donniebrasco
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 887
- 771
Habari ndugu zangu, natumai mko salama.
Kwanza naomba niseme niliwahi kuwa mtumiaji wa mirungi Na pia mnywaji wa POMBE Na mvutaji wa SIGARA.
Naunga mkono upambanaji wa madawa ya kulevya kwa kudhuru afya zetu .
Tatizo langu ni kwamba vita kwenye mirungi imekuwa kubwa wakati madhara take ni madogo kuliko SIGARA kwa mujibu wa mashirika ya afya ya KIMATAIFA.
Takwimu zipo za madhara ya SIGARA Na POMBE ambazo ni za kusikitisha sana kulinganisha Na mirungi Na tukiwa wa kweli ndo tutafanikiwa.
Sisemi mirungi iruhusiwe la hasha ,lakini najiuliza ni taifa gani hili ambalo linakataza kitu chenye madhara kidogo Na kuacha vyenye madhara makubwa.
Hii ni link ambayo wanasayansi wa KIMATAIFA waliweka vilevi ishirini Na kupima madhara yake kimwili ,kijamii na ,utegemeaji wake. Mirungi ilikuwa ya mwisho kwenye athari mbili hizo kati ya tatu Na ikawa ya 17 kwenye athari nyingine wakati SIGARA Na POMBE vilionekana vikiwa Na madhara makubwa zaidi kwa mbali.
Legal intoxicant - Wikipedia
Ombi langu kwa wananchi Na serikali tushirikiane kupiga vita lakini pia tusiige tu vitu.
Kama vile ambavyo tumekataa kuwaiga Wakenya Na Wasomali kwenye matumizi ya mirungi kwa nini tuendelee kuwaiga wengine kuhalalisha SIGARA Na POMBE huu utakuwa unafiki mkubwa ambao mungu hatotusamehe nao.
Naheshimu sana mamlaka zinazohusika kutunga sheria msikae tu takwimu zipo pitisheni sheria kutokana na jamii yetu SIGARA Na POMBE ni hatari kwa taifa letu kuliko mirungi labda hata kuliko vilevi vingine vyote kwa pamoja.
Simamieni haki sio kupitisha sheria kwa kuiga au kwa pressure kutoka nchi nyingine.
Nawashukuru sana ndugu zangu.
Mungu ibariki Tanzania.