Misamaha ya kodi haina ulazima kwa Tanzania, ndio sababu ya kuwakaba raia wa chini kwa tozo

OEDIPUS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
243
500
Misamaha ya kodi mara zote huwa ni kwa jili ya wawekezaji ambao misamaha hiyo husababisha mapato mengi kupotea na kwenda kumkaba asiye na kitu, ambaye ni mwananchi wa chini kutoa tozo, ushuru, ada nk. Sababu wanayosema ya kutoa msamaha wa kodi ni kuvutia uwekezaji, sababu ambayo ni mfu kwa kuwa tuna vitu vingi vya kuvutia wawekezaji mbali na msamaha wa kodi.

KUWAVUTIA WAWEKEZAJI
Wawekezaji huvutiwa na vitu vingi, ikiwemo miundo mbinu, Malighafi na Urahisi wa wafanyakazi(Cheap labour) kwa sisi watanzania, Cheap Labour ipo, malighafi zipo, miundo mbinu ndio kidogo ya kurekebishwa na kuweka sawa ili muwekezaji afanye biashara zake, mbali na yote hayo sisi tumeona kutumia Msamaha wa kodi kama kigezo hali ambayo inazidi kuwaumiza wananchi, mathalani wanafanya kazi kwa maslahi mabovu nk

Aidha kwa baadhi ya bidhaa, sisi ni WAMILIKI pekee, ‘Monopoly’ I.e Tanzanite, kwa eneo hilo ilibidi tupige kodi tunavyoweza badala yake tunatoa misamaha ya kodi eneo hilo na kwenda kumbana mwananchi kwa tozo ya miamala

Aidha biashara kubwa kama za madini, mawasiliano nk zinaingiza fedha nyingi na kwa nchi zinazoendelea biahsara hizi zinafaida kubwa, Fikiria muwekezaji wa madini anapewa ‘grace period’ na msamaha wa kodi… halafu mtu anyelipwa Tsh. 100,000 kwa mwezi anakumbana na tozo kibao.

MWANANCHI WA CHINI ANALIPA SEHEMU KUBWA SANA
Wananchi wa chini hawana uwezo wa kubargain na serikali lakini wanalipa sehemu kubwa ya vipato vyao kiasi ambacho wanakereka na kuumizwa na maisha yao. Kwa wale wawwekezaji wakubwa ambao mathalani anaweza kudaiwa kodi Tsh. Bilioni 300 anauwezo wa kukaa mezani na kubargain ambapo ndipo serikali yetu inapoteza mapato

Sioni haja ya mwananchi wa chini kukumbana na mrundikano wa tozo, huku wafanyabiashara wakubwa wakitamba kwa misamaha, grace periods, na wakiwa na watumishi wasiowalipa maslahi mazuri. Inahitajika nia ya dhati ya kuweka sawa katika kipengele hiko ili kama nchi tupate maslahi kwenye vyetu tulivyonavyo

Signed, OEDIPUS
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom