MISA-Tanzania yatoa tamko kuhusu kufunguliwa kwa magazeti manne

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
10 Februari 2022

TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISATANZANIA), imepokea taarifa ya uamuzi wa serikali kuyafungulia magazeti manne, yaliyofungiwa kufanyakazi nchini kwa miaka kadhaa sasa.

Magazeti hayo binafsi ambayo leo yamepewa leseni na serikali kuanza tena kuchapisha na kusambaza magazeti nchini ni; Mawio, Mwanahalisi, TanzaniaDaima na Mseto.

Uamuzi wa huo ulitangazwa leo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, aliyesema kuwa serikali inataka kufungua ukurasa mpya wa mahusiano na vyombo vya habari nchini.

Aidha, Waziri Nnauye pia ameahidi kuunda kamati ya pamoja kati ya serikali na wawakilishi wa wanahabari ifanye kazi ya kupitia vifungu vya Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016, ili kupeleka marekebisho ya sheria hiyo bungeni.

Alipotafutwa na MISA-Tanzania, mmiliki wa gazeti la Mawio, Simon Mkina, aliipongeza serikali kwa uamuzi wa kuyafungulia magazeti hayo baada ya mchakato wa muda mrefu.

Msimamo wa MISA-Tanzania

MISA-Tanzania inaunga mkono nia ya serikali kufungua ukurasa mpya wa uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wa taarifa nchini, ikiwamo kutekeleza matakwa ya katiba ya nchi na mikataba na matamko ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Aidha, tunapongeza uamuzi wa kuongeza muda kwa waandishi wa habari kuwa na kiwango cha elimu ya Stashahada (Diploma), pamoja na kufungua milango kwa wadau wa tasnia ya habari, waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari nchini.

MISA-Tanzania inawataka wanahabari kujiendeleza kielimu, kuendelea kuchapa kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na maadili ya taaluma hiyo, katika kupasha habari kwa misingi ya kuelimisha, kuburudisha na kukosoa.

MISA-Tanzania inaahidi kushirikiana na serikali na wadau wengine kukuza na kuendeleza tasnia ya habari kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kuhusu MISA-Tanzania

MISA-Tanzania inalinda na kutetea uhuru wa habari, uhuru wa kuongea na haki ya kupata taarifa nchini Tanzania. Taasisi hii ni sehemu ya Media Institute of Southern Africa (MISA), ambayo ilianzishwa mwaka 1996,yenye matawi katika nchi nane za Kusini mwa Afrika (SADC) na Makao Makuu nchini Zimbabwe.

Lengo la MISA ni kusimamia uhuru wa kujieleza, haki ya kupata habari pamoja na uwepo wa tasnia ya habari iliyo huru na yenye uwakilishi mpana wa vyombo vya habari kusini mwa bara la Afrika.

PIA SOMA:

- Serikali yayafungulia magazeti ya MwanaHALISI, Tanzania Daima na Mseto
 
Hivi Mwaky-embe yuko mtaa gani? Sijamsikia kitambo!
Wajumbe walikula kichwa alienda kule akaanza kujitapa sijui yeye ana degree nne, anafundisha vyuo vikuu Saba, wajumbe wakasem huyu halali yetu wakabaki nae.

Ameshaisha ananyonyoka nywele vizuri zaidi kwa sasa.
 
Utasikia Nape for Presidency....2030...Hongera Nape na Serikali SSH
 
Back
Top Bottom