Misaada na mkutano wa accra, ghana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misaada na mkutano wa accra, ghana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by waziri kalala, Sep 2, 2008.

 1. w

  waziri kalala Member

  #1
  Sep 2, 2008
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HIVI kweli tunazungumzia jinsi ya kutumia misaada ipasavyo? Mwaka huu 2008? Hii si aibu jamaa?

  YAMKINI ni utegemezi wetu wa msaad ndio uliotufukisha hapa tulipo. Kwa sababu hii Waafrika tunakuwa kama boya au pulizo-tukijazwa fedha za nje na wafadhili tunaona tunaoongoza vizuri na tumeletea nchi neema na mafanikio.

  Misaada ikikatwa balaa, njaa na mabaa. Haionekani pengine hii misaada ni nuksi.

  Ukiangalia misaada yenyewe wanapewa wanasiasa ambao biashara zao ni za miaka 5 tu au sana sana 10. Anayeahidiwa zawadi Na Mo Ibrahim ni Rais au waziri mkuu tu, je, mawaziri wengine katika kipindi chao wataacha kugawa msaada katika mafungu 3 yaliyo sawa. Moja la chama tawala; la pili lake na la tatu lifanye kazi msaada uliyoombewa kwayo!

  WAFADHILI waache kutudanganya hakuna nchi inayoendelea kwa misaada tu.

  Na wao wanajua wanachofanya ni ujinga na sisi tunajua wanachokifanya ni ujinga na wanatushangaa kuona tunakubali ujinga wao kwa hiyo wanajua kabisa kwamba bila wao sisi sio chochote sio lolote. Wanatudharau. Na ndio maana mzungu akiumi kidole ni sawa na Waafrika laki moja kufa! Na tunakubali hilo!!!

  UKWELI ni kwamba wakina Barricks, De Beers, AngloAmerican na wengine wakitulipa kitu kinachoeleweka hata haja ya msaada wa wazungu hatutakuwa nayo. In fact, Tanzania inaweza ikawasaidia hata wazungu. Lakini siamini kuwa ni CCM ambayo imeanza kuiuza nchi kwa Marekani ndiyo itakayoweza hili. Kwenda Marekani ni tangazo la wazi kwamba sisi bakuli mzee tupa makombo yako yakatusaidia. Tumeshindwa miaka hii, karne hii kujua watu wa kushikana nao kwa dhati nao sio wengine ila ni watu kama nchi za Kiarabu, Russia, Uchina, Venezuela na kadhalika. Mbeki chini keshawagutukia Wamarekeni ambao japo wanatoa kidunchu ukifananisha na nchi za Scandinavia lakini eti tunawaheshimu zaidi kuliko Denmark, Netherland, Norway, Ireland, Sweeden kwa hayo makombo yao. Hapa iko sababu watafiti fanyeni kazi yenu? Au kuna mtu anapenda kushangaa shangaa na taa za New York Tanzania????
   
 2. w

  waziri kalala Member

  #2
  Sep 2, 2008
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KWA tabia hivi hatuonekani kwamba sisi ni ' mala..' na tunajipeleka kwa mabwana anayetudanganya ana hela nyingi kumbe jamaa keshafilisika na sisi kwa kuwa mzubao japo tunashauriwa na wengine bado tunaamini hanazo kumbe hamnazo na pengine bwana huyo keshaubeba pia. Kimwana Tanzania nakuonea huruma mie kujipelka kwa Jilimarekani utaupata tu!
   
 3. w

  waziri kalala Member

  #3
  Sep 2, 2008
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KWA tabia hivi hatuonekani kwamba sisi ni ' mala..' na tunajipeleka kwa mabwana anayetudanganya ana hela nyingi kumbe jamaa keshafilisika na sisi kwa kuwa mzubao japo tunashauriwa na wengine bado tunaamini hanazo kumbe hamnazo na pengine bwana huyo keshaubeba pia. Kimwana Tanzania nakuonea huruma mie kujipelka kwa Jilimarekani utaupata tu!
   
Loading...