Misamaha ya kodi: Chanzo cha kumong'onyoa uzalendo wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misamaha ya kodi: Chanzo cha kumong'onyoa uzalendo wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasheshe, Jun 7, 2009.

 1. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ndugu zangu,

  Kwa mawazo yangu kama kuna kitu kinapunguza sifa/nguvu za mtu kuwa na uzalendo kamili ni huu ugongwa wa msamaha wa kodi.

  Kwa maoni yangu wawakilishi wa wananchi ndio watu ambao wanatakiwa wapewe treat ambayo ni sawa kabisa na wananchi wajue machungu na matamu ya wanaowawakilisha.

  Kwa muda mrefu sielewi ni kwa nini mwakilishi wa wanachi awe-exempted na kodi ya namna yoyote ile.

  Nionavyo mimi exemption ya kodi ni ulaghai wa serikali kudanganya kwamba watu fulani hawalipwi hela nyingi kumbe wanalipwa fedha nyingi.

  Lakini muhimu pia ukitaka kila mwananchi apende na kutetea nchi yake wakati wote hakikisha analipa kodi.

  Asitokee mwananchi yeyote yule nchini asilipe kodi, alipe kulingana na uwezo wake. hata kama ni sh. tano kwa mwezi lakini aweze kusimama mbele ya raia wenzake na kusema nimelimia sh. tano kwa taifa langu, hivyo na-demand kuletea maji, afya na kadhalika.

  Mwisho, ninakerwa na msamaha wa kodi wa namna yeyote ile.
   
 2. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi naashangaa hapo nchini kwetu kusikia kitu kinaitwa kusamehe kodi. Hata kule katika dini (mimi si mjuzi wa hayo) nasikia pia watu walikuwa wakilipa kodi. Na kwetu ndio hiyo Zakaat. Sasa hapa leo unasema unamsamehe mtu kodi - vyereje?
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Sasa mimi raia wa kawaida nitakuwa na hamasa gani kulipa wakati wabunge, mawaziri, majaji wanapeta hawalipi kodi???

  Uzalendo wangu utatoka wapi??

  Angeaza JK tukajua 2008 amelipa kodi kiasi gani!
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Misamaha ya kodi ni mwanya mkubwa wa rushwa, futa yote anaetaka kuwekeza alipe kodi, anaetaka kutangaza dini alipe kodi nk nk
   
 5. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,741
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Misamaha ya kodi nadhani ilikua ni janja ya viongozi wa miaka hiyo ya nyuma. eti wafanyakzi wa serikali,madaktari etc. wanakuwa na exemption kwa sababu gani?????????kodi ni jukumu la kila mwananchi mwenye kipato kiwe kikubwa au kidogo kwani unatakiwa kulipa kadiri ya mapato yako.Hapa ndipo rushwa ilipozaliwa kwa nguvu zote.Watu wote walipe kodi hata kama una nyadhifa ya kufika mbinguni lipa kodi period!!
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Tuko pamoja, sioni mantiki ya kusamehe kodi kwa taasisi yoyote na kwa raia yeyote.

  Lazima kila mtanzania aweze kusimama mbele ya mwenzake aseme mimi nimechangia nchi yangu kiasi hiki cha kodi.
   
 7. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145

  Mzalendohalisi,

  Nakupata, wewe kweli mzalendo halisi!!! very strong point!
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Tunaomba akina Zitto na Dr. Slaa watueleze kwa nini huwa hawawi wakali kwenye hili?
  Na watueleze kweli kuna haja ya kuwa na misamaha ya kodi?

  Ni kwa nini? Kusamehe kodi kuna maslahi gani kama sio lugha ya ulaghai tu?
   
 9. M

  Maskini Mimi Member

  #9
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This will be the best thing if achieved, as it will be in line with Cannons of taxation 'fairness' - everyone should pay tax.

  Nchi za wenzetu hata marais wanatakiwa wafile tax returns and declare income and pay resultant tax na hapo tutpata kuwakamata viongozo amabo awana evade tax kama yalivyotokea UK hivi karibuni (though not directly related with Tax, wao waliwaibia wananchi kwa kudai matumizi yao binafsi)

  Watu wote, biashara zote, taasisi zote lazima zilipe kodi ili kuondoa uonevu.

  Kama wakitokea wabunge watakaoweza kusubmit hilo suala bungeni na likapitishwa itakuwa ni jambo kuu Tanzania.

  Lakini tukumbuke wazi kwamba wabunge wetu wataliona hilo ni jambo gumu kwao (they are selfish) kwani sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 inasamehe kodi kwa wabunge wote pindi wanapolipwa GRATUITY mwishoni mwa kipindi (5 years). Refer EXEMPT AMOUNTS - paragraph 1 (s) of the Second schedule to the Income Tax Act, 2004.

  Vile vile raisi halipi kodi juu ya mshahara wake na marupurupu yote yanayotokana na yeye kuwa raisi!! Refer EXEMPT AMOUNTS - paragraph 1 (a) of the Second schedule to the Income Tax Act, 2004.
   
 10. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Tunaelekea kipindi cha uchaguzi hawa wanaojiita wabunge mahiri wa upinzani wakiwabana Spika na Rais... hili linaweza kutendeka.

  Kwa nini? Kwa kuwa sheria hiyo ilipitishwa kipindi ambacho wote hawakuwa kwenye vyeo walivyo navyo leo, na kumbuka kwamba wote wanapenda warudi kwenye viti vyao baada ya uchaguzi.

  KODI LAZIMA ILIPWE NA KILA RAIA na kiwe kigezo kikubwa cha kupenda Nchi Yetu.

  Kodi ni kichocheo kikubwa cha uzalendo wetu na kitafanya raia wote walioko vijini wafuatilia mapato na matumizi ya halmashauri zao.
   
 11. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Uzalendo wangu uko pale pale.


  Kasheshe,
  Kwa mantiki hiyo hizi sifa na nguvu 'kamili' za Uzalendo wangu lazima uwe na, wa-kulipa kodi. Ninakubaliana.
  Kwa mantiki hiyo hiyo bila hivyo(kulipa kodi) siwezi kuwa mzalendo 'kamili'?

  Hapo juu tunagongana!

  Na hawa watu ni wananchi hao hao au ni watu fulani tu?
  Fafanua...


  Kwa nini nipende Nchi yangu kwa masharti?

  Uhakiki gani huu unaozungumzia? Kuhakikisha kuwa tunapata huduma kwa mda mfupi anafanya nani, TRA?

  Ala kulli hali, kuna umuhimu wa kufanyia utafiti Misamaha hiyo unayozungumzia hususani umuhimu umekuwa kwa faida ya nani, misamaha hii huwa inakuja na wakati(dynamic) hivyo umuhimu wa kupitia na kufanya uhakiki wa faida zake na huko kumong'onyoa uzalendo wetu lazima ifanywe.

  Ndugu yangu, misamaha ya kodi itakuwepo, nafikiri mara nyingi huwa zinachangia pale kunapokuwa kuna kitega uchumi ambao unahitaji nguvu zote za dola,na udundulizaji wa hali ya juu ili kufanikisha azma hizo, za uwekezaji, huwa mara nynigi zinakuwa na faida maradufu na za mda mrefu.

  Misamaha itaendelea na Uzalendo wangu utaendelea.

  Ahsante
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Na hii sio rahisi watu wa kawida kupewa. Wanapewa walewale with access to the big shorts making those decisions. Ninakubaliana kabisa na wewe kuwa hili nalo laweza kuwa mwanya mkubwa wa rushwa. Misamaha yenyewe haiko very clear inatolewaje tolewaje kwa watu wa kawaida
   
 13. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kama hulipi kodi wewe sio mzalendo kamili wa Taifa letu, na kama unakwepa kodi wewe ni fisadi kwenye Taifa letu.
  Misamaha ya kodi mara nyingi imetolea kwa wawakilish, mawaziri, watumishi wa umma etc. Kibaya ni kwamba misamaha hiyo hiyo sio fair mfano na inakelezwa vibaya mfano mtumishi ana msamaha wa kuingiza gari. mwenye kuingiza VX msamaha utakuwa mkubwa kuliko mwenye kuingiza bajaji----> mwishowe ni kama ufisadi fulani hivi.  Well, kama hutoi kodi ni kitu gani kitakufanya uwe na complete ownership of project, fedha za umma, mashirika ya umma etc.  Swali unapokwenda kwenye hospital ya binafsi ukichajiwa 100,000/- kama huduma unakuwa na nguvu ya kudai huduma bora si ndio? basi ukitoa kodi kwa kadri ulivyojaliwa utakuwa na nguvu hiyo hiyo... hivyo utawala bora utadumishwa.

  Hakuna umuhimu wa kufanya utafiti wowote maana hata faida zinazopatikana kwa walengwa zinakuwa hazitendi haki...nakupa mfano... shirika la dini linaloingiza miradi ya bil 5. litakuwa na msamaha mkubwa kuliko zinaloleta bidhaa za million moja. Na mfanyakazi anayeingiza Range Rover atakuwa anapata msamaha mkubwa kuliko anayingiza corola. kwa nini isiwe... posho fulani kwa vyeo fulani mtu aamue mwenyewe anunue gari la gharama kwa uamuzi wake?

  In short misahama ya kodi haina faida... raia wote walipe kodi kulingana na uwezo wao and must be well calculated and with no discrimination of any nature. na zisiwe za kuwafaidisha wajanja!
   
 14. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Naona utafiti mbadala hapo.
  Mie bado Mzalendo.
  Ahsante kuelimishana.
   
Loading...