Miradi Mikubwa ya Uzalishaji Umeme wakati wa Mzee Ruksa ni ipi? Toka hapo...

Hivi kwanini unapenda kufabricate maneno ili ya fit unachoamini?Mimi naweza kununua hisa,matter of fact ninazo hisa na zinaniletea faida kiasi fulani.Ninaweza kununua hisa kadhaa kama NMB itawekwa DSE...I can easily do that....na ninayo nafasi hiyo kama watu wengine walivyo na nafasi hiyo
Unachokwepa kukubali ni kuwa asilimia nyingi ya watanzania hawana uwezo,wala information kuhusu ununuzi wa hisa au uwekezaji kwenye haya mashirika.I can say 90% hawana uwezo wa kufanya hivyo.Sasa ndugu yangu kwanini una act kama hujui hili?Au unataka tu kupoteza muda kwa kupindisha lugha?....ukisema watanzania wana hali mbaya kiuchumi,it doesn't neccessarily mean kila mtanzania ana hali mbaya kiuchumi.
You are better than that,acha hizo lugha tata mkuu.

hapana miye napenda mtu ajaribu kusema anachomaanisha; ukisema "asilimia nyingi" nayo ni neno lenye maana. Kuwekeza si lazima iwe hisa na kwenye posti zako za kuwakandia Watanzania ulizungumzia "uwezo" bila kufafanua. Unapowakandia Watanzania kwa ujumla wao - kama ulivyofanya - na wewe unajijumuisha unless unatengeneza exception. Ni lazima uwe tayari kukwepa internal contradictions. Jambo hilo ni muhimu ili tujue tunazungumzia kitu kile kile, kwa mfano sasa najua ulikuwa unamaanisha kununua hisa, lakini mwanzoni hukusema miye ningejuaje wakati umesema Watanzania hawana "uwezo" wa uwekezaji?
 
I won't waste time on this,ila kama unataka tuzungumzie kudorora kwa uwekezaji wa umeme,then we can have a discussion/debate.....the rest is just circus.
 
I won't waste time on this,ila kama unataka tuzungumzie kudorora kwa uwekezaji wa umeme,then we can have a discussion/debate.....the rest is just circus.

yeah.. lakini usiwe unatoa general statements without qualifying them. Turudi kwenye mjadala.
 
Mkuu,
Haya yote ni mambo ya privatization as championed by Mtei,ambaye aliasisi CDM.Serikali haikuinvest kwenye umeme wakidhani TANESCO itabinafsishwa,na nimeshasema mara nyingi kuwa privatisation/free market haitomfaidisha mwananchi wa kawaida.
Baada ya mwalimu,kila mtu kivyake....sasa mnalalamika nini? si mlisema serikali haiwezi kuendesha kitu chochote?Waambieni hao private investors wachimbe mabwawa muone real charges za umeme.
Privatisation ni siasa au ideology ya CDM,ila imewatokea puani sasa mnajifanya wajamaa na kutaka serikali iwekeze kwenye umeme...what the hell happened?
Kobello, ni lini CHADEMA walipata kuiongoza nchi hii na kutekeleza sera unayosema eti waliichampion ya privatisation na ambayo sasa "inawatokea puani"? Mtei alikuwa serikalini wakati Katibu Mkuu wa CCM wa wakati ule hayati Horace Kolimba alipokwenda Malaysia kutuletea hili dude IPTL linalotutafuna mpaka leo? Ipo saini ya Mtei katika Mkataba wa kijambazi wa IPTL? Ni Mtei aliyesaini mikataba ya Aggreco? Songas, Richmond, Dowans n.k.? Kisha utuwekee jamvini role ya Kikwete katika kuiingiza IPTL na Richmond, halafu utuambie CHADEMA na Mtei wanaingiaje katika sakata hili.
Tunawaomba sana msitutoneshe kidonda cha ujambazi uliokithiri uliofanywa na CCM miaka yote hii wa kupora mali na amali za taifa na kutuingiza katika mikataba yenye sumu inayofisha bila ya kupigiwa kelele. Dunia sasa imegeuka na ufahamu wa watu juu ya maovu mliyotufanyia kwa miango kadhaa sasa umeongezeka pia. Sasa tunaelewa fika ni nani wa kwanza kutuingiza mkenge wa IPTL - Mwinyi na Kikwete aliyekuwa waziri wake wa Nishati na Madini mwaka ule 1994.
Ajabu ni kwamba karibu woote waliohusika na kashfa hizi wapo bado hai, wanaendelea kupumua na kutukoga wengine wakiwa na madaraka makubwa tu ndani ya serikali baadhi yao wakiendelea kulipwa pensheni na serikali huku wakiendelea kufaidi matunda ya mikataba mibovu kwa kugata gawiwo na walioshirikiana nao. Mimi naamini kwamba ipo siku sheria itachukua mkondo wake iwe kesho, mwezi, mwaka au hata baada ya miaka mingi ijayo.
Aibu kwa CCM na viongozi wao walafi na wezi wakubwa! Kifo kwa CCM. Mungu ibariki Tanzania, waangamize mafisadi wote.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Source: Raia Mwema by J.Mihangwa

KATIKA sehemu ya kwanza ya makala hii, tuliona jinsi mkataba wa miaka 20 wa kuuziana umeme [PPA] ulivyofikiwa kati ya IPTL na TANESCO, mkataba ambao umeitupa nchi yetu gizani kwa mgawo wa umeme wakati serikali itaendelea kuilipa IPTL zaidi ya Sh. bilioni 6 kwa mwezi kwa umeme usiokuwepo kwa kipindi chote hicho.
6bn x 12x20=? halafu kuna mtu hajui kwanini bei ya umeme ni ghali.
Tamko la serikali kupitia kwa Waziri wa Madini na Nishati, William Ngereja, hivi karibuni kwamba tatizo la umeme nchini litamalizika mwaka 2015, linakwenda sambamba na muda wa mkataba huo wa IPTL wa miaka 20 [kuanzia 1995] utakapomalizika mwaka huo
waziri wa serikali ya CCM, hapa hakuna Chadema au CUF isipokuwa kwa mtu anyejifanya hayawani.
Tuliona chimbuko la mkataba huo wa kifisadi, kuanzia na ziara ya Waziri wa Mipango wa wakati huo, hayati Horace Kolimba nchini Malaysia, Julai 1994, alikozungumza na wawekezaji katika sekta ya umeme wa nchi hiyo na kuwaomba waje nchini kuangalia uwezekano wa kuwekeza ili kupunguza tatizo la umeme.
Katibu mkuu wa CCM, sio Mtei kama wanavyoamini wenye chuki.
Agosti 19, mwaka huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mechmar, inayomiliki asilimia 70 ya hisa za IPTL, Bw. Datuk Baharuden Majid, aliongoza ujumbe mzito kutoka Malaysia kuja kufanya mazungumzo na serikali yetu juu ya uwekezaji huo. Walioshiriki katika mazungumzo hayo kwa niaba ya serikali yetu ni pamoja na Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa wakati huo [na sasa Rais wa Tanzania], Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Simon Mhaville, Kamishna wa Nishati Msaidizi, Ester Masunzu, na Msaidizi wa Rais Ali Hassan Mwinyi wa Mambo ya Uchumi, Dakta Juma Ngasongwa.Viongozi na watendaji hao wakuu wa serikali, kwa nia njema na thabiti kabisa, waliukaribisha uwekezaji huo bila kujua kwamba hatimaye ungeingiliwa na "dumuzi" mharibifu; kwa maana ya ufisadi kwa njia na mtindo ule ule uliotumika kwa kashfa ya rada.Mwezi mmoja baadaye, Septemba 1994, Mkataba wa Maelewano [MOU] ulifikiwa baada ya kuthibitishwa na Mwanasheria Mkuu wa nchi, kuwa ulikuwa mzuri na wa manufaa kwa nchi; licha ya
tahadhari kutoka kwa washauriwa wa TANESCO – Kampuni za Acres [Canada] na Hunton and Williams [UK], kwamba uwekezaji huo ulikuwa hati ya kifo kwa sekta ya umeme na kwa uchumi wa Taifa.Kumbukumbu zinaonyesha kuwa, ufisadi mwingi na mkubwa wa kutisha kwa uchumi wa nchi,
mara nyingi umefanyika karibu na chaguzi kuu hasa katika enzi hizi za demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Mfano hai ni pamoja na kashfa za Meremeta, EPA, Richmond/Dowans na nyinginezo, ambapo mabilioni ya fedha jasho la wananchi, yameporwa bila huruma na mikataba mibovu kuingiwa kwa kisingizio cha "usalama", "ustawi" au "manufaa" ya Taifa, wakati ukweli ni kinyume chake. Mkataba wa IPTL unaweza kuwa mmoja ya mbinu hizo.
Ni katika kipindi hicho, kigogo mmoja wa Chama [Dakta Abdallah Kigoda] aliyekuwa na cheo cha chini tu kwenye Tume ya Mipango ya Taifa, aliteuliwa kuwa Mtunza Hazina wa CCM, na hivyo kuingia katika "gurudumu" la Chama tawala.Baada tu ya kutiwa sahihi kwa Mkataba wa Ujenzi [EPC] mwaka 1997, alipanda cheo ghafla kuwa Waziri wa Wizara nyeti yenye dhamana ya sekta ya umeme nchini. Ni mwafaka gani huo wenye matukio tata na tete yenye kushabihiana?Ufisadi katika mradi huu ulianza kujidhihirisha mwezi Februari, 1995 katika ununuzi wa mitambo ya mradi. Awali, Kampuni ya Wartsila ilikuwa imeomba kuuza jenerata za kufua umeme 11 aina ya Slow Speed Diesel [SSD] zenye uwezo wa kuzalisha megawati 116 za umeme kwa bei ya dola milioni 53 tu pamoja na vifaa vyote.
Lakini Februari 15, 1995 bei ya jenereta hizo iliongezwa kinyemela kufikia dola milioni 85.7, na dola milioni 114.2, Januari 1996, na hatimaye dola milioni 163.5 kwa gharama za ujenzi [EPC] na dola milioni 126.39 kwa jenereta 10 tu.
Nyumba 37 zilizopangwa kujengwa pale Tegeta zilipunguzwa kutoka 37 hadi 6, lakini kwa gharama ile ile ya nyumba 37 kwa dola milioni 7.6!
Kuna ushahidi kuonyesha kwamba, kampuni hiyo hiyo Wartsila, iliziuzia nchi nyingine za Kiafrika, ikiwamo Kenya, Jenereta kama hizo za Mradi wa IPTL, kwa chini ya dola milioni 60. Na kama kwamba hiyo haikutosha, IPTL ilibadili mitambo SSD na kusimika mitambo hafifu na ya bei ya chini zaidi lakini ya aghali kuendesha, aina ya Medium Speed Diesel [MSD] kwa bei ile ile ya SSD, ili kujipatia kivuno kwa kupora kutokana na tofauti ya bei kinyume na mkataba, na bila TANESCO kujua
Kwa hiyo, ukichukulia kwamba nchi yetu iliuziwa mtambo mbovu kwa bei mbaya; ukichukulia pia kwamba mradi huo uliongezwa gharama kinyemela kwa asilimia 130 badala ya gharama halisia; na ukichukulia zaidi kwamba mkataba huo wa kitapeli umeifanya Serikali yetu kulipa zaidi ya Sh. bilioni 6 kwa mwezi kwa umeme usiokuwepo na nchi kuingia gizani; hivyo kwa njia hii, ufisadi wa IPTL umetwisha mzigo uchumi wa nchi na kuturudisha nyuma hatua tatu katika maendeleo
Historia yajirudia kwenye radaHistoria kama hii imejirudia kwenye kashfa ya rada ambapo Serikali imedai kila mara kutokuwapo ushahidi juu ya ufisadi huo hadi tumeumbuliwa na jamii ya kimataifa kama tulivyoona mwanzo.Hatimaye IPTL ilianza kuzalisha umeme Januari 15, 2002 kwa asilimia 50, chini ya uwezo uliotajwa katika mkataba; huku TANESCO ikitakiwa kulipa zaidi ya dola milioni 4.6m kwa mwezi au dola milioni 55 kwa mwaka, kwa huduma na kwa kutumia umeme wa IPTL. Chini ya mkataba huu, TANESCO [Serikali] inalipa dola milioni 3.6 [Shs. bilioni 5.4] kama ada ya huduma za mtambo [capacity charge] pekee kila mwezi. Juu ya malipo hayo, TANESCO inalipa senti 13 za Kimarekani kwa kila yuniti ya umeme kwa kuendesha mtambo kwa nusu ya uwezo wake [yuniti moja ni sawa na kilowati moja] kwa mwezi, na kufanya gharama zote kwa TANESCO kufikia zaidi ya Sh. bilioni kwa mwezi au Shs. bilioni 90 kwa mwaka.
Wananchi wabebeshwa zigo
Tunafahamu kwamba, TANESCO hawana fedha za kulipa malipo haya. Njia pekee kwa TANESCO ni kuongeza bei ya umeme kwa Watanzania masikini. Kwa mujibu wa gharama hizi, umeme wa IPTL unapashwa kuuzwa senti za Kimarekani 13 au Sh. 120 kwa yuniti ikilinganishwa na umeme rahisi wa Kidatu [hydro] wa senti 3 au Shs. 28 kwa yuniti.
Ni kwa sababu hii kwamba, serikali sasa inatoa ruzuku zaidi ya dola milioni 1.6. [Sh. 2.4] kwa TANESCO kila mwezi. Pamoja na hatua hiyo, bado mzigo kwa TANESCO ni mkubwa, na kwa vyovyote vile lazima bei ya umeme kwa mlaji iongezeke kati ya asilimia 15 na 35.
Ongezeko hili sio tu linamuumiza mtumiaji wa kawaida; bali pia linapunguza hamasa ya wawekezaji kutoka nje. Kwa nchi yetu, IPTL ni nyoka mwenye sumu kali aliye chini ya uvungu.
Niungane na Brian Cooksey katika mada yake The Power and the Vainglory [uk. 3] kwa kutaja tu kwamba, kama isingekuwa hujuma za IPTL/VIPEM, tayari Tanzania ingekuwa inavuna gesi yake ya asili na kuokoa mamilioni ya fedha za kigeni kutokana na kuagiza mafuta ya mitambo.
Vivyo hivyo, hasara kwa uchumi wa nchi kutokana na upungufu wa umeme tangu mwaka 1997 ingeepukika kama mradi wa Songas usingehujumiwa na "sakata" hili na mizengwe hii ya IPTL.
Baya zaidi ni kwamba, Watanzania wamebebeshwa gharama kubwa za umeme pamoja na deni kwa taifa ambalo fedha zake zimenufaisha wajanja wachache. Baadhi ya wajanja hao wangali pamoja nasi, wakiendelea kutumbua salama walichopora. Serikali inapofumbia macho ufisadi huu, wananchi waieleweje?
Hakuna mahali popote pametajwa CUF,TLP, CHADEMA au Mzee Mtei, Dovutwa, Mziray au Lipumba.Haihitaji elimu yoyote kutambua bali kujua kusoma na kutafakari.
Tofauti, viongozi wakubwa wa CCM wametajwa akiwemo hayati Horace Kolimba, Abdallah Kigoda, Jakaya Mrisho Kikwete, ambao si tu wamekuwa serikalini bali wengine wapo hai na serikalini.
 
Hiyo deal yote ya IPTL inajulikana ipo all over the web!....ukiwa mtu unayeabudu au sujudu mwanadamu mwingine,ujue kuna some psychological disorder ambayo si rahisi kuitambua.
Tunazungumzia uwekezaji wa serikali kwenye umeme post-mwalimu,and you my brother,looks like you've been offended when I connected the founder of your party,your philosophy as a whole when it comes to our economy,
There are so many articles or essays or reports on this issue of privatisation and Mtei's connection to the whole outcome.But it seems that you just found that out.Some scholars think he has nothing to do with this mess,some think he has a lil bit,some think he has a lot to do.But that depends on a person.
Now,even before Nyerer retired,the government already had started to increase private/parallel sector involvement in transportation,people who had "own accounts"i.e people working overseas,or people with relatives or just with forex can import pick-ups,daladalas...and other things but IMF was still pressuring the govt to liberalise,Donor countries pressured the only "project-funding" donors,the NORDIC countries and accused them of being too soft,they had to succumb.
Now after 86,the country began to follow a free market economy,TANESCO haiuziki,umeme hauwi generated,mabwawa hayatunziki,wawekezaji kwenye kilimo hawatufaidishi na wanamaliza vyanzo vyetu vya maji n.k
Uwekezaji kutumia mafuta mazito ni gharama na hatuko tayari kulipa zaidi.....na hao private investors are all fd up.Wakati IMF wanaikaba Tanzania yeye alikuwa upande wa IMF,admittedly usibishe.
In other words that was kind of "an accessory to murder/rape/roberry......or "Enabler" and those kind of people are more or less responsible for the crime.
 
I am a good citizen of this country. No one is offended I guess with your connection, but people are offended by malicious elements injected in the topic to an extent of adulterating it.
This forum could be used for constructive ideas not misleading the public by trivial and irrelevant connections.
If one believes that Mtei has connection with Richmond, Dowans, IPTL then readers must be offended big time!!.
If one believes that Chadema has once ruled this country, that's an offense per se!
 
Kuna kitu nimejaribu kukufanyia utafiti mdogo kwa ajili ya hoja yangu ambayo itaonesha kuwa tatizo la umeme Tanzania linahusiana na CCM hasa baada ya Rais Mwinyi, likaendelezwa na CCM chini ya Mkapa na sasa CCM chini ya Kikwete. Huwezi kuzungumzia tatizo la nishati hii nchini bila kugusa CCM. Hata hivyo, naomba mwenye kujua Rais Mwinyi alianzisha miradi gani mikubwa ya kuzalisha umeme akianticipate ukuaji wa uchumi?
Hebu angalia kwenye bold,suala la mradi wa mwinyi amejibiwa.
Mimi naona wewe ndio unaiharibu topic just because nimemuunganisha kiongozi wako mtukufu na kudorora kwa uwekezaji kwenye nishati.Hivi mazingira gani yatakuwaso liberal,so condusive kwa watu kuwekeza?...hii serikali ipo tayari kuua watu wake ili kumleta mwekezaji.....kwanini hawawekezi kwenye umeme?
Even the foreign aid shifted the mode from project funding to imports facilitation,as a treasurer he facilitated and enabled the washington consesus to privatise our economy,we were even forced to have multiparties....now we are blaming CCM for what? Accepting IMF conditions? or for not accepting IMF conditions?
Stick to the topic...we are talking about connections and you are talking about........i don't even know!
 
@Kobello, Tanganyika and later Tanzania imekuwa chini wa utawala wa TANU/CCM. Na tunaweza kusema Tanzania imekuwa chini ya CCM since birth maana TANU ndio CCM kwa sasa. Hakuna uchaguzi mkuu hata mmoja uliofanyika katika nchi hii ya Tanzania, wananchi (a) wakamchagua Mzee Mtei, IMF, the World Bank kuongoza nchi na (b) kuchagua serak za Mzee Mtei, IMF & the world Bank. Chaguzi zote zilifanyika zimechagua viongozi toka CCM baada ya campaign za kuuza sera/ilani za chama/vyama vyao. Na so far tumekuwa na Rais Mwal Nyerere, Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete, wote hawa wakiwa wanatoka TANU/CCM.

Hakuna mahali popote tumemskia viongozi wetu wakuu wakinadi ilani au sera na kusema zimetoka kwa Mzee Mtei, IMF, the Wold Bank. hakuna! Na hata wakati ccm wananza ku-implement sera ya privatisation hawakutuambia kuwa wanafanya hivyo kwa niaba ya mtu au chombo chochote. Ni wewe kupitia JF ndio umekuwa unadai ccm wanatekeleza sera za za Mzee Mtei, IMF & the Wold Bank! Lakini kumbuka tumechagua viongozi wa ccm na sera zao (hivyo ndivyo mmekuwa mnatumbia hasa wakati tunaandamana kudai haki zetu).

Now, up until mid 1990s sekta ya umeme ilikuwa ya uhakika, pamoja na kwamba haukuwa umefikia kila kaya Tanzania, lakini wale waliokuwa wameunganishiwa umeme walikuwa wanaupata. TANESCO walikuwa hawazilishi giza, na neno mgao wa umeme halikuwa wimbo wa Taifa. Maajab zaidi bwawa la Mtera lilikuwa linajaa maji ya kutosha kuzalisha umeme! Kuanzia mid 1990s bwawa la Mtera 'lilipokataa' kujaa maji ndipo neno umeme lilipoanza kuambatana na neno 'mgao'.

Sasa kwa muhtasari wa mtititiko huo hapo juu Kobello unatakiwa useme -with evidence ccm (a) sera ya ccm kuhusu sekta ya umeme ni ipi? (b)wametekelezaje sera hiyo? (c) uwekezaji kwenye sekta ya umeme (d) kwa nini tuna mgao wa umeme?

Kama ccm wanatekeleza sera ya Mzee Mtei, IMF or the World Bank, je, wamefikia wapi na wamekwama wapi? Kama wamekwama kwanini? Na kubwa zaidi kwa nini waiamua kufuata sera ambayo sio yao?
 
Kwa maneno hayo ya kitaalam,basi CCM italaumiwa kwa kila kitu..so whats the point of trying to connect CCM na uwekezaji kwenye nishati?Since it's the only party that has been in power for the last 50yrs.
Kwanini mnachukua credits kwenye kupunguzwa kwa bei yza sukari na vyakula?Mbona mnaconnect hiyo na operation sangara?Kwani slaa ameshakuwa rais?
Kwanini mnachukua credits kwenye uundwaji wa katiba mpya?...kwani CDM,CUF,NCCR wamewahi kuhodhi serikali? Na mnasema mimi naenda nje ya topic kwani hapa tunazungumzia nini kama sio connection?
Au unataka nikuonyeshe maandishi ya watu wengine wataalam na sio makuli kama mimi walioambiwa na mtei kuwa kwenye maongezi yeye alisimamia kidedea matakwa ya IFM?
Hivi kwa mfano katiba mpya ikiruhusu serikali za kanda(federal/state govts) na zika fail vibaya kutakuwa na connection yoyote na CUF/CDM?
Nakuomba ukae kitako ufikirie kabla ya kukejeli watoa hoja,simply because you think you are an "expert" or sumthin.
 
Back
Top Bottom