Mipango miji ilikuwa enzi ya mkoloni, sio sasa

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,800
Unapotembea katika miji mikongwe au maeneo waliyoishi wakoloni hasa Wazungu utaona jinsi miji ilivyopangwa maridhawa. Barabara zimenyooka, nyumba zimejengwa kwa kupangwa sawia, viwanja vina ukubwa unaolingana, maeneo ya kupumzika maeneo ya michezo, bustani n.k.

Kichefu chefu ni pale unapotoka nje ya mji kwenda maeneo yaliyopimwa na wataalamu wetu wenyewe tena wenye nchi yao. Kwanza barabara hazieleweki, unakuta eneo ni tambalale lakin barabara zimepinda pinda. Unakuta barabara inaanza pana,mbele nyembamba tena imeishia kwenye nyumba ya mtu. Nyumba zimebanana na hazina mpangilio.

Nyumba moja imeangalia kusini ingine magharibi. Nyumba kubwa nzuri ya vigae pembeni kuna vibanda vya magunia na masalfeti. Yaani ni vululu vululu. Sijui sisi raha yetu ya maisha nini.

Hivi mipango miji wetu huwa wanapima nini au mipango miji yetu inanamna yake ya kupanga tofuti na wenzetu?

Nchi yetu ni kubwa sana, maeneo mengi yako tupu na hayatumiki kwa chochote kwanini tubanane? Kwanini tushindwe kuwa na maeneo mazuri ya kupumzika,michezo na burudani kwa watoto na familia?

Siku hizi watu wanajitahidi sn kujenga nyumba nzuri shida ni mpangilio. Nakumbuka waziri mkuu alisisitiza sn kutengwa kwa maeneo ya burudani kwa maeneo yote mapya yanayopimwa, japo sioni kama kuna kuna utekelezaji.

Naiomba serikali iweke sheria kali kwanza ya kuwasimamia mipango miji, lakini pili kwa raia watakaovunjwa sheria za ujenzi holela. Jamani tunatia aibu! Aliefika Mbeya ataamini ninachosema.

Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio ut

Ndio utajua tofauti za kufikiri kati ya watu.
 
ukweli mchungu huu!
tujichunguze vizuri, pengine kuna kitu kimekosana ila wenyewe hatujijui na hawa weupe wanajua ndo maana baadhi yao wanatunyanyasa na wale wasiotunyanyasa wanafanya hivyo kwa shingo upande. ni kama kuna kitu wanaogopa tutawaambukiza.
si barabara tu, hata katika baadhi ya taasisi. fika Kibaha Boys High school uione sasa na uombe picha ya zamani ilipokuwa mikononi mwa wenyewe.....utalia! fika Lindi sekondari na uombe picha ya zamani ilipokuwa mikononi mwa wahindi na uilinganishe na ilivyo sasa.....utachoka!!
 
Kunasehemu moja Iringa nilipita kuna kamwinuko kidogo halafu kuna bonde zuri la tambalare, nimepita hapo tena mwaka jana mwishoni, kwakweli nimesikitika kwa jinsi walivyojenga kiholela na tayari pamesha jaa. Ukiwa kwa juu unamulikwa na reflection za mabati, yaani wangejenga kwa mpangilio mzuri pangependeza sana.
 
Sipendi hii Hali, nakumbuka viwanja vikigawiwa utashangaa, unaambiwa tu haya ww kiwanja chako mwisho hapa.

Kuanzia hapa mpaka hapa ni barabara, daaah hivi tukoje
 
Mimi Mbeya naijua, ukiangalia mji wa Sokomatola Hadi majengo, japo kwa Sasa nyumba ni kuukuu, lakini mpangilio ulikuwa vema sana, njoo makunguru, mwanjelwa, nenda mama John, isanga, shuka simike kule, Hadi nzovwe, daaaah! Unachoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom