Miraji 'Sheva' Athumani, amka inakusubiri dunia, wakati ndiyo huu

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,691
Yule mtoto kutoka kitaa chenye mishe mishe zake ndani ya Dar Es Salaam, Manzese pale kwa Madee Ali, pale ambapo Richard Mabala alipafanya setting ya kitabu chake cha 'Hawa the Bus Driver' ndipo hapo maskani kwa Miraji Athuman, winga wa mpira
.
Pengine ana historia kubwa sana juu ya soka lake, huenda kapitia mengi kwenye career yake, kuanzia Mwadui, Lipuli mpaka Simba, ila sote tunajua kuwa jamaa yupo kwenye peak, hata wanae wa Manzese wanajua hilo
.
Kwa level aliopo sasa Miraji tayari yupo kwenye spotlight ya mawakala barani Afrika, hii inatokana na ukubwa wa klabu anayocheza, mnapokaa nae kitaa mkumbusheni nini maana ya Professional football, mkumbusheni nini maana ya professionalism na professionality, hapo tu ndio tofauti ya Messi wa Argentina na Messi wa kubatizwa wa mitaani kwetu
.
Mwambieni Miraji kuwa mitaa haijawahi kuishiwa vipaji kama chake, mafundi wa kariba yake na moto kama wake, ni lazima yeye aje kujitofautisha
.
Mwambieni Miraji kocha wake Aussems aliyefukuzwa aliona kitu ndani yake, akamsogeza mpaka 10 sasa ile deep lying forward , Mwalimu alitaka universality, ndio sifa ya Professional lazima ukichafue namba nyingi, kule winga tayari katupa kitu, sasa kazi kwenye area 14 pale
.
Mwambieni Miraji kuwa umri alionao kwa soka la Ulaya amechelewa sana ila sio haba kupambana kucheza soka kubwa Afrika Kaskazini kwa Waarabu au hata Ulaya yenyewe, mkumbusheni Miraji wale wenzetu kule wanataka namba yani takwimu, apambane kuzipika namba uwanjani, hakuna kulala
.
Mnapokaa na Miraji huku vijiweni mkubusheni nini maana ya branding, page yake ya Instagram na Facebook ziwe kisasa, kuna vingi sana kwa mchezaji bora kutoka kwa wenzetu dunia ya kwanza
.
Ila cha mwisho mkumbusheni stori za mafundi waliobaki nchini tukaishia kusema jamaa alikuwa anajua sana mpira , msifiche kuhusu stori za West Ham na El Mereikh, ila muhimu mkumbusheni Dar Es Salaam uking'atwa na mbu ni malaria
jr_farhanjr-20191201-0001.jpeg
 
Asiwe tu mchezaji wa msimu mmoja! Nani amesahau moto wa Shiza Ramadhani Kichuya? Sasa hivi yupo wapi?
 
Salum Aboubakar Sure Boy
Said Khamis Juma Ndemla
Mohammed Hussein Tshabalala
Jonas Gerrard Mkude
Shomari Kapombe
Ibrahim Ajibu Migomba

Hawa jamaa maisha ya Dar es salaam wameamua kuridhika nayo kabisa, sijui ni mahali gani tunakwama ila kwa namna ambavyo wachezaji hawa wakiwa katika ubora wao hawakustahili kuwa nchini mpaka muda huu
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom