Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,632
- 697,794
Siasa zetu zinazidi kupoteza hadhi zinazidi kujidhihiri namna zisivyo halisi zilizojaa uchimvi na Siasa za kutukuza na kusifu..! misamaha ya kisiasa si halisi bali ni makubaliano
Ni biashara
Ni maslahi
Ni viapo
Ni mikataba
na 50/50 win win situation.
Mara nyingi chochote kinachoenda hewani masikioni mwa wote ni matokeo tu..... makubaliano na maandalizi yalikwisha fanyika huko nyuma ya pazia!
kama kwenye vikao vya ndugu tu ama wanandoa hutengeneza utaratibu na makubaliano ya kuombana radhi basi wengine ni mfumo huohuo wanafuata.. .
Hakuna hata mmoja anakurupuka kutoka kwake na kuwasha gari moto kwenda moja kwa moja kumfuata anayemhitaji ili wamalizane bila kufanya mawasiliano kwanza labda iwe kumalizana kubaya na si kufanya patano ...
Misamaha ya kisiasa ni vigezo na masharti
Nipe nikupe
Umeshika makali nimeshika mpini
Nikubalie hiki upate hiki
Nikatalie hili ukose haya.
Misamaha ya kisiasa haikuanza jana au juzi ni ya muda mrefu lakini kamwe haikuwahi kutangazwa... hadhira iliona tu matokeo mifano ni mingi.... maji ya shingo, maji ya shingo maji ya shingo.
Mirija inapokatwa
Mabomba yanapozibwa
Connection zinapokatishwa
Betri zinapochomolewa waya
Na makaburi yenye uvundo yanapoanza kufukuliwa mzee huna jinsi utaomba Pooh! asikudanganye mtu wanasema hakuna mkate mgumu mbele ya chai. Unafika mahali na kuchagua upande wenye maslahi binafsi zaidi!.
Ukiona nyani Mzee ujue kakwepa mishale mingi mshale utakaompata hautakiwa na madhara makubwa kwake, kwakuwa hana cha kupoteza tena Misamaha ni ya wavulana kwakuwa bado wanaota ndoto nyingi.... halisi na za kufikirika.
Lakini wamepigwa kelebu... kofi la aibu japo mwisho wa siku unaangalia unapata nini kwenye nini... ..
Mlevi mmoja alisikika akisema eti "Boss hanuniwi"