Misaada kwa waathirika wa mabomu gongo la mboto ilenge mahitaji yao! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misaada kwa waathirika wa mabomu gongo la mboto ilenge mahitaji yao!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Anold, Feb 22, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Toka eneo la gongo la mboto likumbwe na milipuko ya mabomu, tumeshudia watu mbalimbali wakitoa misaada kwa waathirika, naamini kila aliyekuwa ananyoosha mkono wake alikua na nia nzuri kuonyesha upendo wake kwa wahanga. Pamoja na ukweli kuwa msaada hauna masharti lakini ningeshauri wale wanaoguswa katika utoaji wazingatie mahitaji halisi ya watu hakuna sababu kabisa kutoa vitu kama biskuti na juice wakati wakati kuna mahitaji ya msingi yanakosekana, aidha kutokana na hali ya uaminifu kuwa jambo adimu ndani ya jamii yetu, kuna kila sababu ya kujiridhisha kuwa misaada hiyo inawafikia walengwa vinginevyo midaada hiyo itaangukia kwenye mikono ya wajanja. aidha vyombo vilivyopewa jukumu la kufanya tathimini vifanye kazi hiyo usiku na mchana kubaini wathirika ili misaada hiyo inayotolewa iwafikie walengwa kwa muda muafaka kuliko ilivyosasa kulundikana sehemu huku wahusika wakiendelea kuhangaika.
   
Loading...