Miradi mikubwa inapokimbizwa iishe chini ya muda uliopangwa 'critical path methods' huzingatiwa?

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Wakuu humu Jf,

Nawasalim!
Kwa muda sasa nimekuwa nashangaa kusikia miradi mikubwa ya ujenzi ikiharakishwa ili imalizike chini ya muda aliopangiwa makandarasi. Huwa najiuliza maswali yafuatayo sipati majibu:

1. Miradi hii huzingatia 'critical path project management methods'? Na kama ndivyo, wanafanyafanyaje?
Nitoe mfano:

Ili zege la nguzo au beam likomae kuna minimum period (labda 3 weeks) ambao hauwezi kupunguzwa kwa mujibu wa codes za taaluma. Kwahiyo wanafanyafanyaje?

2. Kwa kufanya kazi usiku na mchana inabidi idadi ya baadhi ya laboures na wasimamizi wafanye over time kwaa malipo ya ziada na/au waongezeke ili wafike site kwa shift. Je hili nalo haliongezi gharama za miradi? Kama ndivyo, hizo gharama za ziada zinalipwaje na mbona wananchi hawaelezwi?

3. Kama ikitokea makandarasi ameharibu kazi kutokana na kukiuka miongozo (codes na 'critical path project management methods' etc) nani atawajibika?
 
Back
Top Bottom