Miradi ya kichina barani Afrika na Asia, Je Tanzania tuna la kujifunza?

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
43,394
81,237
Kenya imezindua SGR ambayo imegharimu 3.5 bn US$ kama mkopo toka Uchina. Wapinzani wa mradi huo nchini Kenya na wana uchumi duniani/world bank wanadai hakuna biashara Kenya itafanya na reli hiyo kurudisha hela hiyo! Another concern ni kuwa miradi mingi ya wachina africa ni substandard na hivyo ndani ya miaka 7-10 itakuwa imechakaa na kudai hela tena ya kuitengeneza
Mfano: Sri Lanka ilijenga bandari kwa mkopo wa 1 bn US$ toka uchina. Sasa ni mwaka wa saba (7) bandari iko idle haina meli za kuhudumia. Jana kulikuwa na meli moja tu! na hivyo Sri Lanka imeshindwa kulipa mkopo na kulazimika kutoa dau ya 85% kwa uchina katiak bandari hiyo.


Je TZ tuna la kujifunza?

Source: BBC Swahili News 9.00 PM today.
 
Wachina wako kibiashara, ni jukumu la wanaotaka huduma yao kujitafakari na kuona faida na hasara za Wachina kabla ya kuingia nao mkataba.
 
1. Je unataka kutugombanisha na rafiki zetu?
2. Tunapenda upole wao: hawahangaiki na mazingira, utawala bora, uwazi, demokrasia, ...
 
Ukoloni wa kisasa huo ....na huku kwa waafrica ndio wanatujulia vizuri kweli! Tumebumbazwa na kufikiri wachina wanatupenda na ni marafiki wetu wa kweli!
Countries Don’t Have Friends; Just Interests!
 
hakuna la kujifunza, kama tumewalika Tanga ina maana bado tunawahitaji.
 
Kiwira Coal Mines walijenga Wachina, Reli la Tazara walijenga Wachina, Viwanda vingi vilivyojengwa enzi za Mwalimu vingi vilijengwa na Wachina, so walioviua ni akina nani?
 
Back
Top Bottom