kutokana na mazingira hayo, TRA imesaini makubaliano na NRA, ili wafanyakazi wake wajengewe uwezo katika ukusanyaji mapato, hasa ukaguzi na uwazi katika ukusanyaji na ulipaji kodi.

  "Kama mnavyojua sasa Tanzania tunaelekea kwenye miradi mikubwa ya kuchimba gesi, mafuta na madini, hivyo ni muhimu wafanyakazi wa TRA kuwa na uelewa mkubwa wa kukusanya kodi kwa kampuni kubwa," alsiema Kitillya.
  Awali, Mkurugenzi wa NRA, Svein Kristensen, alisema inawezekana Tanzania ikakusanya kodi kubwa iwapo wafanyakazi wa TRA na Watanzania watakuwa wazi na kushirikiana.

  Kristensen alisema Norway yenye watu chini ya milioni tano, imekuwa ikukusanya kiwango kikubwa cha kodi na kimefikia kuchangia asilimia 42.8 ya pato la taifa hilo.Pia, hafla ya kusainiwa makubaliano hayo ilihudhuriwa na Balozi wa Norway nchini, Ingumu Klepsvik.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,806
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  Kitilya na wewe mwenyewe ni tatizo kubwa katika ukusanyaji wa mapato kwa mfani ulishindwa kukusanya kodi ya shilini bilioni 500 baada ya Airtel kuinunua Zain. Umekuwa mstari wa mbele kuifanya TRA kama kitengo cha chama cha magamba na kumshupalia Dr Slaa badala ya kufuatilia wakwepa kodi wa kubwa wanaoikosesha nchi mapato ya mabilioni . Umekuwa kimya mno! kuhusiana na misamahama mikubwa ya kodi inayozidi kuongezeka bila kuishauri Serikali ifute misamaha hiyo hasa kwa makampuni ya nje yakiwemo yale yanayochomba madini. Kazi ya kuiendesha TRA imeshinda na hii siyo siri.
   
 3. MANI

  MANI Platinum Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,412
  Likes Received: 1,871
  Trophy Points: 280
  Wameongeza gharama za kuagiza magari kwa walalahoi ndio wanakoweza kuwakamua hao wengine hawagusiki !
   
Loading...