Miradi Mikubwa ya Uzalishaji Umeme wakati wa Mzee Ruksa ni ipi? Toka hapo... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miradi Mikubwa ya Uzalishaji Umeme wakati wa Mzee Ruksa ni ipi? Toka hapo...

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 29, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu nimejaribu kukufanyia utafiti mdogo kwa ajili ya hoja yangu ambayo itaonesha kuwa tatizo la umeme Tanzania linahusiana na CCM hasa baada ya Rais Mwinyi, likaendelezwa na CCM chini ya Mkapa na sasa CCM chini ya Kikwete. Huwezi kuzungumzia tatizo la nishati hii nchini bila kugusa CCM. Hata hivyo, naomba mwenye kujua Rais Mwinyi alianzisha miradi gani mikubwa ya kuzalisha umeme akianticipate ukuaji wa uchumi?
   
 2. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Mimi wala sijui nikuwa bado natoka kamasi na kunywa maji ya bomba kwa kukinga mdomo kipindi hicho na umeme sikuweza kuuona mgao. Sijui ni miradi gani mwinyi aliianzisha waliokuwa na uwezo wa kujifuta kamasi watuambie miradi gani mwinyi aliyoifanya.
   
 3. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mwinyi ndie alieasisi na kuanzisha IPTL Tegeta
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Limbani kwa hiyo mradi wa IPTL ulikamilika wakati wa Mwinyi? Naulizia ile iliyokamilika katika miaka kumi ya Mwinyi.
   
 5. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  uko sahihi kuwa ni ccm na serikali zake baada ya awamu ya kwanza. wakoloni waliiacha hale na nyerere akaacha mtera na ndugu zake. mwinyi na mkapa hawakuona umuhimu wa umeme!!! ni kama waziri mkuu wa uingereza enzi za faraday ambae hakuona umuhimu wa maonesho ya kwanza ya faraday aliyoyafanya kuhusu ugunduzi wake wa umeme. faraday alimjibu kwa upole waziri mkuu huyo kuwa umuhimu wa maonesho yake atauona wakati watakapokusanya kodi na hivyo mapato ya taifa!!! wa kwetu wanashuhudia adha nchi iipatayo
   
 6. katabu

  katabu JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mmh. Mimi nakumbuka mwishoni mwa utawala wake ndipo tulikuwa tunaokota vishilingi moja vingi njiani, kisha tunavichezea, badala kwenda kununua bumunda. Nilikuwa bado kid.
   
 7. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Inabidi 2015 TAnzania iwe na Rais makini kama Dr.Slaa au S.Ahmed Salim ilituondokane na mibalaa hii na hata hivyo Mwinyi, Mkapa na huyu Sharobalo Kikwete pamoja na wafuasi wao wapelekwe mahakamani kujibu shutuma nyingi za ufisadi hasa Mkapa na Sharobalo Kikwete wanatakiwa wakanyee debe
   
 8. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Haya yote ni mambo ya privatization as championed by Mtei,ambaye aliasisi CDM.Serikali haikuinvest kwenye umeme wakidhani TANESCO itabinafsishwa,na nimeshasema mara nyingi kuwa privatisation/free market haitomfaidisha mwananchi wa kawaida.
  Baada ya mwalimu,kila mtu kivyake....sasa mnalalamika nini? si mlisema serikali haiwezi kuendesha kitu chochote?Waambieni hao private investors wachimbe mabwawa muone real charges za umeme.
  Privatisation ni siasa au ideology ya CDM,ila imewatokea puani sasa mnajifanya wajamaa na kutaka serikali iwekeze kwenye umeme...what the hell happened?
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Guys

  Naomba bora tuliangalie hili suala kwa marefu na Mapana maybe for once tungeacha ushabiki na kuwa walau objective kwenye kujibu au kuchangia hii mada. One would have thought kuwa kijireserach kidogo na hasa from someone who post ina forum that prides it members as GREAT THINKERS angeweza kuliangalia hili kwaupana zaidi. Issues za kutazama hapa ni zi fuatazo:


  -Current state ya Umeme Tanzania  -Makosa yaliyofanyika wakati wa liberalisation ya sekta ya Umeme  -Role ya NSSF kwenye hili itakuwa ni ipi?  -Je NSSF wanaruhusiwa na stakeholders wao kuingia kwenye hii biashara yak u generate umeme?  -Je kuna faida yoyote itapatikana kwenda NSSF?  -Je wenzetu wan je wanafanya vipi?


  Sasa majibu ya hapa yanaweza yakatoa mwanga walau kiasi mkaelewa why I support hawa jamaa kufanya mambo kama haya.
  Umeme Tanzania:


  Tanzania mwenye jukumu la generate, transmit and distribution ya umeme zamani ilikuwa exclusively TANESCO ambayo kama mjuavyo ni shirika la umma kwa asilimia 100 na wako responsible kupply asilimia 98 ya umeme Tanzania
  Statistics zinasema hivi:

  - Megawati 381 za umeme ambao tunatumia sasa hivi unatokana na vyanzo vya maji


  -Tanzania tuna uwezo wa kuzalisha mpaka Megawatt 5,000 ya umeme


  - Per capita electricity consumption yetu ni 46/KWh per annum, ambayo inakuwa kwa asilimia 11-13 au zaidi


  Hiyo ni moja kati ya sababu serikali inataka sana secta binafsi ziingie kwenye haya mambo ya kugenerate umeme. Mind you nchi ina watu milioni 40 na ni LESS THAN 10 % wako connected kwenye umeme. Serikali yetu pamoja na madudu mengi yanayotokea huwa ni competent kwa kujua matatizo ila tatizo huwa ni kwenye namna na njia ya kuyatatua hayo matatizo.

  Ndio maana kama mnakumbuka miaka ya 90's waliamua kulegeza masharti na kufanya reform kwenye hii sekta ya nishati na kuruhusu wazalishaji binafsi na hapo ndipo walipoingia the Songas na IPTL kwa nia ya kupunguza shedding, Of course it was not without controversy za akina RUGEMALILA (the same dude aliyeingia ubia na TRITEL) na mwishowe wakapelekana mahakamani, yaani IPTL na TANESCO lakini kujua haya yote inabidi uelewe connection kati ya EastCoast Energy v/s Independent Power Tanzania Limited (IPTL) v/s Songas v/s Ministry of Energy and Minerals (Wizara ya Nishati) v/s Parastatal Sector Reform Commission (PSRC) v/s Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) v/s VIP Engineering Limited (VIP), v/s (TANESCO) v/s NETGroup Solutions vs SIDASida) na bila kuwasahau waheshimiwa wa pale World Bank.  Lakini ukiachilia hao wauzaji wakubwa kulikuwa na wauzaji wengine wadogo kwa TANESCO, kama vile Tanwat (2.5 MW), Kiwira Coal Mine (6.0 MW) na bila kuwasahau Kilombero Sugar (2.5 MW) Mindhali humu kuna GREAT THINKERS nashauri mtafute Economic Recovery Program (ERP) ya 1986-1989 kati yetu na jamaa wa World Bank na IMF ndio mtaelewa kiini cha yoote haya ya reform kwenye sekta hiina zinginezo

  MAKOSA TULIYOYAFANYA:  1. POOR COORDINATION: Victim mkubwa hapa alikuwa ni ESI nah ii ilisababishwa na poor coordination. Kupitia wizara mabali mbali (jambo ambalo mpaka leo linaendelea) bilakusahau wadau na wahisani wakati uleee wa kujadili mikataba ya Songas na IPTL. Kama taifa we PAID A HEAVY PRICE. Of course itakuwa ni jambo rahisi sana kukaa hapa na kuanza mambo ya finger pointing lakini haya ndio yale yale kuwa hatutaki kutatua mambo madogo madogo kama ya COORDINATION imagine HAZINA vs NISHATI vs TANESCO vs DONORS vs EVERYONE !!!  2.POOR PRIORITIZATION: Tusijindanganye, evitable consequence of poor coordination is that power sector reforms have been neither clearly prioritized nor implemented na Serikali yetu. Mfano mdogo hatuna clear policy framework for private sector investment katika secta hii, issue skama target percentage of private generation, standard investment incentives and contractual norms kwa jili ya PPA. Bila kusahau kuwa hatuna clear and feasible roadmap for how to make the main off-taker financially and technically viable. Matokeo yake Sekta hii ya Nishati Tanzana in the last 20 years has the sector has gone from dealing with crisis after crisis (kwanza kiangazi cha miaka ya 90 then issue ya high capacity charges, na mengineyo), hii yote imepelekea kudelay of the planning and execution of fundamental reforms necessary for the long-term sustainability of power supply and expansion kwenye nchi yetu na mbaya zaidi hatujui hata priority zetu ziko wapi when it comes to alternative energy!!!! Yaani tumekuwa kama motto mkiwa asiye na baba wala mama wala ndugu wa kumtazama.
  3. FAIR AND INDEPENDENT REGULATION: Bila hii hatutofika na hakuna investor atakaye taka kuja kuinvest kwenye hiii sektaka kama hatuna transparency . Imagine kama regulator angekuwepo enzi zile IPTL na Songas wameanza it means akina Mhavile and Co wangekuwa wako bize kuzalisha umeme badala ya kushinda Mahakamani na kwingineko. Sasa hivi tunao EWURA lakini hao wamekuwa kama vile PPRA hawana nguvu zozote zile na sote tunajua no one knows or lets just say its unclear when truly independent oversight will commence. This fact may have cost the country past and present investments and may ultimately impact on future investments.  Sababu zingine ni kutokuwepo kwa uwazi kwenye UNFAIR BIDDING PROCESS, ARBITRATION , CURRENCY DEVALUATION na mengineyo bilakusahau kuwa tunashindwa kua attract makampuni ya uhakika kama TATA kwa kuwa we are not interested na pili hawa washazowe mambo ya transparency sie hayo hatutaki...!  ROLE YA NSSF


  Kwenye hili as far as I know NSSF itakuwa ni IPP yaani independent power Producer kama walivyokuwa wengine ila kazi ya distribution ni ya Tanesco hivyo kama wataleta ma generator yao au watatengeza wa Jua au upepo au Gesi toka songo songo thats up to them


  JE SHERIA INAWARUHUSU NSSF KUFANYA HIVI:

  I would imagine NSSF sio PPF so I cant see them getting involved na jambo ambalo liko kinyume au sheria haiwaruhusu kulifanya. Sina sheria Mama ya ambayo naweza ku quote lakini kama kuna IPP zaidi ya 10 Tanzania sidhani kama wameenda kinyume na sheria. Nadhani hii ipo kwenye investment policy yao so this shouldn't be an issue. Pia si vibaya mkajua kuwa shirika hili lina BOARD ambayo wao ndio wenye maamuzi ya mwisho kwenye mambo kama haya na ndani ya bodi wapo wawakilishi wa wafanyakazi sasa sidhani kama maamuzi yanaweza kufanywa na mtu mmoja

  RETURNS:

  Kama watu wa investment as far as I know ni kuwa kwa Tanzania inasemekana return ya investment kwenye umeme ni 300% sasa surely hapa naona ni win win situation kwa NSSF


  WENZETU NJE WANAFANYAJE?

  Malaysia, Philipines,Brazil,Vietnam,India, Jordan, Egypt na kwingineko Pension Funds zao wameinvest kwenye umeme na wanapata returns kubwa sana
  Btw TANESCO washankatia umeme ntarudi baadae.


  https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/101401-nssf-kutatua-tatizo-la-umeme-tanzania.html
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,344
  Trophy Points: 280
  Kobello, Ukisoma mpango wa maendeleo wa mwaka 1963 utaona TANESCO pamoja na kuwa shrika la umma lilikuwa na maamuzi yake, mfano kukataa leseni ya kugawa umeme Tukuyu, Musoma n.k. Dhana ya kulifanya liwe shirika huru si ya leo!!

  Makamba Jr amekiri wazi kuwa tatizo limeanza mwaka 1996. Wakati tatizo linaanza Mzee Mtei alishaacha kazi miaka zaidi ya 15 na sidhani sera zake alizotaka ziliwahi hata kufikiriwa. In fact kujiuzulu kwake ni kutokana na kutokubaliana na baadhi ya maamuzi.

  Kama privitization ni idiology ya CDM, sina tabu na hilo, mimi nashangaa unaposema sera hiyo imewatokea CDM puani. Sikumbuki siku CDM wamewahi kuongoza nchi hii, na kwahivyo naamini hawajawahi kupata fursa ya kutimiza sera zao kama walivyokusudia, nadhani tusiwasingizie.

  Tatizo la TANESCO linatokana na kuingiliwa sana kisiasa, imeonekana ndio mahali rahiisi pa kupitishia mirija ya watu. Angalia TANESCO ikiguswa utasikia Ikulu, BUNGE, na kila mtu anakimbilia huko. Si mbio za kusaidia sekta ya nishati ni mbio za kulinda maslahi.
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Matatizo yalianza wakati wa Mzee Ruksa hasa pale TANESCO ilipokuwa-earmarked kwa privatization. Tukumbuke wakati wa huu mambo mengi ya IMF yalikuwa implemented bila ya kuwepo na proper framework and no one knew or cared to think of the outcome. Na ni kipindi hiki IPTL ilikuwa 'imported' TANESCO being a mwali-mtarajiwa hakukuwa na investment yoyote then later on wazo la ku-privatize TANESCO likafifia but already TANESCO was in bad shape.

  Kuhusu IPTL - Yes, mambo yote yalifanyika wakati wa Mzee Ruksa (start to finish). Na Mgao wa umeme ulianza mara baada ya kifo cha aliyekuwa Managing Director Salvaroty Mosha- wakati wa Mzee Ruksa pia.

  Miradi mikubwa? uh... nchi ilikuwa inaendeshwa kwa gia ya 'zima moto' excpet for the occasional IMF plans!

  Tuje kwa Mkapa: Mkapa alipoingia ndio akaleta Vision 2025, na ili kufikia hiyo vision, akatengeza strategies (MKUKUTA). Sasa umeme unaongelewa sana kwenye MKUKUTA kama chachu ya maendeleo lakini in real sense investment imekuwa hakuna. NetGroup walijikita zaidi kwenye kukusanya madeni lakini hawafanya investment yeyote. Hata kuondoa tope kwenye bwawa la Mtera hawakufanya hawa watu badala yake waliishia kupaka majengo rangi!

  Kwa Kikwete: Huyu anajuwa sekta ya umeme kiliko kwani ndiye akikuwa waziri wa nishati wakati wa IPTL. Hata hivyo ni vigumu ku-pin point nini hasa anataka kufanya na hii sekta maana kaweka mezani miradi mingi iliyokuwa kabatini i.e Stigler power project, lakini amekuwa amekuwa kwenye gia ya 'dharura'.

  So TANU/CCM walijitahidi na umeme, lakini COOL/CCM - NIL.
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Kobello are you saying tatizo la umeme leo hii Tanzania limesababishwa na Mzee Mtei? Listen, nilitaka kuandika sana lakini popcorn zimeisha hivyo hawatengenezi tena wino! does that make sense to you?
   
 13. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Mtei alipojiuzulu,privatisation was not our policy,it came after his resignation.
  Mashirika mengi yliyokuwa profitable were privatised partly due to IMF policies,na serikali ikajitoa kuwekeza kwenye umeme kwa muda mrefu tu.
  Hata kama CDM wangekuwa madarakani wasingefanya cha maana,tulikuwa na umeme mwingi in the 70s than now,hakuna mtu binafsi atayewekeza kwenye umeme with current tarrifs,umeme lazima uwe chini ya serikali 100% la sivyo mtu wa kawaida hatoweza kuumudu.
  /CDM hawana plan yoyote ya kutatua tatizo la umeme,never had and never will.....whe you stand for something,you are ideologically responsible.....
  Wewe unafikiri kwanini hakuna private investment kwenye umeme?......sera yenu ni ipi?
   
 14. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Wewe rudi maktaba ukaangalie nani chanzo cha haya ma-barrick,IPTL,na vimbwanga vingine.....Mr. IMF na wenzake.
  Kama utakosa,jaribu kuangalia interview zake kuhusu role of the public sector.....hayo mambo ya popcorn na wino siyaelewi.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wakati Tanesco inakuwa earmarked for privatization, ilikuwa katika hali mbaya kwa kiasi gani?
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Naomba nijipe uenyekiti wa mada hii yangu; tayari nimeshaona dalili ya watu kwenda huko na huko. So twende taratibu. Tuanze na swali hili la kwanza na tukubaliane kabla hatujaenda huko kwingine. Miradi ya wakati wa Mwinyi ya umeme iliyoanzishwa na kukamilika hadi hivi sasa nimeambiwa ni ule wa IPTL. Je hili ni kweli?
   
 17. W

  Wanzagi Member

  #17
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  68 MW Pangani falls power station construction began in 1991 and commissioned late 1994
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Unazalisha at what capacity sasa hivi?
   
 19. W

  Wanzagi Member

  #19
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmh ndugu yangu mi nilidhani unaulizia mradi mkubwa uliojengwa wakati wa Mzee Ruksa. Accurate info za uzalishaji wa sasa itabidi uwatafute Tanesco ila kama sikosei kwa muda mrefu umekuwa ukizalisha 64 MW against 68 MW installed capacity
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  TANESCO wakati huo haikuwa na hali mbaya kihivyo na tunaweza kuifananisha na NBC (bank). Tatizo au source ya kuiweka kwenye privatization list ilitokana na hofu kuwa TANESCO isingiweza kumudu growing demand. Na hasa kwa kuangalia mtaji wakaona wanaihitaji capital injection plus efficiency kwenye kusambaza umeme - yaani connectivity. Na ilikuwa wagawe TANESCO in 3: Infrastructure, Production & Distribution. Infrastructure ingebakia serikalini. IPTL was the first company we can say ilikuja baada ya hii IMF-backed dismantalling plan. The rest is history!

  Sasa hivi wanataka kufanya hivyo hivyo- kugawa TANESCO in 3.
  IPTL - Mwinyi through & through.
   
Loading...