Mipango Kabambe iwe ndio mkataba na kipimo cha mafanikio kiutendaji ya Wakurugenzi/ Mameya/ Wabunge ma Madiwani wa Halmashauri za Miji yetu

Kamukhm

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,625
2,000
Mipango Kabambe Master plan, ni dira ya maendeleo ya mji/taasisi, ambayo huandaliwa kwa kuzingatia Ushirikishwaji wa wadau na ushauri wa kitaalamu wa taaluma zote.

Huu mpango unaeleza kwa ujumla mahitaji ya msingi ya mji, namna bora ya kuyafikia mahitaji haya, na majukumu ya kila mmoja katika kutimiza mahitaji haya ili kuleta tija kwa umma wote iwe kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiteknolojia.

Hii mipango inaandaliwa kwa fedha nyingi sana. Na TAMISEMI wanalipa wakandarasi kuandaa hii mipango, ambayo ukiisoma hakuna mji masikini. Miji yote ni vibrant na inter connected vizuri kuleta maendeleo jumuishi.

Kwa mujibu wa document hizi, biashara zimeshamiri, afya zimeboreka, kuna matumizi mazuri na uwekezaji unaleta tija kubwa katika matumizi ya fedha za serikali.

Kwanini yote haya hayatokei!? Kwa mujibu wa mpango!?

1) Mipango inaandaliwa kama dili tu au requirement za kupata fedha na sio vipaumbele vya halmashauri na serikali kwa ujumla.

2) Siasa imechukua usukani toka kwa wataalamu, matokeo yake miji inaendeshwa kwa matamko ya watu wasio wataalamu na ushauri usioongozwa na tafiti

3) wananchi wamedekezwa,. Na hawapendi kufuata sheria na taratibu. Kwa eneo hili nazungumzia kuheshimu mpango kwa kuutekeleza kama inavyotakiwa. Moja ya maeneo wananchi wanakochangia ni kupitia uvamizi wa maeneo Tengefu na kulia lia kwa wanasiasa.

Nini kifanyike
Kama nilivyosema kupitia Kichwa cha Uzi huu.

Kwa kuwa mpango Kabambe (Master plan) ni mawazo ya wananchi tena yaliyoongozwa na utaalamu, basi yafuatayo yafanyike.

1) Mafanikio ya wakurugenzi yapimwe kwa kiwango cha utekelezaji wa master plans na sio makusanyo kama ilivyo sasa.

2) Sera/ilani za wagombea zijengwe juu ya namna ya kutekeleza master plan (mpango kabambe). Hayati Mzee Benjamin Mkapa alisisitiza juu ya kuwa na "Continuity" nadhani hii ndio itakuwa Mwarobaini.

3) Halmashauri na Serikali kwa ujumla ijenge utamaduni wa kusimama na sheria (kuboresha utawala wa kisheria) bila hivyo matamko yanaweza kutumika vibaya na watu kwa manufaa binafsi ikiwemo kupata umaarufu katika siasa.

4) Mipango ya halmashauri iibuliwe kutoka katika mahitaji orodheshwa ndani ya Master plan. Sio kuibuka ni miradi ambayo haitakuwa na uhusiano wenye tija na miradi.iliyopo tayari, inayoendelea au itakayokuja.

#Mungu Atujalie mafanikio tele katika kazi zetu. Na Alibariki Serikali yetu na Viongozi wake. Amin.#
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,813
2,000
Umesahau ni bwana yule ndio anaamua nini kifanyike,hao watendaji wa halmashauri unawaonea tu.
 

Kamukhm

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,625
2,000
Umesahau ni bwana yule ndio anaamua nini kifanyike, hao watendaji wa halmashauri unawaonea tu.
Lakini swala La Ugumu wa utekelezaji wa master plan sio swala jipya.. limekuwepo tangu enzi za mwalimu, likashamiri wakati wa mzee wa ruksa na kuota mizizi nyakati za hayati mzee Mkapa na Mh. Kikwete.

Ni swala tunalohitaji kulitafutia Mwarobaini. Ili kuboresha mazingira ya kufanya kazi na biashara nchini.
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,813
2,000
Lakini swala La Ugumu wa utekelezaji wa master plan sio swala jipya.. limekuwepo tangu enzi za mwalimu, likashamiri wakati wa mzee wa ruksa na kuota mizizi nyakati za hayati mzee Mkapa na Mh. Kikwete.

Ni swala tunalohitaji kulitafutia Mwarobaini.. ili kuboresha mazingira ya kufanya kazi na biashara nchini.

Mkuu nakubaliana na wewe ‘ performance’ ya mtu ndio imuweke ofisini , italeta ushindani baina ya watendaji ambayo ni nzuri kwa afya ya utendaji, lakini pia hii system itawaibua watendaji wale incompetent hivyo kuwa exposed na kuachia office🤣🤣, nimeipenda topic yako
 

Kamukhm

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,625
2,000
Mkuu nakubaliana na wewe ‘ performance’ ya mtu ndio imuweke ofisini , italeta ushindani baina ya watendaji ambayo ni nzuri kwa afya ya utendaji, lakini pia hii system itawaibua watendaji wale incompetent hivyo kuwa exposed na kuachia office, nimeipenda topic yako
Na ukweli ni kuwa huwezi kujitungia mtihani na ujisahihishe mwenyewe.

Kwa upande wa vyama Ilani ziandaliwe kwa kuzingatia mipango kabambe.. ikiwemo mipango ya maendeleo ya nchi..

Wengi watajikuta sio competent.. :) hasa eneo la wabunge na madiwani.. wanaibukaga na hoja hazina kichwa wala miguu kuwafrustrate watendaji kisa yalikuwa ahadi za kampeni..

Hapana tuweke akili yetu sote kwenye uelekeo mmoja
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,813
2,000
Mimi nadhani nafasi pekee ya kugombaniwa kisiasa iwe ni urais tu na yeye mamlaka yake yaishie kwenye kuteua mawaziri tu! Wabunge, madiwani na watendaji wengine wapewe kazi baada ya kudemonstrate wanaweza kutekeleza hayo majukumu, na wapewe muda initially mdogo wa kuonyesha uwezo wao, wakivurunda out of office! 🤣🤣🤣😉😉😝, hii itatenganisha siasa na kazi, ambalo ni tatizo linalosumbua utendaji katika halmashauri, ubunge nchini
 

Kamukhm

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,625
2,000
Mimi nadhani nafasi pekee ya kugombaniwa kisiasa iwe ni urais tu na yeye mamlaka yake yaishie kwenye kuteua mawaziri tu! Wabunge, madiwani na watendaji wengine wapewe kazi baada ya kudemonstrate wanaweza kutekeleza hayo majukumu, na wapewe muda initially mdogo wa kuonyesha uwezo wao, wakivurunda out of office! , hii itatenganisha siasa na kazi, ambalo ni tatizo linalosumbua utendaji katika halmashauri, ubunge nchini
Waheshimiwa ukienda na muswada huu lazima wakuazimie bila kujali tofauti za kisiasa.

Kwa sasa wengi hata hawajui kwamba wanagombea.. ila lazima uwaone wanarogana.. kila.kitu kimekuwa stahiki kwanza..

Na wenye uwezo waogopa madaraka maana hakuna Sehemu ya kuuonesha huo uwezo.. ni business as usual.. komaa.uchaguliwe ukimaliza kaa kula maisha
 

Kamukhm

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,625
2,000
Kwanini mada kama hizi za ki-Azimio la Arusha huwa zinakosa wadodosaji au wachangiaji!?

Ni ubinafsi, au kuhisi mawazo kama haya yakifanyiwa kazi yanaondoa uhuru wa viongozi kukaa kitako!? Kula na kunenepeana!?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom