Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,237
- 34,183
Wakuu wengi wa hizi taasisi ni wazee wasio na exposure na wasio na uthubutu. Haya mawazo watayatoa wapi? Na ukiwapa watakuelewa?Kama ni mimi ningepewa mamlaka/kazi ya kuliekebisha hili.
Ningetumia hawahawa wanafunzi wa DIT,UCLAS,Ardhi,UD--na technical colleges wafanye projects za ku-design miji mipya--kila chuo ningekipa wilaya moja ya ku-design--na hapa kila group ya wanafunzi ipewe kata 1.Kuwe na makazi,viwanja vya michezo,barabara,dampo,mipangilio ya miti na huduma zote muhimu za kijamii(mini-towns)--kama hizi Town creator..
Kungekuwa na namna ya ku-rate na kuzitumia hizi designs zao katika kupanga miji--kwa ushauri wa kitaalamu kutoka kwa hawa "maprofesa" wenye ujuzi zaidi.Maeneo ambayo tayari yanamilikiwa na watu binafsi--yapewe uhuru wa kuendeleza au kuuza.
Tatizo elimu yetu iko kwenye vitabu zaidi---unakuta hawa urban planners---hajawahi ku-design chochote maishanii mwake.
hata hizi shule na mahospitali tunayojenga---wataalam wangepewa pro-bono--wajitolee--kwa ajili ya taifa---taifa liwe na templates kama 10 zilizorasimishwa---kamwe tusingekuwa na vishule vya ajabu ajabu mtaani...the same kwa maduka,open spaces,viwanja vya mipira etc
Ni mawazo yangu tu--lakini kama ingetumika hili wazo tungeweza kufika mahali--tuache SIASA.
3D Site Plans drawing example
Hizi hapa chini ni urban gardens--zilizopo Copenhagen--duara moja lina nyumba kuanzia 16 hadi 20...Na maeneo yote TZ hili linatushinda kweli?
View attachment 1727833View attachment 1727834View attachment 1727835