Miraji Mtaturu Mkuu wa Wilaya ya Ikungi aibuka Bingwa kwenye kura za maoni katika kuwania jimbo la Tundu Lissu kupitia CCM

Nyankuru Wankuru

JF-Expert Member
Apr 22, 2018
1,199
1,346
Matokeo ya kura za maoni CCM Jimbo la Singida Mashariki Ndg Miraji Mtaturu ameshinda kwa kura 396 sawa na ushindi wa 66% kati ya kura 634 huku wagombea wengine 12 wakigawana kura zilizosalia.
===

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Miraji Mtaturu ameshinda kura za maoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) baada ya kupata kura 396 kati ya 634 sawa na asilimia 63

Mtaturu ndiye atakayesimama katika kinyang'anyiro cha kuwania Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki baada ya Tundu Lissu(CHADEMA) kuvuliwa Ubunge mnamo Juni 28, 2019

Kampeni za uchaguzi katika Jimbo hilo zinatarajia kufanyika kuanzia tarehe 19 hadi tarehe 30 Julai 2019 na siku ya uchaguzi itakuwa ni tarehe 31 Julai, 2019
 
MATOKEO YA KURA ZA MAONI CCM JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI .

1. CHIKU GALAWA - 40

2. HAMISI ABEL MAULIDI - 12

3.HUME EMMANUEL JAPHET - 1

4.IHONDE JEREMIA MATHIAS - 4

5.KULWA SHILINDE KASULE - 1

6. LISSU MARTIN ZEPHANIA - 29

7. MWANAHAMISI MUNJORI - 7

8. MGONTO THOMAS KITIMA - 79

9. MEDA SYLVESTER KORNELI - 3

10. MKHOTYA MORICE PATRICK - 4

11. MSARU LAZARO MSENGI - 17

12.MARIAMU ALU NKUMBI - 7

13. MIRAJI JUMANNE MTATURU - 396
 
Chadema hawana pesa ya kushiriki uchaguzi .au upinzani hauna pesa ya uchaguzi pamoja na kupokea ruzuku.
 
Back
Top Bottom