Miradi ya ushirikiano wa kilimo ya China inainua wakulima wadogo barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,008
1,029
1649985684730.png


1649985700128.png


1649985714682.png


Na Tom Wanjala

Katika harakati za kusaidia kuboresha na kuimarisha usalama wa chakula barani Afrika, China inazidi kuwekeza katika vituo vya maonyesho ya teknolojia ya kilimo (ATDCs), vilivyoanzishwa na kampuni na taasisi za China. Vituo hivi pia vimeinua maisha ya wakulima wengi kutokana na uwepo wa nafasi pana iliyopo kwa wao kuuza mazao yao kwenye soko kubwa la China.

Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi nyingi duniani ambazo zinanufaika na China katika nyanja ya kilimo, kupitia vituo vya maonyesho ya teknolojia ya kilimo. Vituo hivyo vinapatikana katika nchi 23 barani Afrika na vimesaidia kuleta teknolojia na ujuzi wa kilimo Afrika kutoka China.

Dhana ya vituo vya maonyesho ya teknolojia ya kilimo ilianzishwa mwaka 2006 wakati wa mkutano wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, ili kuwasaidia wakulima wadogo katika bara zima. Wanasaidia kuboresha usalama wa chakula katika nchi nyingi, kupitia teknolojia ya kisasa ya Kichina ya kilimo na njia bora za kuimarisha kilimo chenyewe.



"Lengo la ATDCs hizi lilikuwa, ni pamoja na kujaribu na kuonyesha hadithi ya mafanikio ya kilimo ya China, mafunzo ya wafanyakazi katika maonyesho ya teknolojia, kisha kwa mapana lengo la ATDC kwa mujibu wa machapisho mengi ya 2011 ni kwamba, zimeanzishwa kufanya kazi ya kukuza uhusiano kati ya nchi hizo na nchi mwenyeji, kusaidia katika uzalishaji wa nafaka, kukuza teknolojia ya kilimo dhidi ya usalama wa chakula wa nchi zinazopokea msaada,’’ haya ni kwa mujibu wa George Mudimu, mtafiti katika Taasisi ya Kupambana na Umaskini, Ardhi na Mafunzo ya Kilimo ya Umoja wa Mataifa, ya Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini.

Kupitia ATDCs, China imeleta teknolojia mbalimbali za kilimo kwa Afrika. Kwa mfano, mataifa mengi ya Afrika yanatumia vifaa vya kisasa vya kilimo ambavyo vimerahisha shughuli za kilimo na pia kutoa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa wakulima hao.



Kuna ATDCs 23 katika bara zima la Afrika, ikiwa ni pamoja na Zambia, ambapo zaidi ya wakulima wadogo 200 wanapata mafunzo kila mwaka.

"ATDC ya Zambia, ambayo ilijengwa mwaka 2011, ina takriban ekari 120. Ina vifaa vyenye thamani ya dola za Marekani milioni 10. Kando na vifaa hivi, wakulima pia hupata mafunzo ya kuboresha kilima chao kupitia warsha za mara kwa mara na shughuli nyingine zinazohusiana na vituo hivi,” alisema Mudimu.

Nchini Afrika Kusini, China imefungua kituo cha mafunzo ya maonyesho ya ufugaji wa samaki, huku wakulima wadogo nchini Zimbabwe pia wakinufaika na fedha za ATDC.

"Nikiangalia mfano wa Zimbabwe, wengi wa wakulima wetu kwa sasa, ni wakulima wa kijamii, na wakulima vijana. Wameshiriki katika mpango wa mageuzi ya ardhi na kupata mashamba madogo au kupata shamba moja kubwa. Hii ni katika harakati ya kujaribu kusukuma mazao ya biashara, ambayo pia huleta pesa za haraka," alisema Blessing Simura, mtafiti wa kujitegemea.



Kupitia ushirikiano kati ya China na Afrika, miradi mingi zaidi ya misaada ya maendeleo ya kilimo inaweza kuanzishwa huku nchi nyingi zikihitaji ushirikiano huo kutokana na changamoto zinazoletwa na janga la uviko-19.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, limesema karibu watu milioni 98 wanakabiliwa na uhaba wa chakula barani Afrika, idadi ambayo ATDCs inalenga kupunguza.
 
China wanatechnology za kilimo simple Sana zikitumika Afrika zitainua kilimo
 
Back
Top Bottom