Misaada ya Lwakatare yakataliwa

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Baadhi ya vituo vya afya huko Bukoba vimekataa kupokea misaada ya vifaa vya afya toka kwa mbunge wao Bwana Lwakatare.

Wakieleza sababu za kukata kwao wamesema ni maelekezo toka serikalini.

Chanzo: Mwananchi
 
Last edited by a moderator:
Mbona habar yako imejifungafunga…?? Iweke sawa kwanza
 
Watakuwa hawajielewi hao!!tukianza kutengana kwa itikadi tutafikishana pabaya
 
Tunaweza kuzifahamu kazi za mbunge, kwa kuangalia kazi za Bunge, maana mbunge ni mwakilishi wa jimbo (wananchi) katika Bunge: “Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba hii” Ibara ya 63(2), pia na Ibara ya 64(1) inaelezea kazi za Bunge, juu ya kutunga sheria. Hivyo basi Mbunge, ni mwakilishi wa jimbo lake katika chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kina madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake.Hivyo kutoa misaada, kusalimia misiba na kuwatembelea wagonjwa si kazi za mbunge. Hizi zimo ndani ya wajibu wake yeye kama mwananchi katika jamii anayoishi. Hata asingekuwa mbunge, angetakiwa kufanya hivyo maana wananchi wote wanafanya hivyo.
 
Kazi ya mbunge siyo kutoa misaada kazi ya mbunge ni kuishauri serikali kupeleka maendeleo kwa wananchi.
Kuna mtu ambaye kazi yake ni kutoa misaada?

Au Misaada ni ubinadamu wa yoyote aliyenacho au mwenye uwezo au hata kujinyima ili kusaidia yule anayehitaji zaidi?

Au wewe unapotoa sadaka au kusaidia mtu ni moja ya kazi zako ?
 
Kazi ya mbunge siyo kutoa misaada kazi ya mbunge ni kuishauri serikali kupeleka maendeleo kwa wananchi.


Leo hii ndo unatuambia hilo??

Wakati ule mlipokuwa mnamsakama Mh Mnyika kuhusu matatizo ya maji na barabara Ubungo elimu hii haukuwa nayo?

Ficha upumbavu wako kidogo
 
Kazi ya mbunge siyo kutoa misaada kazi ya mbunge ni kuishauri serikali kupeleka maendeleo kwa wananchi.
Hamtaki misiba isipokuwa yenu tu, mikutano isipokuwa ya kwenu tu, kushukuru wananchi isipokuwa ninyi tu, kusaidia jamii ni ninyi tu, ...... Kusifia ni kila kitu chenu..... Sijui twendapi?
 
Kazi ya mbunge siyo kutoa misaada kazi ya mbunge ni kuishauri serikali kupeleka maendeleo kwa wananchi.

huko ndio kuchanganyikiwa!! Tanzania ujinga hautaisha na ndio maana ccm inachaguliwa.Bado mna mawazo ya kijinga sana. hivi mbunge wa upinzani akitoa misaada ya vitabu au madawa mkatae tu kwasababu ni mpinzani? i cannot imagine kama dunia hii ina watu wa aina hii serikalini.
 
Hawa wabunge waache usanii...lema na Nassari wameleta ambulance kwenye mikutano lakini hawajazikabidhi serikalini.
Halafu kwa nini hakuwasilisha huo msaada halmashauri ?
 
Nimesoma habari hii na kiukweli nimeona aibu sana ! Kuna taarifa kwamba kaimu mkurugenzi wa manispaa ya bukoba , richard mihayo alitimua mbio ili kukwepa lawama kutoka ' juu '
 
Hawa wabunge waache usanii...lema na Nassari wameleta ambulance kwenye mikutano lakini hawajazikabidhi serikalini.
Halafu kwa nini hakuwasilisha huo msaada halmashauri ?
Hivi kuna mtu wa kukuelewa wewe humu jf tena ? Wiki ijayo ndio kile chungu cha monaban kinavunjwa , sasa je utasalimika ? Maana wewe ni mmoja wa waliotafuna hela zake , mtapukutika wote kudadeki !
 
Back
Top Bottom