Misamaha ya kisiasa Utamaduni mpya uliojaa ghiliba, uongo na usanii

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,552
Siasa zetu zinazidi kupoteza hadhi zinazidi kujidhihiri namna zisivyo halisi zilizojaa uchimvi na Siasa za kutukuza na kusifu..! misamaha ya kisiasa si halisi bali ni makubaliano
Ni biashara
Ni maslahi
Ni viapo
Ni mikataba
na 50/50 win win situation.

Mara nyingi chochote kinachoenda hewani masikioni mwa wote ni matokeo tu..... makubaliano na maandalizi yalikwisha fanyika huko nyuma ya pazia!
kama kwenye vikao vya ndugu tu ama wanandoa hutengeneza utaratibu na makubaliano ya kuombana radhi basi wengine ni mfumo huohuo wanafuata.. .

Hakuna hata mmoja anakurupuka kutoka kwake na kuwasha gari moto kwenda moja kwa moja kumfuata anayemhitaji ili wamalizane bila kufanya mawasiliano kwanza labda iwe kumalizana kubaya na si kufanya patano ...

Misamaha ya kisiasa ni vigezo na masharti
Nipe nikupe
Umeshika makali nimeshika mpini
Nikubalie hiki upate hiki
Nikatalie hili ukose haya.
Misamaha ya kisiasa haikuanza jana au juzi ni ya muda mrefu lakini kamwe haikuwahi kutangazwa... hadhira iliona tu matokeo mifano ni mingi.... maji ya shingo, maji ya shingo maji ya shingo.

Mirija inapokatwa
Mabomba yanapozibwa
Connection zinapokatishwa
Betri zinapochomolewa waya
Na makaburi yenye uvundo yanapoanza kufukuliwa mzee huna jinsi utaomba Pooh! asikudanganye mtu wanasema hakuna mkate mgumu mbele ya chai. Unafika mahali na kuchagua upande wenye maslahi binafsi zaidi!.

Ukiona nyani Mzee ujue kakwepa mishale mingi mshale utakaompata hautakiwa na madhara makubwa kwake, kwakuwa hana cha kupoteza tena Misamaha ni ya wavulana kwakuwa bado wanaota ndoto nyingi.... halisi na za kufikirika.

Lakini wamepigwa kelebu... kofi la aibu japo mwisho wa siku unaangalia unapata nini kwenye nini... ..

Mlevi mmoja alisikika akisema eti "Boss hanuniwi"
 
Mungu atujarie tumalize kipindi hiki kigumu kuwahi kutokea.
Siasa zetu zinazidi kupoteza hadhi.... Zinazidi kujidhihiri namna zisivyo halisi .... Zilizojaa uchimvi... Siasa za kutukuza na kusifu
Misamaha ya kisiasa si halisi bali ni makubaliano
Ni biashara
Ni maslahi
Ni viapo
Ni mikataba
Na 50/50 win win situation

Mara nyingi chochote kinachoenda hewani masikioni mwa wote ni matokeo, makubaliano na maandalizi yaliyokwisha fanyika huko nyuma ya pazia
Kama kwenye vikao vya ndugu tu ama wanandoa hutengeneza utaratibu na makubaliano ya kuombana radhi.. Wengine ni mfumo huohuo wanafuata...

Hakuna hata mmoja anakurupuka kutoka kwake na kuwasha gari moto kwenda moja kwa moja kumfuata anayemhitaji ili wamalizane bila kufanya mawasiliano kwanza.... Labda iwe kumalizana kubaya na si kufanya patano
Misamaha ya kisiasa ni vigezo na masharti.. Nipe nikupe... Umeshika makali.. Nimeshika mpini.... Nikubalie hiki upate hiki... Nikatalie hili ukose haya....

Misamaha ya kisiasa haikuanza jana au juzi... Ni ya muda mrefu lakini kamwe haikuwahi kutangazwa... Hadhira iliona tu matokeo... Mifano ni mingi
Maji ya shingo... Maji ya shingo... Maji ya shingo....
Mirija inapokatwa
Mabomba yanapozibwa
Connection zinapokatishwa
Betri zinapochomolewa waya na makaburi yenye uvundo yanapoanza kufukuliwa... Mzee huna jinsi... Utaomba Pooh asikudanganye mtu... Wanasema hakuna mkate mgumu mbele ya chai.... Unafika mahali na kuchagua upande wenye maslahi binafsi zaidi.....!!!!

Ukiona nyani Mzee ujue kakwepa mishale mingi... Mshale utakaompata hautakiwa na madhara makubwa kwake kwakuwa hana cha kupoteza tena..... Misamaha ni ya wavulana kwakuwa bado wanaota ndoto nyingi... Halisi na za kufikirika....!!!!!!

Lakini wamepigwa kelebu... Kofi la aibu... Japo mwisho wa siku unaangalia unapata nini kwenye nini....!!!! Mlevi mmoja alisikika akisema eti BOSS HANUNIWI.....!!!!
 
Kwa mara ya kwanza toka nimekuwa na kuangalia Siasa zetu awamu hii kuna kila kihoja,ama zaidi ya vihoja,hata mm nadhani pana ukweli kiasi fulani kama haya maigizo wanayofanya wanakuwa washakubaliana,lkn najiuliza hii fomula ya wapi , kwani wakiombana msamaha lazima awatangaze wenzake au aweke na makamera kama kaombwa msamaha, hawa watu sijui wa wapi hawa, awam yao ipite tu maana kila iitwapo leo wanatuletea vichefu chefu
 
Kwa mara ya kwanza toka nimekuwa na kuangalia Siasa zetu awamu kuna kila kihoja,ama zaidi ya vihoja,hata mm nadhani pana ukweli kiasi fulani kama haya maigizo wanayofanya wanakuwa washakubaliana,lkn najiuliza hii fomula ya wapi , kwani wakiombana msamaha lazima awatangaze wenzake au aweke na makamera kama kaombwa msamaha, hawa watu sijui wa wapi hawa, awam yao ipite tu maana kila iitwapo leo wanatuletea vichefu chefu
Iko namna hii wadanganyika wengi bado maBwege nowdays watawala wamewabatiza majina mapya wanaitwa wanyonge Sasa kwakuwa uchaguzi umekaribia na hao waomba misamaha ina wajinga wengi wapiga kura kwa namna waomba misamaha walivyo mchana stono manake watu wa waomba misamaha hawatapigia kura stono na kama unavyojua hali ngumu aliyonayo muombwa msamaha kwenye sanduku la kura hana namna zaidi yakubaki mamlakani kwa kutumia dola sasa analazimisha misamaha angalau wajinga wa waomba misamaha waone Sasa wamepata na kura kwa stono naamini umeelewa sasa
 
Iko namna hii wadanganyika wengi bado maBwege nowdays watawala wamewabatiza majina mapya wanaitwa wanyonge Sasa kwakuwa uchaguzi umekaribia na hao waomba misamaha ina wajinga wengi wapiga kura kwa namna waomba misamaha walivyo mchana stono manake watu wa waomba misamaha hawatapigia kura stono na kama unavyojua hali ngumu aliyonayo muombwa msamaha kwenye sanduku la kura hana namna zaidi yakubaki mamlakani kwa kutumia dola sasa analazimisha misamaha angalau wajinga wa waomba misamaha waone Sasa wamepata na kura kwa stono naamini umeelewa sasa
Nimekuelewa Mkuu , hapo sina swali wanyonge sie hahaha dadekiiii
 
Aliwapatanisha bashite na marehemu wa clouds media mbele ya mseveni lakini sikuwahi kuona wameelewana mpaka kifo kilipomkuta yule boss wa clouds media, sasa kwa huu usanii wanaofanya sasa hivi sijui kama utaleta matunda
ukiona nyumba yako inasambaratika lazima utumie njia yyte ile kuirudisha isimame, ni jambo la kawaida kusamehe, mbna cdm iliwasamehe Kube na Komu, uajabu unakuja pale ambapo mtu anafanya kinyume na ushabiki wetu kisiasa ndo maana tunaona maajabu.
 
Unapomuita mkuu wa chama chako cha siasa mshamba na akasikia ukitamka neno hilo, wewe uliyemtusi una kila sababu ya kumuomba msamaha.

JK alichukulia poa tu upuuzi kama huu lakini sio kila mtu anao moyo wa upole na kuchukulia poa tu.
 
Siasa zetu zinazidi kupoteza hadhi zinazidi kujidhihiri namna zisivyo halisi zilizojaa uchimvi na Siasa za kutukuza na kusifu misamaha ya kisiasa si halisi bali ni makubaliano ni biashara ni maslahi ni viapo ni mikataba
na 50/50 win win situation.

Mara nyingi chochote kinachoenda hewani masikioni mwa wote ni matokeo, makubaliano na maandalizi yaliyokwisha fanyika huko nyuma ya pazia kama kwenye vikao vya ndugu tu ama wanandoa hutengeneza utaratibu na makubaliano ya kuombana radhi wengine ni mfumo huohuo wanafuata.

Hakuna hata mmoja anakurupuka kutoka kwake na kuwasha gari moto kwenda moja kwa moja kumfuata anayemhitaji ili wamalizane bila kufanya mawasiliano kwanza labda iwe kumalizana kubaya na si kufanya patano

Misamaha ya kisiasa ni vigezo na masharti nipe nikupe umeshika makali nimeshika mpini nikubalie hiki upate hiki nikatalie hili ukose haya.Misamaha ya kisiasa haikuanza jana au juzi ni ya muda mrefu lakini kamwe haikuwahi kutangazwa hadhira iliona tu matokeo mifano ni mingi maji ya shingo, maji ya shingo maji ya shingo.

Mirija inapokatwaMabomba yanapozibwa Connection zinapokatishwaBetri zinapochomolewa waya na makaburi yenye uvundo yanapoanza kufukuliwa mzee huna jinsi utaomba Pooh! asikudanganye mtu wanasema hakuna mkate mgumu mbele ya chai. Unafika mahali na kuchagua upande wenye maslahi binafsi zaidi!.

Ukiona nyani Mzee ujue kakwepa mishale mingi mshale utakaompata hautakiwa na madhara makubwa kwake, kwakuwa hana cha kupoteza tena Misamaha ni ya wavulana kwakuwa bado wanaota ndoto nyingi halisi na za kufikirika.

Lakini wamepigwa kelebu kofi la aibu japo mwisho wa siku unaangalia unapata nini kwenye nini Mlevi mmoja alisikika akisema eti "Boss hanuniwi"
Wataalamu wa Siasa watuambie hii ndio aina gani ya Siasa? Enzi za Mwl. Nyerere ilikuwa ni Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, kwa Mwinyi Siasa za Soko Huria, kwa Mkapa Siasa za utandawazi na ubinafsishaji, Kwa Kikwete, Siasa za demokrasia na utawala bora. Hii ya sasa hizi siasa za mara kupigiwa simu usiku wa manane, mara Nape, January, William sijui wamepiga magoti, n.k. ni siasa gani?
 
Back
Top Bottom