Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,865
- 3,800
Unapotembea katika miji mikongwe au maeneo waliyoishi wakoloni hasa Wazungu utaona jinsi miji ilivyopangwa maridhawa. Barabara zimenyooka, nyumba zimejengwa kwa kupangwa sawia, viwanja vina ukubwa unaolingana, maeneo ya kupumzika maeneo ya michezo, bustani n.k.
Kichefu chefu ni pale unapotoka nje ya mji kwenda maeneo yaliyopimwa na wataalamu wetu wenyewe tena wenye nchi yao. Kwanza barabara hazieleweki, unakuta eneo ni tambalale lakin barabara zimepinda pinda. Unakuta barabara inaanza pana,mbele nyembamba tena imeishia kwenye nyumba ya mtu. Nyumba zimebanana na hazina mpangilio.
Nyumba moja imeangalia kusini ingine magharibi. Nyumba kubwa nzuri ya vigae pembeni kuna vibanda vya magunia na masalfeti. Yaani ni vululu vululu. Sijui sisi raha yetu ya maisha nini.
Hivi mipango miji wetu huwa wanapima nini au mipango miji yetu inanamna yake ya kupanga tofuti na wenzetu?
Nchi yetu ni kubwa sana, maeneo mengi yako tupu na hayatumiki kwa chochote kwanini tubanane? Kwanini tushindwe kuwa na maeneo mazuri ya kupumzika,michezo na burudani kwa watoto na familia?
Siku hizi watu wanajitahidi sn kujenga nyumba nzuri shida ni mpangilio. Nakumbuka waziri mkuu alisisitiza sn kutengwa kwa maeneo ya burudani kwa maeneo yote mapya yanayopimwa, japo sioni kama kuna kuna utekelezaji.
Naiomba serikali iweke sheria kali kwanza ya kuwasimamia mipango miji, lakini pili kwa raia watakaovunjwa sheria za ujenzi holela. Jamani tunatia aibu! Aliefika Mbeya ataamini ninachosema.
Nawasilisha
Sent using Jamii Forums mobile app