Miradi ya maendeleo China -Uganda inagusa wananchi moja kwa moja

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,587
215,179
Wakati serikali ya CCM inatuamisha kuwa China ni rafiki zetu na kuwa tuna historia ya miaka mingi na nchi hiyo. Miradi ya maendeleo ya serikali ya watu wa China nchini Uganda inagusa maisha ya watu moja kwa moja. Mfano wa miradi hiyo ni Naguru Hospital yenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa wa nje na vitanda 100 vya wagonjwa wa kulazwa.

Mkurugenzi wa hospitali alisema wana mlango wa Kipanya huduma kufikia vitanda 500 vya wagonjwa wa kulazwa. Huduma za kila siku katika hospitali hiyo huendeshwa kwa ushirikiano wa wataalamu wa China na Uganda.

Viongozi wetu tunaomba miradi kama hii hapa kwetu kama marafiki zetu wanaweza kuwekeza na sisi tunufaike na matunda ya urafiki huu.

1593140686478.png

1593140732579.png
1593140747612.png
 
Hao wachina walipokuja Dar na meli yao ya matibabu mlilalamika.

Kwetu miradi ya maendeleo inawagusa malaika peke yao.

Kama siyo miongoni mwa hao malaika hutoweza kuona chochote, iwe ni ndege ama viwanda 8000+ vilivyojengwa ndani ya miaka mitano.
 
Kuna aina tatu za maendeleo.
. Maendeleo ya vitu
.Maendeleo ya watu
. Maendeleo ya watu na vitu.

North Korea, Ethiopia ,Rwanda na nchi za kidikteta na kikomunisti wao Wana maendeleo ya vitu lakini watu dhoofu hali.Hapa vipaumbele ni vya mtawala kutafuta sifa na Wala si tija kwa wananchi.Watawala wakiishi kifalme huku watawaliwa wakifanywa masikini kimakusudi kwa kuwasomesha namba ili waweze kutawaliwa, matajiri na wasomi wakishughulikiwa haswaa kwa kulazimishwa ili uwe salama ni lzm umuabudu mtawala kinyume chake ni kifo,risasi, kubambikiwa kesi.
Cuba Ina maendeleo ya watu.
USA,Canada, Scandinavian,Dubai, Ulaya zina maendeleo ya watu na vitu.Yaani maendeleo ya vitu yanaenda sambamba na maendeleo ya watu.Hakuna kimoja kinamtangulia mwenzake.Maendeleo yeyeto yasiyoreflect maisha ya watu achilia propaganda hayo siyo maendeleo yamfaao mwanadamu.
 
Wewe ni kilaza kweli kwanini kama barabara na umeme wa REA na madaraja hauwausi wananchi wa moja kwa moja si wabunge wetu wa upinzani si wangeyakataa lakini badala yake wanayaomba hayo mamridi kila siku na sijaoina anayepinga ujenzi wa fly over nk. Kuhusu hospital ndo zinakamilika jumla ya hosptial zaidi ya 67..Inamaana tuko mbali zaidi ya uganda > Ungeleta hoja ya Kilimo ningekuelewa
 
Marekani maendeleo yanagusa watu wachache sana.
Kumbuka hata bima ya afya kwa wote imeweza kupitishwa wakati wa Obama ikaitwa ObamaCare; ni mfumo ambao uliwezesha watu wa chini kuchangia kidogo na matajiri kuchangia sana ili walio wengi waweze kumudu matibabu kwa mfumo matibabu kwa kutumia bima.

Scandinavian countries ni mfano w nchi ambapo maendeleo yanakuwa jumuishi kwa kugusa watu na vitu
 
Katika kipindi cha miaka 5 wewe umeona bombadia tu barabara za kiwango huzioni , mambo ya umeme , sgr na reli ya kawaida au ndio unatoka kupata , inueni miyo.
Wengine niwapumbavu wakupuuzwa
hao hao Uganda wanajengewa kipande cha Barabara Chenye Ghalama kubwa Duniani
Kwa utajiri gani walio nao
 
Miradi ya stendi za wapita zao wachache mikubwa kila mkoa ingekuwa ni hospitali za rufaa kila mkoa ingegusa wengi. Hospitali za Rufaa kubwa kila mkoa au mji au wilaya ingekuwa ni aina nzuri ya Maendeleo ya Watu badala Maendeleo ya Vitu kama stendi hii hapa chini:

Source : Global TV online
 
Maendeleo ya Vitu ktk sera ya CCM Mpya inapewa kipau mbele na msisitizo na Katibu wa CCM Mpya Kanali mstaafu Ngemela

Source: Global TV online

More info:
Habari zaidi za mradi huu ambao pia mikoa mingine chini ya serikali ya CCM Mpya wanaitekeleza kote nchini Miradi ya Maendeleo ya Vitu :

UJENZI WA KITUO CHA MABASI CHA NGANGAMFUMUNI KUANZA RASMI
thumb_215_800x420_0_0_auto.jpg
Posted On: January 16th, 2019
MAYA.jpg
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imesaini mkataba na kampuni ya ukandarasi ya kimataifa ya CRJE (EAST AFRICA LTD), kwa ajili ujenzi wa kituo cha Kimataifa cha mabasi cha Ngangamfumuni.

Ujenzi wa kituo hiki cha Kimataifa cha mabasi cha Ngangamfumuni(Ngangamfuni International Bus Stand Terminal ) utaanza rasmi Januari 17 mwaka huu 2019 mbapo hadi kukamilika mradi huu wa ujenzi utagharimu zaidi ya tsh bilioni 27.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Mkurugenzi wa Manispaa ya
Moshi, Michael Mwandezi alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho utatekelezwa kwa awamu tatu tofauti huku ukichukua muda wa miaka miwili hadi kukamilika.

Hata hivyo Mwandezi alisema kuwa mradi huo mpya wa kituo cha mabasi utaibadilisha Manispaa hiyo katika Nyanja ya kichumi pamoja na utekelekezaji wa malengo ya Serikali kuhakikisha miradi yake inakamilika kwa wakati.

Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Moshi Rayamod Mboya alisema kuwa,ujenzi wa kituo cha Ngangamfumuni ulisubiriwa kwa muda mrefu na wananchi wa Manispaa ya Moshi na wadau wa usafirishaji hivyo kukamilika kwake kutaongeza hadhi pamoja na kutoa fursa ya ajira kwa wakazi wa Manispaa ya Moshi.

Alisema ujenzi wa kituo hicho cha mabasi utatekelezwa kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza itakuwa ni kukamilisha eneo la maegesho ili kuweza kuanza kazi ambapo awamu nyingine ni pamoja na kuanza ujenzi wa jengo la gorofa tano ambalo litakuwa na Hoteli,maduka, migahawa pamoja na ofisi mbalimbali.

10 Juni 2020 : Chemchemi chini ya majengo ya stendi mpya Moshi yapasua vichwa vya wataalam
Source : Azam TV

Kukamilika kwa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi cha ngangamfumuni kutaifanya Manispaa ya kuwa mojawapo ya Manispaa zitakazokuwa na kituo ya mabasi chenye ubora zaidi nchini na ukanda wa Afrika Mashariki.

Source : UJENZI WA KITUO CHA MABASI CHA NGANGAMFUMUNI KUANZA RASMI
 
Kuna vitu kama tungeamua kuwa creative and strategic tungepiga hatua kwa haraka kwa kuwa na maendeleo ya vitu na watu.
Mathalani,
Kwa mujibu wa kumbukumbu za wizara ya afya, zaidi ya 97% ya madawa na vifaa tiba tuna-import kutoka China/India.
Kuanzisha kiwanda ili kupata dhamana ya kibenki, ikiwamo TIB sio rahisi kuwa na 40% ya project cost.

Ila kama wizara ya fedha na wizara ya afya, wizara ya ardhi na wizara ya viwanda zingetoa dhamana kwa mtu mwenye innovative investment project say ya kutengeneza pamba za hospitali, au bandeji, au gauze au mashuka; apeleke proposal. Ikipitiwa anapewa ardhi, mkopo kwa kununua mashineries, then training ya staff, pamba inanunuliwa ndani.
Soko wizara ya afya kupitia MSD.
Hii ikifanyika pamba yetu ina-meet local demands, kazi zinapatikana, Tanesco inauza umeme, NSSF anapata wanachama, TRA tax base inaongezeka, kwa PAYE, Corporate tax na 18% VAT kupitia manunuzi ya bidhaa na huduma kwa viwanda.

Bajeti imepita, wabunge wetu walikuwa busy kuwaza mafao na itakuwaje kwenye mchakato.
Hili ni moja tu ya eneo ambapo TIC&EPZA walitakiwa wajenge mifumo ili start-up zilenge kukuza uchumi kwa ku-cut down imports na ikiwezekana kuongeza exports.
Inturn tunajikuta kila mwaka kujisifia kuagiza madawa worth bil 300.

Mimi ungenipa dhamana ya kiserikali kukopa walau ningehakikisha MSD hanunui tena mashuka made in China.
Uniform za watoto wa shule vitambaa vinakuwa made in Tanzania.

Kama ni ubia, ufanyike kwa wao kutukopesha machineries za ku-process kwa guarantee ya serikali; watupe training vijana wetu wa veta walau washone chupi na sidiria kwa ajili ya soko la africa.

Ni aibu tunawekeza 17bil kwenye stand ya mabasi, wakati tungewekeza less than 6bil, tukakoma kuagiza mashuka na chupi na leso kutoka china.

Its high time to be very very serious

Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote
 
Miradi ya stendi za wapita zao wachache mikubwa kila mkoa ingekuwa ni hospitali za rufaa kila mkoa ingegusa wengi. Hospitali za Rufaa kubwa kila mkoa au mji au wilaya ingekuwa ni aina nzuri ya Maendeleo ya Watu badala Maendeleo ya Vitu kama stendi hii hapa chini:

Source : Global TV online

Changamoto ya baadhi ya watu wanaotoa tafsiri hasa ya maendeleo kwa kujenga stand za mabasi ni kwa kuwa wana uhakika wa "kuvuta" wakati wa ujenzi au wanaweza kuvuta pia kwenye collection za mapato kwa stand kama ya Msamvu Morogoro au Dodoma.

Ila kwa muono mwingine, kama ingejengwa hospital kama mtoa hoja ulivyosema, na sehemu ya hela ikakopeshwa Mtanzania sio fedha, ila mitambo ya kuchakata hata dawa za syrup za watoto au watu wazima. Iwe panadol au dawa za kikohozi, na mwingine akapewa mtambo kuchakata chupa za kufungashia dawa, na mwingine akapewa mkopo wa mitambo ya boxes za packaging;

Outcome na impact ya huu mradi wa kijamii na mrejesho wake kibiashara kwa kurejesha fedha kwenye kapu kuu ili na wengine wakope ungekuwa mkubwa zaidi.

Bahati mbaya, Wizari wa viwanda sijui huwa wanawaza nini kuanzia Mwijage, Kakunda na sasa Bashungwa.
Kuna wakati hata simu zao ukiwapigia kuomba appointment walau kuonana na kuzungumza hawapokei simu.
Loh, it breaks our hearts tunapokuwa na Rais mwenye kuonesha vision, then wasaidizi wanashindwa kutafuta collaborators kuitafsiri vision na kuchagiza implementation yake kwa haraka zaidi
 
Miradi ya stendi za wapita zao wachache mikubwa kila mkoa ingekuwa ni hospitali za rufaa kila mkoa ingegusa wengi. Hospitali za Rufaa kubwa kila mkoa au mji au wilaya ingekuwa ni aina nzuri ya Maendeleo ya Watu badala Maendeleo ya Vitu kama stendi hii hapa chini:

Source : Global TV online

Hizo hospital za wilaya sio maendeleo yanayo gusa watu
 
Hizo ni shanga au? Hizo alizovaa huyo mgonjwa.

Akili yangu ishahama kabisa
 
Wakati serikali ya CCM inatuamisha kuwa China ni rafiki zetu na kuwa tuna historia ya miaka mingi na nchi hiyo. Miradi ya maendeleo ya serikali ya watu wa China nchini Uganda inagusa maisha ya watu moja kwa moja. Mfano wa miradi hiyo ni Naguru Hospital yenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa wa nje na vitanda 100 vya wagonjwa wa kulazwa.

Mkurugenzi wa hospitali alisema wana mlango wa Kipanya huduma kufikia vitanda 500 vya wagonjwa wa kulazwa. Huduma za kila siku katika hospitali hiyo huendeshwa kwa ushirikiano wa wataalamu wa China na Uganda.

Viongozi wetu tunaomba miradi kama hii hapa kwetu kama marafiki zetu wanaweza kuwekeza na sisi tunufaike na matunda ya urafiki huu.

View attachment 1489074
huku tunajenga wenyewe bila hata wachina 🇨🇳🇨🇳🇨🇳🇨🇳🇨🇳
 
Kuna aina tatu za maendeleo.
. Maendeleo ya vitu
.Maendeleo ya watu
. Maendeleo ya watu na vitu.

North Korea, Ethiopia ,Rwanda na nchi za kidikteta na kikomunisti wao Wana maendeleo ya vitu lakini watu dhoofu hali.Hapa vipaumbele ni vya mtawala kutafuta sifa na Wala si tija kwa wananchi.Watawala wakiishi kifalme huku watawaliwa wakifanywa masikini kimakusudi kwa kuwasomesha namba ili waweze kutawaliwa, matajiri na wasomi wakishughulikiwa haswaa kwa kulazimishwa ili uwe salama ni lzm umuabudu mtawala kinyume chake ni kifo,risasi, kubambikiwa kesi.
Cuba Ina maendeleo ya watu.
USA,Canada, Scandinavian,Dubai, Ulaya zina maendeleo ya watu na vitu.Yaani maendeleo ya vitu yanaenda sambamba na maendeleo ya watu.Hakuna kimoja kinamtangulia mwenzake.Maendeleo yeyeto yasiyoreflect maisha ya watu achilia propaganda hayo siyo maendeleo yamfaao mwanadamu.
ulishawahi kuishi Havana Cuba au unadanganya watu hapa
 
Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom