Misafara ya viongozi wa Serikali ni manyanyaso kwa watumia barabara

Misafara ya wenzetu inatumia precise timings kwa kutumia GPS, msafara ukifika Bagamoyo, wanaona time calculations msafara utafika Mbezi saa ngapi, then kabla ya just 5 minutes before ndipo barabara zinafungwa. Hizo GPS kwenye hizo SUV zenu za nini?.
 
Hii misafara aisee acha tu kuna siku nilipewa adhabu ya kimya kimya ila nilishika adabu,kulikuwa na msafara nikaegesha garimsafara upite nikaanza kuufukuzia nyuma kwa kasi ili niepuke jam za barabara kwa advantage ya huo msafara kufika kama kilometa moja gari lililokuwa mwisho wa msafara likakaa pembeni kidogo likapunguza mwendo kabisa nikalipita akaanza kunifuata nyuma kwa spidi ya hatari nikajua kimewaka nikiwasha indicator ananibana nisikate ikabidi ninyooshe nao wanapokwenda nilitokea moshi nikapelekwa hadi karibia na makuyuni mafuta yakaniishia na mie nilikuwa naishia bomang'ombe ,jamaa wakajua adhabu inanitosha baada ya kuona gari kama inamiss miss wakajua ni wese hilo limekata ndiyo wakanipita ,sitakaa nisahau lile tukio maisha
 
Wakati mnawekwa pembeni jamaa anaingia kuoga nyie mnakaa tu anywe chai ndo atoke sasa kwann wasichukue mfano wa nchi Jirani Burundi
 
Ni Ujinga Sana Mkuu, Hivi Unakaaje Zaidi ya Masaa Mawili Anapita Mtu na Mke Wake. Sjui Huu Upuuzi Utaishi Lini Wallah
Lakini si wanapita kasi tabu iko wapi?Wangejuwa wamepanda bulldozer nami ningemaindi
 
Hivi wewe unajua kuwa ikifungwa Nyerere road unapata option njia nyingine? Tena inajulikana kabisa siku fulani anakuja watafunga njia. Sasa unaenda Morogoro njia imefungwa uko katikati kuna njia mbadala utachepuka?
Mimi sikubaliani na yote hayo bali sitaki double standard kabisa wakati ule niltembea kwa miguu kutoka Posta hadi Kenyata Drive pale mbele ya Salender ndipo nikapata option ya Bodaboda, yaani jiji lilisimama bila sababu yoyote ile. Mimi ndo napinga hilo na hili la sasa
 
Back
Top Bottom