Miradi ya Mwenge: Udanganyifu huu wa kutumia ujinga wa baadhi ya watzania kufuja kodi zet hadi lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miradi ya Mwenge: Udanganyifu huu wa kutumia ujinga wa baadhi ya watzania kufuja kodi zet hadi lini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kyamkwikwi, Oct 28, 2012.

 1. K

  Kyamkwikwi JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 28, 2012
  Messages: 441
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndg Watanzania wenzangu, kwa masikitiko makubwa sana nawasihi tuungane sasa kupinga wizi huu wa pesa na kodi zetu kwa kutumia kisingizio cha mbio za mwenge wa huru.

  Nimekuwa nikijaribu kufuatilia kwa makini sana kuhusu mamia ya miradi ambayo huwa inafunguliwa kila kona ya nchi kipindi cha mbio za Mwenge ili kuona jinsi gani inasaidia kuwakwamua wananchi katika lindi hili la umasikini. Kila mwaka huwa tunashuhudia kwenye vyombo vya habari na wengine wetu huwa washiriki kabisa wa matukio mbalimbali ya mbio za mwenge ambapo Wtz wengi huaminishwa kwamba eti mwenge unahamasisha maendeleo na kuibua miradi mipya. Wameenda mbali zaidi na kuongeza uongo mwingine eti kwa kumbiza mwenge umoja na uhuru wa Wtz unadumishwa, eti mwenge huo unachoma maadui, mbona haujawachoma wao ambao ni maadui namba moja wanaoongoza kuiba raslimali za watanzani tena mchana kweupe bila aibu, wangapi tunawajua ni waamishaji wakubwa wa pesa zetu na wezi wakuu wa wanyama bila kutaja madini na maeneo mengine, kwa nini mwenge hauwachomi hawa. Au wakisema maadui wanamaanisha wale wanaopinga wizi na ufisadi wao, wanaowasema na kuwazomea ndio maadui wao, hii inakera sana.

  Hebu angalieni picha hizo hapo, hiki ni kibanda cha mabati kilichoitwa mradi wa mashine ya kusaga na kukoboa kama walivyodai wao. Kimefunguliwa tar. 01//10/2010 na kiongozi wa mbio za mwenge, sas hivi ni kichaka na makazi ya mbu na popo. Kibanda hiki kiko mkoa mpya wa Geita tena mjini na sio vijijini, ukitokea barenge njia ya kwenda kwa askofu kabla ya kufika kidaraja cha katundu mkono wa kulia utakiona hiki kibanda cha popo na mijusi kiko kwenye manyasi na bango kubwa mbele likisomeka "ASANTE KIKWETE POSHO MILL, MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA." Hii ni sehemu iliyo wazi kabisa, mkuu wa mkoa wa geita, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, na viongozi wote hupita maeneo haya, lazima wanapaona lakini si wameshakula chao likipanda hata likoza kwani la nini tena....

  Kuna bango kwenye jiwe la msingi likinadi ufunguzi wa kibanda hiki cha popo kama mradi uliofunguliwa wakati wa mbio za mwenge 01/10/2010, leo tunamaliza mwaka 2012 na kibanda kiko kichakani na wala sina hakika kama kweli kimeorodheshwa kwenye asset za mkoa au ndo hivyo wameshajilipa kwa kun'goa mashine na kila kitu na kuuza, nani ajuaye....?? Mategemeo yangu yalikuwa kwamba round ya pili ya mwenge ingekuwa kutembelea miradi iliyofunguliwa na kuangalia maendeleo yake lakini badala yake nimesikia na mwaka huu eti wamefungua miradi mipya. Watanzania hivi kweli karne hii ni ya kutenga bajeti ya mabilioni ya pesa eti kuzunguka na mwenge nchi nzima, kwa faida gani hasa..?? Nakubali uanzishwaji wa mwenge wakati huo ulikuwa na mantiki katika kujenga umoja na kuonyesha ishara ya ushindi dhidi ya wakoloni na kuutangaza uhuru wetu. Je, hakuna museums tukaweka mwenge wetu wa uhuru kama kumbukumbu ya kihistoria tukaacha huu ujinga. Kumbuka kuwa hawataki kuuweka mwenge makumbusho kwa sababu ndo njia moja wapo rahisi ya kukomba pesa zisizo ratibiwa, wanakula tu huku wakitangaza miradi hewa bila aibu.

  Nawaomba Watanzania kwa umoja wetu sote ebu tulikate hili jinamizi la mbio za mwenge lenye uvundo wa UFISADI uliokubuu. Walimu tunasema pesa ya kuwalipa stahili zao hazipo, madaktari tumewacheka eti wana tamaa japo sisi wananchi ndo tulitakiwa kuyadai yale waliokuwa wakiyalalamikia, shule zimekuwa magofu, dawa tunalishwa feki, hospitali pananuka usiseme, rushwa kila kona ya nchi, maisha kila siku double, ETI TUNAKIMBIZA MWENGE NA KUFUNGUA MIRADI HEWA.....!!!! Kila kukicha Mhesh. Yuko Kwa Obama anaomba asaidiwe net za mbu, SHAME ON HIM....!! Hakika hii laana Chama Cha Mabwepande (CCM) hata mfanyeje haiwabakizi lazima muanguke na kupasuka matumbo tu kabla ya kukanyagwa na kuzikwa, hopeless kabisa

  Please let us "SAY NO" ebu tuwe wazalendo na uchungu na pesa zetu - zitutumikie basi, shida na changamoto ziwepo zile ambazo ni za lazima na sio hizi za watu wanaiba halafu kesho wanatutangazia majukwaan sisi masikini, sisi masikini......!!!
   

  Attached Files:

 2. K

  Kanundu JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 891
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu!

  Subiria mwaka kesho, watakuja kuizindua tena hiyo Mashine ya Kusaga. Na wataipa bei na kusema ni mradi mpya. Si umeona hapo kwenye jiwe la uzindizi pameandikwa kwa rangi ya buluu! Next time wana pafuta na kuandika "MASHINE HII IMEZINDULIWA NA MWANAASHA K."

  Kuna Mashine moja ya kusaga inatumia maji, ina milikiwa na Kijiji kimoja Tarafa ya Amani Wilayani Muheza. Mashine hii, kila hilo li moto wakilipitisha, eti ni mradi mradi mpya umefunguliwa na mbio za hilo li moto. Kwa kukadiria ni kama mara zaidi ya 10, wanafungua na kuzindua hiyo Mashine.
   
 3. melxkb

  melxkb JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukitafakari kwa makini utangundua kuwa ni ujinga na ushamba wa wananchi kudanganywa danganywa kama vitoto vichanga na kuuza utu wao kwa ujira mdogo huku wakijiteketeza kwa kwa kuachilia kila kitu walicho nacho, njaa mbaya sana. We angalia wote wanaokesha kwenye hilo li moto kwani wana nini zaidi ya kupewa uniform za CCM na ubwabwa ili wakeshe wakicheza ngoma.
   
Loading...