Uchaguzi 2020 Miradi hii mikubwa ya barabara, maji kumpa kura za ndiyo Mbunge anayetetea Jimbo la Ilemela, Angeline Mabula

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Miradi hii mikubwa ya barabara, maji kumpa kura za ndiyo Mbunge anayetetea Jimbo la Ilemela, Angeline Mabula

MGOMBEA ubunge jimbo la Ilemela kupitia CCM, DK. Angeline Mabula amesema katika kipindi cha uongozi wake amefanikiwa kufanya kazi kubwa kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo ya miundombinu ya barabara na maji.

Kauli hiyo imeitoa jana wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Ilemela zilizohudhuliwa na wageni mbalimbali wakiwemo Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Moses Nnauye na Mbunge wa Magu aliyemaliza muda wake, Desdery Kiswaga.

Mabula amesema ndani ya miaka mitano kwa kushirikiana na viongozi wenzkae wamefanikiwa kujenga kilomita 37 za barabara kwa kiwango cha lami huku kilomita nyingine 51 zikiendelea kujengwa.

Amesema pia wamefanikiwa kufungua njia katika maeneo mbalimbali ya ndani ya wilaya ya Ilemela na kuzijenga kwa kiwango cha changarawe.

Mabula ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, amesema barabara za mitaa na nyingine zilizofunguliwa zina urefu wa kilometa 47

Mabula pia amesema kuwa kilomita hizo 47 zilizojengwa kwa nguvu za wananchi tayari zimechukuliwa na kuingizwa kwenye mpango wa wakala wa barabara za mijini na vijijini (Tarura) ili ziwekwe kwenye mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami.

Miongoni mwa barabara zilizojengwa kwa kiwango cha lami ndani ya miaka mitano ya Mabula ni ile ya Sabasaba - Kiseke - Busweru ambayo ilikuwa katika hali mbovu na kusababisha wakati mwingine kushindwa kupitika.

"Barabara tulizofungua kwa kiwango cha changarawe sio fedha za mfuko wa jimbo wala za Rais Magufuli ni nguvu za wananchi nyie wenyewe na kushirikiana na mimi na hii mmefanya kazi kubwa hongereni sana," amesema Mabula.

Mabula amesema kwa upande wa elimu, katika miaka yake mitatu pamoja na mambo mengine wamefanikiwa kujenga shule tatu za msingi kwenye wilaya hiyo.

Amesema katika kukamilisha ujenzi wa mindombinu ya shule hizo, wananchi wa Ilemela waliweza kujitokeza na kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni 311.

Katika upande wa maji, amesema wamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa miradi mbalimbali kwa kujenga tenki la maji eneo la Nyasaka lenye ujazo wa lita Milioni 1.2.

Pia ametaja maeneo mengine yalipojengwa matenki hayo ni mji mwema tenki lenye ujazo wa lita Milioni 1.2, Nyamhongoro tenki lenye ujazo wa lita laki tano na tenki kubwa la Busweru lenye ujazo wa lita milioni tatu.

Miradi ya maji iliyojengwa na Serikali kwa usimamizi wa Angeline Mabula, umegharimu kiasi cha zaidi ya Tsh. Bilioni 50.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilemela Nelson Mesha, amewashukuru wananchi kwa kukiamini chama hicho na kuwachagua viongozi kutoka chama hicho mwaka 2015 na kuweza kuwasaidia kutafsiri ilani ya chama hicho katika mambo mbalimbali ikiwemo kuchangia ujenzi wa madarasa.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James ambaye alikua mgeni rasmi katika uzinduzi huo alisema,kazi waliotumwa kwa miaka mitano wameifanya.

“Mwaka 2015 wakati tunakuja kuomba kura hapa barabara hii ya Sabasaba -Kiseke -Buswelu ilikuwa mbovu na watu walikuwa wanalalamika lakini sasa imejengwa na inapitika.

"Ilemela kulikuwa hakuna hospitali ya Wilaya lakini sasa tayari imejengwa pia katika kipindi cha miaka mitano mambo mengi yamefanyika ikiwemo hospitali, shule,reli,meli,ndege na vitu vingine hivyo nawashangaa wanaosema kuwa tumeleta maendeleo ya vitu wakati vitu.

Nape Nnauye amewashauri wananchi wa Ilemela kuacha kubadilisha mbunge au viongozi kama shati kwa kuwa mbunge anayemaliza muda wake amefanya kazi kubwa.

Mjumbe wa halmshauri kuu ya CCM Taifa Mnec Jamal Babu amewaomba wananchi wa Ilemela kumpa kura zote za ndiyo mgombea wa ubunge huyo wa CCM ili aweze kumalizia kazi iliyobaki.

MWISHO
 
Kwani katoa mshahara wake kuileta?

"Msitufanye wote wajinga"
 
Sio rahisi kihivyo, siku hizi watu wana akili aiseee
 
Ameshindwa kusaidia upimaji wa viwanja na kutoa hati kwa wanailemela japo ndo wizara yake
 
Nampa pole sana huyo mama, afanye kazi ya ziada hapa ilemela, Jana niliona mkutano wake hapo sabasaba, amesomba watu kwa mabasi ya ISAMILO kutoka sehemu mbalimbali kuja kwenye mkutano wake wakati inatakiwa watu wenyewe kwa mapenzi yao waje wakusikilize ili upime ushawishi wako.
 
Maji ni shida wilaya ya Ilemela Kiseke,buswelu,kahama,nyamhongolo maji hayatoki miezi sasa na futui jana walifutuka juu ya maji Ilemela ni shida. Barabara za mtaa nyingi zinapitika kwa shida,...bado anakazi
 
Back
Top Bottom