Miradi hii itekelezwe pamoja! (picha) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miradi hii itekelezwe pamoja! (picha)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 27, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Flyovers kama hizi:
  Pale Magomeni!
  [​IMG]

  Au za namna hii maeneo ya Ubungo!!
  [​IMG]

  Au pale kuzunguka Mnazi Mmoja!
  [​IMG]

  Kuna mradi wa vitambulisho na mradi wa kujenga flyovers! Binafsi napendekeza miradi yote hii miwili itekelezwe kwa wakati mmoja. As a matter of fact, sioni sababu ya kutangaza tenda, serikali au waziri achague kampuni anayoaimini ina uwezo kuliko nyingine na kuipitisha kutekeleza miradi hii.

  Haya mambo ya kuangalia sheria na kufuata taratibu za tenda kama ilivyo katika PPRA ya 2004 na ndugu yake wa 2005 ni kupoteza muda kwa sababu tutaishia kulaumiana tu. Tayari tumeonesha ni vigumu kwa viongozi na watendaji kufuata sheria hizi (kwani ni ngumu sana!).

  Vinginevyo tunachoweza kufanya ni kucheza bahati nasibu tu, weka makampuni 10 yanayogombania tenda, mtoto aitwe achomoe moja, yaishe!

  Miradi hii miwili inahitajika sana katika kuonesha kuwa Tanzania imeendelea! Ni miradi ambayo kila Mtanzania aniihitaji na kwa hakika itainua maisha ya mamilioni ya wananchi wetu.

  Maisha ya wananchi kama hawa wa Migori Mtera (picha na Mjengwa)

  [​IMG]

  au mjasiriamali huyu (picha na Mjengwa)

  [​IMG]

  Kama kuna mradi mwingine ambao unaweza kuunganishwa na miradi hii itakuwa vizuri ili tumalize miradi yote wanayoiwazia.
   
 2. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ukiacha hili la kununua mitambo ya DOWANS ambalo linaendelea na lile la mchakato wa vitambulisho vya Taifa, serikali pia imenunua rada ya Tshs 2.2bn kwa ajili ya mamlaka ya hali ya hewa. Swali langu hapa ni je uchumi wetu umekuwa kiasi cha mapato kuongezeka na hivyo kuona umuhimu wa kufanya mambo muhimu au ni kutokana na serikali transparent (uwazi) ya awamu ya nne ndiyo maana sasa tunajua transaction nyingi za nchi?

   
  Last edited: Feb 27, 2009
 3. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sehemu za nyanda za juu kusini kutakuwa na ngurumo na mvua za hapa na pale. Sehemu za kati kaskazin, ziwa victoria zitakuwa kavu......
  pepo za pwani zitavuma kusini Kaskazini na hali ya bahari itakuwa shwari!!!! ISIJE IKAWA KUNA MKONO WA MTU!!!!
   
 4. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Miradi hii ikianza utaona watu watakavyotajirika ghafla, na vikampuni uchwara vitakavyopata tenda za zege, nondo, taa za barabarani...Kati ya malori kumi ya mchanga, manne ya kigogo !! Bila hivyo miradi hii haitafanyika, kukiwa na ka-rushwa kidogo miradi inaenda haraka sana ili Wakubwa nao wapate chao.
  Kuna utafiti ulifanyika Brazil ikaonekana kwamba bila rushwa "to grease the hands of officials", nchi ingesimama, na biashara zote zingekufa. Je na sisi ifike mahali tukubali ukweli huu ???
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mradi wa kudumisha Muungano kwa kujenga reli itakayounganisha bandari ya Zanzibar na Daresalaam uendelee.
  [​IMG]
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji sijui kama ulisikia tetesi kuwa kuna mwanamfalme mmoja kutoka Uarabuni alitaka kutoa msaada wa kujenga daraja la kivukoni/kigamboni lakini alikataliwa kwa kuwa hakutoa 10 percent kwamheshimiwa aliyetakiwa kuidhinisha. Haya yote yanaweza kufanyika kama zikiwepo hizo 10 percent nyingi nyingi.
   
 7. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ebwana MMK hiyo picha ya kwanza inafaaa sana mitaa ya Kimara pale kama unashuka ubungo ila ndio tutabakia kuona tuuuu
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  CCM iking'olewa yote yanawezekana ,lakini ndani ya utawala wa CCM hakuna moja litakalokuwepo ni fedha kuliwa na wajanja wachache ,yaani unatafuta rada wakati hauna umeme ,maajabu haya ya karne ya 21.
  Dar kumejaa maguzo ya umeme ya taa za barabarani ajabu hakuna hata moja linaloonyesha japo dalili za kumwesa mwesa ,ni kiza tu utafikiri upo katikati ya bahari na taa za magari kama za wavuvi ,na taa za vibatali majumbani kama meli za kitalii.
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Sio hiyo ya mwarabu aliyetaka kujenga hilo daraja akaombwa ten percent tu; iko nyingine mfadhili alitaka kutupa grant ili tununue chakula cha kutusibu njaa, waziri akaomba apewe commission ya ten percent, yule jamaa akafuta msaada!!
   
 10. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Tatizo Viongozi wetu wa kibongo ni wabinafsi sana. mradi huu kwa ajili ya Dar es Salaam bado unazungushwa zungushwa mpaka leo, utekelezaji hakuna mpaka itakapo patikana namna ya kupata 10%.
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji hiyo miradi katika picha alizopiga mjengwa ndiyo hali halisi ya mahali pote katika nchi hii na hapa ndipo JMK anapata mahala pa kusimamia kuwa ametengeneza ajira 1500000 na anategemea kuvuka malengo kabla ya 2010. Kwake kazi kama hizi hapo anasema ame create ajira.
  Lakini najiuliza hizo data wamezipata wapi? Watupe analysis yake. Km atueleze nitegeneza ajira kwa kuingiza machinga kadhaa katika soko la ajira Dar, na mama ntilie kadhaa katika mkoa wa Singida na wabeba mizigo kadhaa katika mkoa wa Tanga na kadhalika. Hii ya kutuambia uongo kila leo, we are fed up.
  Mi nadhani hata hawa wataingizwa kwenye hesabu za kikwete. Is it?



  _IGP5605 i.jpg
   
 12. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MMKJ Salam Baba,
  Kabla hatujaunganisha miradi mingine kwanza tuondoke katika hali hii ya kuishi katika NCHI YA KUFIKIRIKA!!!!! JE hiyo miradi miwili uliobuni FEDHA zake unazo?????? au ndio mpaka TUKAOMBE???? Na MAENDELEO yepi yatakayoletwa na vitambulisho??? Na FLAIOVA la Ubungo au popote Dar es salam, una hakika kuwepo kwake ni MAENDELEO??? na yanamnufaishaje MWANAKIJIJI kama ambae hata ASPIRINI huipati baada ya mwendo wa maili kumi kuifuata ZAHANATI?????
   
 13. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Hakuna cha ajira 1.5m wala nini, watanzania wanadanganywa tu.
   
 14. B

  Bibi Ntilie JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 245
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asalaam aleikum, Bwana asifiwe, Mzee wa Kijiji, kama kawaida yako umechokoza ili watu waogelee katika kutoa mawazo yao.

  Mie nasema, muda wa kujenga hizo flyovers katika nchi yetu bado haujafika. Hata hapo utakapofika, utahitaji mipango madhubuti na ya muda mrefu. Hizo flyovers zikiwekwa Ubungo zitapita juu ya nyumba za watu?! Litaanza tatizo lingine la kuwaondoa mamia kama si maelfu ya watu na kuwalipa fidia zisizolingana na usumbufu watakaoupata.

  Watanzania wanaopasawa kufikiriwa na wanaohitaji maendeleo kwa wakati tulionao ni wenzetu walio wengi vijijini ili angalao na wao waweze kuonja raha za kimaisha za watu wa mjini kama kuwa na barabara za lami, umeme na maji ya bomba na shule bora zenye walimu bora. Bado vijijini mahitaji yao muhimu ni yaleyale tangu enzi za Uhuru ama "Enzi za Mwalimu" kama anavyotuambia Masanja Mkandamizaji. Kwa wale wazee kama mie watakumbuka kwamba moja ya juhudi alizozifanya Mwalimu ni kujaribu kubadili hali ya maisha ya wananchi wa mijini na vijijini kwa pamoja. Mijini wananchi walihamasishwa na kusaidiwa kujenga nyumba bora za kudumu badala ya zile za makuti, (makuti ya Magomeni Makuti yalitoweka 'enzi za Mwalimu' na zikasimama nyumba bora chini ya mpango wa ujenzi wa nyumba za mkopo za vyumba sita za National Housing) waliwekewa umeme na maji ndani ya nyumba hizo. Kama nakumbuka vyema, mpango huo haukuwa wa jijini Dar peke yake bali karibu miji mikubwa yote nchini ilifaidika na mpango huo. Vijijini nako walihamasishwa kuachana na nyumba za nyasi ama matembe badala yake wajenge nyumba madhubuti hata kama ni za miti na udongo zilizoezekwa bati, walioshindwa bati waliezeka kwa madebe. Mpango wa Serikali ulishirikisha wananchi kujenga barabara, shule na zahanati na wakati huohuo zilifanywa juhudi za kuchimba visima ili wananchi waweze kupata maji safi na kuondokana na kwenda mwendo mrefu kutafuta huduma hizo.

  Kutokana na matatizo mbalimbali ya kiuchumi na kisiasa, mpaka leo Serikali haijafanikiwa kufikisha maendeleo ipasavyo kwa wenzetu wote wanaoishi vijijini. Bado vijijini wanahitaji kuwa na nyumba bora, wanahitaji maji safi na salama, wanahitaji shule bora zenye walimu bora na si bora shule.

  Mimi nadhani viongozi wetu na sie Watanzania tunaoishi mijini tusahau kidogo habari ya maendeleo ya hayo ma-flyovers na miradi mingine isiyo ya lazima kwa sasa ambayo itaigharimu Serikali fedha nyingi. Nguvu, fedha na raslimali za taifa ni vyema zielekezwe kwa wenzetu walio vijijini ambao ndio wengi, ili na wao waweze kusogeleasogelea hali nzuri ya maisha. Mwalimu alisema Maendeleo ya kweli ni yale yanayolenga watu, si vitu. Ni bora Serikali ikatumia fedha hata kama ni kwa kukopesha, kuwajengea wenye vibanda vya udongo vinavyoonekana kwenye picha tulizobandikiwa humu, ili na wao waonje maisha ya kuishi kwenye nyumba bora zenye madirisha yanayoingiza hewa safi, kuliko kujenga flyovers ambazo zitatumiwa na wale ambao tayari wanavuta hewa safi ndani ya makasiri au hata wapanda daladala wanaoishi kwenye nyumba za block zilizoezekwa bati.

  Pamoja na hayo, Mwanakijiji, ukiwawekea watu wa Dar es Salaam flyovers ndio unawaambia baadhi ya wakazi wa jiji wazidishe ufisadi na uhalifu mwingine ili wawe na magari mazuri yanayoendana na sura ya flyovers!

  Wino mwekundu umenambia nimepotea kwa wiki kadhaa na kwa angalizo hilo nimetakiwa angalau nichangie au hata niulize swali. Nimechangia. Ukimya wangu unatokana na utu uzima! Nashukuru bado napumua.
   
 15. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Bibi Ntilie tambua kuwa over 70% ya mapato ya kodi hutoka Dar!

  Ni vema kwanza kuimarisha Dar ili kuweza kupata uwezo kuhudumia vijiji!
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Mar 1, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mmmmhhhhh.......
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Dec 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Flyovers za Dar zinakuja... nasikia ndio mahitaji makubwa kwa wakazi wa Dar
   
 18. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #18
  Dec 5, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Hivi kwanini tunapenda miradi ya kimjini? Kwanini TAZARA au Reli ya kati zisiwe na line mbili na za uhakika?
   
 19. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #19
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Flyovers si panacea kwa matatizo yetu. Tunapenda mno majibu mepesi kwa maswali mazito.Tatizo kubwa la flyovers ni kuwa zinaugawa mji. Badala ya kuangalia hayo magari yanayopita tujiulize mtembea kwa miguu atawezaje kuvuka kwenda upande wa pili!

  Njia ni kupunguza magari yanayoingia mjini. Hii inaweza kufanyika kwa kuimarisha public transport kiasi iwe viable alternative kwa wengi ( mabasi yaendao kasi, trams n.k.), kuweka njia nzuri na nadhifu kwa watumiao baiskele na miguu, na muhimu kuliko yote ni kuzuia ujenzi wa maghorofa mapya katikati ya mji na kufungua CBD nyingine ( Paris na La Defense), Gharama ya haya yote ni ndogo mno kulinganisha na hayo ma-flyovers.



  Amandla.......
   
 20. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #20
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,531
  Trophy Points: 280
  Flyovers for what? Kupunguza foleni au kupendezesha jiji? Kama option ya pili,ni ok kwa hao wanaDSM. Ila kama ni option ya kwanza,then it's not ok. Kwani flyovers will never solve traffic jams problem. Watu wanasahau kujiuliza chanzo cha kua na msungamano wa magari DSM na sasa Arusha na Mwanza kidogo. Tatizo lipo katika mipango miji. Ofisi zote kubwa,maduka na vitega uchumi vikubwa kwa DSM vipo posta na kariakoo. Sasa unategemea nini hapo. Ina maani wakaazi wote wa DSM asubuhi lazima waelekee huko iwe kwa private au public transport. Jioni wote wanatoka huko kurejea makwao! Kwa namna iyo hata zijengwe flyovers tatizo halitatatuliwa,ila litaongezeka zaidi. Suluhisho ni kwa mipango miji kupiga marufuku ujenzi wa ofisi na majengo mapya posta na kariakoo,na wa-encourage ujenzi wa satellite towns. Heko kwa TCRA kwa kujenga ofisi zao pale Sam Nujoma Road. Huo uwe mfano kwa makampuni na mashirika mengine ambao wanang'ang'ania kujenga posta na kariakoo ambako wanafanya traffic jams kua inevitable. Ni wakati muafaka kuanza ujenzi nje ya hayo maeneo,outskirts za jiji ziendelezwe kwa ujenzi wa ofisi muhimu,shopping centres (heko kwa mlimani city,ingawa huo mradi siupendi kabisa,hayo nitayazungumza wakati muafaka) na business centres. Na pia ni wakati muafaka kwa ofisi za wizara kwenda Dodoma ambako CDA imewatengea maeneo toka enzi za mwalimu. Utekelezaji wa haya utaondoa ulazima wa flyovers na tatizo la foleni DSM.
   
Loading...