Miradi ambayo nchi za Afrika zingefanya ili kuondoa utegemezi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miradi ambayo nchi za Afrika zingefanya ili kuondoa utegemezi.

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by DEVINE, Jul 9, 2012.

 1. DEVINE

  DEVINE JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 539
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Miradi ambayo kama nchi za Afrika zingeifanya ili kuondoa utegemezi wa nchi za Magharibi.:
  1.Kama kungefanikishwa uanzishaji wa kampuni ya RASCOM 1992.Ambayo ingeendesha satelaiti ya pamoja na kuondoa utegemezi wa kimawasiliano.
  2.Kuanzisha AFRICAN MONETARY FUND (AMF) kule Younde Cameroon mpango uliowekwa ili kuondoa utegemezi kwa IMF.Na kuwezesha African Investment Bank iliyo pangwa Sirte Libya,ingeondoa utegemezi wa WB kama ilivyo kwa Bank of the South kwa mataifa ya Amerika ya kusini.
  3.Miradi ya njia za uchukuzi ya pamoja mf.Reli kutoka Tanzania -South Africa kama ingekuwa kunamtapanyo na muungano wa reli Afrika nzima basi ingekuwa ni rahisi kwenye shughuri za usafirishaji bidhaa na mizigo mizito ndani ya bara.
  4.African community market,labda ingesaidi bidhaa zetu kuwa na thamani ndani ya soko la dunia kwani mataifa ya kigeni yangepaswa kununua kwenye soko la pamoja na si kwenye nchi mojamoja.
  5.Mfumo wa pamoja wa elimu na kubadilishana wataalamu,ingesaidia kukuza teknolojia na ubora wa elimu pamoja na ujuzi ndani ya waafrika wenyewe,na si kutegemea mataifa ya magharibi.
  JE UNADHANI KUNA LA ZIADA,hebu tushirikishane hapa.
   
Loading...