Misaada ya Lwakatare yakataliwa Bukoba

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Bukoba. Baadhi ya wakuu wa vituo vya afya na zahanati katika Manispaa ya Bukoba, wamegoma kupokea misaada kwa ajili ya wajawazito uliotolewa na Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare kwa madai ya kupewa maelekezo na Serikali.

Mbunge huyo mwishoni mwa wiki alikuwa akisambaza vifaa tiba katika vituo vya afya na zahanati, lakini wasimamizi walikataa kuvipokea, huku wengine wakikimbia wakidai walipewa maelekezo na viongozi wao kutovipokea.

Katika hali ya kushangaza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Richard Mihayo ambaye alikuwa katika msafara wa mbunge huyo alitoweka ghafla baada ya kufika Kituo cha Afya cha Zamzam, huku Kaimu mganga, Samwel Chaba akigoma kupokea vifaa hivyo.

Baada ya mkurugenzi kutoweka, mbunge huyo alilazimika kutelekeza vifaa hivyo kituoni hapo na kwenda Zahanati ya Kashai ambako Kaimu Msimamizi wa zahanati hiyo, Emmanel Luviga alikubali kuvipokea.

Katika Kituo cha Afya Rwamishenye vifaa hivyo vilipokewa na wauguzi waliogoma kuzungumza suala lolote.

Baada ya kufika Zahanati ya Kagemu, Msimamizi wake Glory Sailo aligoma kupokea vifaa kwa ajili ya mama wajawazito kwa madai ni maelekezo ya viongozi.

Hatua ya viongozi kuweka vikwazo kwenye upokeaji wa vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh3 milioni ililalamikiwa na Lwakatare aliyedai aliandika barua manispaa na kutoa nakala hadi ngazi ya mkoa, lakini Mganga Mkuu wa manispaa hiyo, Dk Hamza Mgula alisema hajui lolote kuhusu suala hilo.

Akizungumzia suala hilo, Mihayo alisema kwa kawaida vifaa vya tiba ni lazima vikaguliwe na mganga mkuu wa manispaa ili kuthibitisha ubora, hivyo haviwezi kupelekwa bila kuthibitishwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Kama imekataliwa misaada ya Mbunge,leta midaada yako ya SENENE tutaipokea huu ndo msimu wake
 
Hu

Huyo Mganga Mkuu Hamza Mugula alikuwa wapi? Na kama alikuwa hana taarifan je aliwasiliana na Mbunge Lwakatare ili ampelekee huo msaada aupokee na augawe kama ilivyokusudiwa? Hamza mugula acha ukuda wako wa TEMEKE Hospitali.
 
Ukweli wa habari hii ni uthibitisho kwamba ccm ni zaidi ya ubaya!
 
Bukoba. Baadhi ya wakuu wa vituo vya afya na zahanati katika Manispaa ya Bukoba, wamegoma kupokea misaada kwa ajili ya wajawazito uliotolewa na Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare kwa madai ya kupewa maelekezo na Serikali.

Mbunge huyo mwishoni mwa wiki alikuwa akisambaza vifaa tiba katika vituo vya afya na zahanati, lakini wasimamizi walikataa kuvipokea, huku wengine wakikimbia wakidai walipewa maelekezo na viongozi wao kutovipokea.

Katika hali ya kushangaza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Richard Mihayo ambaye alikuwa katika msafara wa mbunge huyo alitoweka ghafla baada ya kufika Kituo cha Afya cha Zamzam, huku Kaimu mganga, Samwel Chaba akigoma kupokea vifaa hivyo.

Baada ya mkurugenzi kutoweka, mbunge huyo alilazimika kutelekeza vifaa hivyo kituoni hapo na kwenda Zahanati ya Kashai ambako Kaimu Msimamizi wa zahanati hiyo, Emmanel Luviga alikubali kuvipokea.

Katika Kituo cha Afya Rwamishenye vifaa hivyo vilipokewa na wauguzi waliogoma kuzungumza suala lolote.

Baada ya kufika Zahanati ya Kagemu, Msimamizi wake Glory Sailo aligoma kupokea vifaa kwa ajili ya mama wajawazito kwa madai ni maelekezo ya viongozi.

Hatua ya viongozi kuweka vikwazo kwenye upokeaji wa vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh3 milioni ililalamikiwa na Lwakatare aliyedai aliandika barua manispaa na kutoa nakala hadi ngazi ya mkoa, lakini Mganga Mkuu wa manispaa hiyo, Dk Hamza Mgula alisema hajui lolote kuhusu suala hilo.

Akizungumzia suala hilo, Mihayo alisema kwa kawaida vifaa vya tiba ni lazima vikaguliwe na mganga mkuu wa manispaa ili kuthibitisha ubora, hivyo haviwezi kupelekwa bila kuthibitishwa.

Chanzo: Mwananchi

Vifaa kukaguliwa ubora na mganga mkuu ni jambo la maana na kwa kuhakikisha ubora ni muhimu hilo lifanyiwe kazi, swali langu ni, je kina mama wajawazito wanunuapo vifaa vya kujifungulia hukaguliwa na nanai?
 
Baadhi ya waganga wafawidhi wa vituo vya afya mjini Bukoba kituo cha zam zam wamekataa kupokea vifaa vilivyotolewa na mbunge wa cdm na mbunge wa cuf(viti maalum)

Hii tabia ni ya kijinga na uuwaji kwani mahospiali na vituo vya afya havina dawa na huduma ni finyu leo hii mganga anakataa kupokea msaada kisa vimetolewa na viongozi wa vyama vya upinzani?

Hii haikubaliki na huyu mganga inabidi ashughulikiwe
 
Baadhi ya waganga wafawidhi wa vitu vya afya mjini bukoba kituo cha zam zam amekataa kupokea vifaa vilivyotolewa na mbunge wa cdm na mbunge wa cuf(viti maalum) hii tabia ni ya kijinga na uuwaji kwani mahospiali na vituo vya afya havina dawa na huduma ni finyu leo hii mganga anakataa kupokea msaada kisa vimetolewa na viongozi wa vyama vya upinzani?hii haikubaliki na huyu mganga inabidi ashughulikiwe
Namwomba Magufuli awachuje baadhi ya watumishi waliokaa kisiasa. Kwanza amtoe mkuu wa mkoa, mkurungenzi na hao madaktari ili wasije kumharibia katika serikali yake. Ama sivyo itabidi wananchi wachukue mamlaka yao ya kufanya maandamano dhidi ya watu hawa wanahujumu harakati za maendeleo majimboni. Nawashauri wananchi Mara hii hao jamaa wakitaka tena kuleta ubazazi wao hebu waonesheni kazi, watumishi wapo ili kuisaidia jamii na si kuhujumu, kama wamechoka kazi waondoke waende kusiko na upinzani.
 
Kweli kabisa hili jambo haliwezi kukubalika kwa jamii,wana kataa kupokea huo msaada wakati kuna wagonjwa wanaambiwa wakanunue nje ya kituo na wagonjwa wengine hawana uwezo kifedha!
 
Bukoba. Baadhi ya wakuu wa vituo vya afya na zahanati katika Manispaa ya Bukoba, wamegoma kupokea misaada kwa ajili ya wajawazito uliotolewa na Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare kwa madai ya kupewa maelekezo na Serikali.

Mbunge huyo mwishoni mwa wiki alikuwa akisambaza vifaa tiba katika vituo vya afya na zahanati, lakini wasimamizi walikataa kuvipokea, huku wengine wakikimbia wakidai walipewa maelekezo na viongozi wao kutovipokea.

Katika hali ya kushangaza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Richard Mihayo ambaye alikuwa katika msafara wa mbunge huyo alitoweka ghafla baada ya kufika Kituo cha Afya cha Zamzam, huku Kaimu mganga, Samwel Chaba akigoma kupokea vifaa hivyo.

Baada ya mkurugenzi kutoweka, mbunge huyo alilazimika kutelekeza vifaa hivyo kituoni hapo na kwenda Zahanati ya Kashai ambako Kaimu Msimamizi wa zahanati hiyo, Emmanel Luviga alikubali kuvipokea.

Katika Kituo cha Afya Rwamishenye vifaa hivyo vilipokewa na wauguzi waliogoma kuzungumza suala lolote.

Baada ya kufika Zahanati ya Kagemu, Msimamizi wake Glory Sailo aligoma kupokea vifaa kwa ajili ya mama wajawazito kwa madai ni maelekezo ya viongozi.

Hatua ya viongozi kuweka vikwazo kwenye upokeaji wa vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh3 milioni ililalamikiwa na Lwakatare aliyedai aliandika barua manispaa na kutoa nakala hadi ngazi ya mkoa, lakini Mganga Mkuu wa manispaa hiyo, Dk Hamza Mgula alisema hajui lolote kuhusu suala hilo.

Akizungumzia suala hilo, Mihayo alisema kwa kawaida vifaa vya tiba ni lazima vikaguliwe na mganga mkuu wa manispaa ili kuthibitisha ubora, hivyo haviwezi kupelekwa bila kuthibitishwa.

Chanzo: Mwananchi
Siasa Ktk Afya Za WANANCHI!!! Kama Suala Hadi Mganga Mkuu Wa Mkoa Avikague Na Kuthibitisha Ubora Wake!!! Je, Kilichomzuia Kufanya Ni Nini!!?? Na Je TBS Wako LIKIZO!!!!??? Mganga Mkuu Ndiye AFISA Wa TBS!!!!!??? Na Why Huyo Mkurugenzi Asimwambie Mbunge Kabla Ya Yeye KUSHIRIKI Ktk Zoezi Hilo Na Baadae Kukimbia!!! HUO NDIO USANII WENYEWE!!!
 
Mkuu hamna logic katika hata kidogo. Kama kweli ishu ni ukaguzi mbona vituo vya Rwamishenye na Kashai hivi vifaa vilipokelewa tena kwa mikono miwili wakati shehena ni moja na watoaji ni walewale? hivyo vilivyopokelewa vilihakikiwa na nani wakati mhusika hayupo?. Hawa ndo majipu ambayo yanatakiwa kutumbuliwa, watendaji wa hivi ni tatizo kwa serikali ya hawamu hii na anatakiwa awatumbue. Hizi halmashauri zimeoza na kuna miungu ya ajabu yenye sura kama yangu na yako.
 
watanzania baadhi ya mambo ni ya hovyo sana. siasa mpaka kwenye uhai wa binadamu. hao waganga walipaswa kutimuliwa kazini mara moja...
 
Kwani kulikuwa na shida gani vifaa vipokelewe na kabla ya kutumika vikaguliwe? Na hayo maagizo kutoka juu kutopokea vifaa inamaana walikuwa na taarifa ya vifaa hivyo ila walikataa makusudi kuvipokea
 
Back
Top Bottom