MIRATHI: Nimeshindwa pa kuanzia kufuatilia mirathi ya Mwanajeshi. Msaada tafadhali

Omwami Nshomile

Senior Member
Jan 26, 2015
132
28
Shikamoo wakubwa, hamjambo vijana?
Me nilifiwa na kaka yangu mwanajeshi tangu mwaka juzi, alikua akifanya kazi JKT Tabora. Baaada ya msiba tulipewa namba ya afsa moja wa jeshi hili ndo atatuelekeza jinsi ya kupata mirathi pamoja na pesa ziliko Benki kwenye account ya marehemu. Sasa yule afsa amegoma kutusaidia kwani tukipiga simu hapokei. Naomba msaada na maelekezo jinsi ya kushughulikia jambo hili.
Natanguliza shukulani zangu.
 
Nenda mahakamani kafungue shauri la mirathi. Pata muhitasari wa kikao cha wanandugu kukuruhusu ufungue mirathi na uwe msimamizi. Then nenda mahakamani uthibitishwe (kama hakutakuwa na pingamizi). Ni process ndefu kidogo, Muombe hakimu/au mwanasheria akuelekeze what next baada ya kuteuliwa/kuthibitishwa na mahakama.
 
Tayari tulishaenda mahakani nikathibitishwa. Baada ya hapo sijui cha kufanya. Tangu mwaka jana. Asante mkuu
 
Tayari tulishaenda mahakani nikathibitishwa. Baada ya hapo sijui cha kufanya. Tangu mwaka jana. Asante mkuu

Anza kukusanya mali za marehemu. Mali za`serikalini kama jeshini, peleka certified copies of the judgement jeshini kuthibitisha kuwa wewe ndie mteule wa mahakama wa mirathi hiyo, naamini watakupa utaratibu wa kudai mafao yake.
 
Naona ingekuwa bora kama ungefuata utaratibu rasmi kuliko kuanza kusumbuana na afisa mmoja mmoja. JKT sio taasisi ya wahuni, ina ofic zake na taratibu zake. Kwa hiyo b4 hujaenda mahakamani fanya maamuzi ya busara na sahihi kwenda HQ pale mikocheni ukapate utaratibu.
 
Shikamoo wakubwa, hamjambo vijana?
Me nilifiwa na kaka yangu mwanajeshi tangu mwaka juzi, alikua akifanya kazi JKT Tabora. Baaada ya msiba tulipewa namba ya afsa moja wa jeshi hili ndo atatuelekeza jinsi ya kupata mirathi pamoja na pesa ziliko Benki kwenye account ya marehemu. Sasa yule afsa amegoma kutusaidia kwani tukipiga simu hapokei. Naomba msaada na maelekezo jinsi ya kushughulikia jambo hili.
Natanguliza shukulani zangu.

Usimtegemee mwanadamu katika mambo yako, jeshi ni taasisi achana nae fuata utaratibu kikubwa wakati unafuatilia hakikisha una cheti cha kifo mkononi, taratibu zingine watakupa wajuzi wa mambo ila kwa uzoefu mdogo nadhani unatakiwa uwe muktasari wa kikao cha familia ambacho kimekupa jukumu hilo la kufuatilia mirathi. Pia ingia kwenye website ya RITA kuna maelezo kuhusu mirathi na njia mbadala kama inavyoeleza chini

Usimamiaji Mirathi
RITA husimamia mirathi ama kwa kuombwa kukifuatia kuteuliwa na mahakama, au kwa kuteuliwa moja kwa moja na mahakama. Katika masuala ya usimamiaji mirathi RITA uongozwa na sheria zifuatazo.
Taratibu / Mahitaji

Kwa maombi

  • Wasilisha barua ya maombi RITA au Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) katika wilaya inayohusika ambayo marehemu ana mali, ambapo DAS atajaza Fomu na kuwasilisha RITA akiomba Kabidhi Wasii Mkuu kusimamia mali za marehemu huyo. Mwombaji awe mtu ana cha kupoteza endapo mirathi haitasimamiwa.
  • Kabidhi Wasii Mkuu atachambua maombi na akiyaona yanafaa kwa kusimamia mali ataiomba mahakama imteue kuwa msimamizi wa mirathi husika vinginevyo atawashauri wahusika njia mbadala ya kuitumia.
  • Lipa ada ya mwanzo ya kusimamia kulingana na ukubwa wa mali .
Kuteuliwa moja kwa moja na mahakama
  • Mtu yeyote mwenye uchungu na mali za marehemu anaweza kuomba mahakama imteue Kabidhi Wasii Mkuu kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu anayehusika. Kabili Wasii Mkuu apatiwe nakala za maombi.
  • Mahakama itasikiliza maombi na kufanya uteuzi kama inavyoona inafaa.
Tanbihi: Baada ya kuteuliwa Kabidhi Wasii Mkuu atasimamia mirathi kwa kukusanya Mali, kulipa madeni na mwishoni kugawanya mali kwa warithi kulingana na sheria inayotumika au makubaliano ya wanaogawiwa, au kwa kufuata wasia, kama upo.

Naona ingekuwa bora kama ungefuata utaratibu rasmi kuliko kuanza kusumbuana na afisa mmoja mmoja. JKT sio taasisi ya wahuni, ina ofic zake na taratibu zake. Kwa hiyo b4 hujaenda mahakamani fanya maamuzi ya busara na sahihi kwenda HQ pale mikocheni ukapate utaratibu.
Asante mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom