Nairobifly
Member
- May 3, 2012
- 75
- 26
Ndugu zangu nikiwa katika pitapita zangu hapa mjini Morogoro, nilikutana na watu 2 waliovalia nguo za ccm wakiwa ktk mazungumzo na mikakati ya kuiba kura ktk uchaguzi mnamo tarehe 14/12/2014. Nilipata kumsikia mmoja wao akisema, kiukweli chama kina hali mbaya na wapinzani wanaweza kuchukua vijiji na vitongoji vingi, sasa cha kufanya hapa ni mwendo wa KUIBA KURA TU NA HII ITAKUWA KWA NCHI NZIMA. Aliendelea kusema kuwa CCM ikipata kura 2 na CDM/CUF 100 cha kufanya hapa ni kugeuza matokeo tu CDM 2 na CCM 100. Alisema mbinu hii ni kwa nchi nzima na itakwenda sambamba na utoaji wa rushwa kwa wakala wa upinzani. My take: ndugu zangu tujiandae kukabiliana na hawa wezi ccm. source mimi mwenyewe.