Mipango ya mapumziko ya mwisho wa mwaka

Nasema

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
556
344
Habari wana MMU?

Naam, mwisho wa mwaka ndio huo na festival season yakaribia.

Huwa napenda kusafiri kipindi hiki, ila kwa sasa naona nimeishiwa plans.

Naomba kwa uzoefu wenu mnipe ushauri wa maeneo ambayo mnaona yanavutia na yatatufaa mimi na laaziz wangu twende kupumzika. Iwe ni ndani ya nchi au nje ya nchi ni sawa.

Natanguliza shukrani kwenu.
 
Njoo Musoma aisee kuna sehemu nzuri sana za mapumziko ila mwambie laaziz abebe na PANGA kabisa maana hawachelewi kukinukisha huku hawa jamaa
 
Sehemu gani Musoma? Naomba details kamili.
 
Nenda Tarangire ukale kuku kwa mrija huku ukikodolea macho wanyama wetu au shuka Zenj ukapate marashi ya karafuu kwa raha zako.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kuna mbuga za wanyama kusini kama selous, kuna saadani, kaskazini (tarangire, manyara, ngorongoro na serengeti, hii inaweza kuwa round trip). Unaweza pia kwenda ruaha na mikumi. Kama unapenda nature na hali ya hewa iliyotulia kwa kipindi hichi cha joto, unaweza kwenda kupumzika lushoto ama udzungwa (camping is the best).

Kigoma pia kuna nice gombe reserves. Ingia tz tourist board kuna details nyingi za options zilizopo.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Nenda upumzike bilila kempsk utafurahi mandhari nzuri na hali ya hewa safi kwa msimu huu wa festival..uku ukijivinjali kwa roho safi na wife
 
Habari wana MMU?

Naam, mwisho wa mwaka ndio huo na festival season yakaribia.

Huwa napenda kusafiri kipindi hiki, ila kwa sasa naona nimeishiwa plans.

Naomba kwa uzoefu wenu mnipe ushauri wa maeneo ambayo mnaona yanavutia na yatatufaa mimi na laaziz wangu twende kupumzika. Iwe ni ndani ya nchi au nje ya nchi ni sawa.

Natanguliza shukrani kwenu.

.....what exactly are you looking for, maana kupumzika kuna kupumzika "jumla" mfano kule Pwani Mchangani beach resorts Zanzibar...wewe ni kula, kulala na swimming (ukitaka) au,....

Kujipumzisha ukiburudika na NATURE, mfano Game Lodges...(Game Drives)....au,

Kujipumzisha miji mikubwa (Nairobi, Dubai, London, etc) shopping included....au,

Kujipumzisha ukiwa na family & friends, hii yaweza ikawa mnafikia Hotel, lakini mna uwezo wa kuwatembelea 'old flames' ;)
 
Nenda Tarangire ukale kuku kwa mrija huku ukikodolea macho wanyama wetu au shuka Zenj ukapate marashi ya karafuu kwa raha zako.

Asante. Huko nilishaenda, ila na mpenzi wa zamani! Naona tabu kurudia na laaziz sasa!
 
.....what exactly are you looking for, maana kupumzika kuna kupumzika "jumla" mfano kule Pwani Mchangani beach resorts Zanzibar...wewe ni kula, kulala na swimming (ukitaka) au,....

Kujipumzisha ukiburudika na NATURE, mfano Game Lodges...(Game Drives)....au,

Kujipumzisha miji mikubwa (Nairobi, Dubai, London, etc) shopping included....au,

Kujipumzisha ukiwa na family & friends, hii yaweza ikawa mnafikia Hotel, lakini mna uwezo wa kuwatembelea 'old flames' ;)

Napenda zaidi kuexplore natural things na kufurahia uumbaji wa Mungu. Offcourse ndani yake kunakuwa na siku za kupumzika kabiiiisa kama ulivyosema beach, etc.
 
Kuna mbuga za wanyama kusini kama selous, kuna saadani, kaskazini (tarangire, manyara, ngorongoro na serengeti, hii inaweza kuwa round trip). Unaweza pia kwenda ruaha na mikumi. Kama unapenda nature na hali ya hewa iliyotulia kwa kipindi hichi cha joto, unaweza kwenda kupumzika lushoto ama udzungwa (camping is the best).

Kigoma pia kuna nice gombe reserves. Ingia tz tourist board kuna details nyingi za options zilizopo.

Sijafika Saadani, unaweza kunipa uzoefu wako? Napenda zaidi kupata maoni ya wateja waliotembelea huko kuliko kuangalia website za wamiliki wa maeneo. Nikivutiwa na wadau kama wewe hivi ndio natafuta zaidi kwao na travel & tours agents.
 
hakuna zaidi ya kaskazini ya Tanzania hasa kipindi hichi cha mwisho wa mwaka.
 
Napenda zaidi kuexplore natural things na kufurahia uumbaji wa Mungu. Offcourse ndani yake kunakuwa na siku za kupumzika kabiiiisa kama ulivyosema beach, etc.

....haya, nenda Zanzibar, Mafia au Mombasa for "Sun, Sea & Sand"
 
daah unafaidi sana

so kila ukiwa na shemeji mpya unatafuta kiwanja kipya pia??

Lol,,nenda kale sato mwanza

Napenda kutembelea viwanja mbalimbali, sipendi kurudia, sio lazima kwa mpenzi mpya ni mi mwenyewe tu napenda!!
 
Ukapumzike kwa kazi gani ya maana uliyolifanyia hili taifa?
 
Back
Top Bottom