Mipaka ziwa Victoria kufutwa, tz tuko tayari kugawa ziwa?

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Jul 28, 2008
2,502
739
Jamani, mipaka ya ziwa victoria watu wanataka kuifuta, ili kusiwe na mipaka kabisa. ziwa victoria linahitajika sana kwa uchumi wa kenya pamoja na kwamba wanamiliki asilimia 6% tu ya ziwa, ila wana viwanda vingi na wanazalisha samaki wengi viwandani kuliko uganda na tz. Samaki kwenye kaeneo kao wameisha, wanachukulia kisiwa cha migingo na mgogoro wake kutaka kufuta mipaka ili waje wavue samaki huku kwetu pia ambako sisi wenye ziwa kubwa tulilinda mazalia ya samaki wetu kwa kukamata na kuchoma nyavu nyingi za kokora pamoja na kuwapeleka jela wanachi wetu.

Hivi tz tuko tayari? wengi wanasema, ati, hii sisi wananchi hata tukipita makelele, hata ile ya ardhi ya EAC, haituhusu, kwasababu wanaoamua ni viongozi wetu na sio sisi, hivi Tz ya aina hii bado ipo? mbona hapa tz siku hizi maamuzi yanakuwa ya wananchi? tuwe macho, viongozi wetu wasituburute tukajikuta wameingia mikataba ya ajabuajabu, wakahatarisha maliasili zetu kwa kuwagawia majirani zetu wanaotutukanaga kuwa sisi hatuna akili hatujasoma na hatujui biashara kazi yetu ni kukaa kwenye mkeka kupiga soga na kula kipunga.

kama kuungana kwenye jumuiya ya afrika mashariki ni muhimu, basi, tunataka MIPAKA YETU YOOOTE ILINDWE, ARDHI YETU ILINDWE, MALIASILI ZETU ZILINDWE ZOOOOTE, tena kikamilifu. la sivyo, watu watakuja wajiuzuru hapa. Mungu ibariki Tanzania.
 
Duh watoto wa kambo wa njaa, then walete dhereu. Haiwezekani we don't need them bana. Wako so hypcratical na warongo. Waendelee kugombea kisiwa chao tu
 
Duh watoto wa kambo wa njaa, then walete dhereu. Haiwezekani we don't need them bana. Wako so hypcratical na warongo. Waendelee kugombea kisiwa chao tu

teheteheeee, ni kweli, kisiwa kidogo kama kile wanakuwa wagomvi, je, siku tukija kubambaruka tukataka ile mipaka irudi, si watachukua mitutu ili waendelee kuneemeka na ziwa la watz na waganda? kwasababu kaziwa asilimia 6% ka kwao hakana samaki wa sasa, hadi viwanda vingi tu kule Kisumu vya samaki vinafungwa. sasa wanataka kuvua kwetu. umenichekesha unaposema "warongo"
 
naona watu hawamsapoti ubongoubungo hapa,,,,mimi namsapoti asilimia zote kwakweli, mipaka ya tz lazima ilindwe na isifutwe kwa maslahi ya wageni. yaani wakenya.naona hapo wakenya watakuwa wamefika mbali kwakweli. hivi inawezekanaje ati?
 
Nyie endeleeni kuukalia uchumi ,jamaa hawalali wanavua usiku na mchana na msishangae kama kama kuna mtu keshapokea 10% ,yeye hata wakivua mpaka mayai ya samaki hana wasiwasi maana hajali maisha ya wengine ni yake binafsi tu.
 
What do you mean wanataka kufuta mipaka ya Ziwa? Unamaanisha boarder yetu inafutwa ama kenya wanatake kutumia eneo la ziwa letu kwa uhuru zaidi! Sidhani kama kunakiongozi yeyote wa nchi mwenye akili timamu anaweza kufuta mpaka wa ziwa kwani atakuwa anafuta mipaka ya nchi!
 
Jamani, mipaka ya ziwa victoria watu wanataka kuifuta, ili kusiwe na mipaka kabisa. ziwa victoria linahitajika sana kwa uchumi wa kenya pamoja na kwamba wanamiliki asilimia 6% tu ya ziwa, ila wana viwanda vingi na wanazalisha samaki wengi viwandani kuliko uganda na tz. Samaki kwenye kaeneo kao wameisha, wanachukulia kisiwa cha migingo na mgogoro wake kutaka kufuta mipaka ili waje wavue samaki huku kwetu pia ambako sisi wenye ziwa kubwa tulilinda mazalia ya samaki wetu kwa kukamata na kuchoma nyavu nyingi za kokora pamoja na kuwapeleka jela wanachi wetu.

Hivi tz tuko tayari? wengi wanasema, ati, hii sisi wananchi hata tukipita makelele, hata ile ya ardhi ya EAC, haituhusu, kwasababu wanaoamua ni viongozi wetu na sio sisi, hivi Tz ya aina hii bado ipo? mbona hapa tz siku hizi maamuzi yanakuwa ya wananchi? tuwe macho, viongozi wetu wasituburute tukajikuta wameingia mikataba ya ajabuajabu, wakahatarisha maliasili zetu kwa kuwagawia majirani zetu wanaotutukanaga kuwa sisi hatuna akili hatujasoma na hatujui biashara kazi yetu ni kukaa kwenye mkeka kupiga soga na kula kipunga.

kama kuungana kwenye jumuiya ya afrika mashariki ni muhimu, basi, tunataka MIPAKA YETU YOOOTE ILINDWE, ARDHI YETU ILINDWE, MALIASILI ZETU ZILINDWE ZOOOOTE, tena kikamilifu. la sivyo, watu watakuja wajiuzuru hapa. Mungu ibariki Tanzania.

Hii ni hatari kama ni kweli inabidi kupigana kweli kweli hakuna kukubali mambo ya kuondoa mipaka hawa jamaa waharibifu na pia hawana utu. Situnao mitaani ni vigumu hawa ngudu zetu wa EAC kukaa nao maana watz wako tofauti na wao wote.

Hivyo kukubali kuondoa mipaka ya ziwa, ni kukubali ziwa letu liondoke maana in no time itakuwa hatari kwani wataharibu kila kitu hafadhali tuendelee kuwekana sawa tutunze raslimali zetu. Hakuna kushare.
 
I think we are getting it wrong! Kama vikira zipo katika uzalishaji na matumizi ya ziwa, na sisi ndio wamiliki wakuu! swala ni kwamba tunagawanaje faida! Kuwa na mtaji mkumbwa katika ubepari ni lazima uwe na nguvu za kufanya majadiliano! sio kufuta tu mipaka! Wakenya wananguvu ya kuvua zaidi yetu - sasa tujipange vipi ama kuweka conditions zipi tupate faida kutoka kwenye production zao!

Pili, swala la kufuta mipaka ni katika matumizi tu na sio umiliki! Hilo liainishwe wazi kabisa! Tusiletewe hadithi za abunuwasi badaye!

Tatu, kama tunafuta mipaka lengo ni tuongeze uzalishaji na pato sio kuonyesha ni jinsi gani tu wakarifu ama tunaenzi pan-africanism bila kuifahamu.
 
Soko la samaki aina ya sangara ulaya lilikuwa likitegemea nchi ya Kenya miaka ya themanini lakini hali ilianza kubadilika mwanzoni mwa miaka ya tisini kwa Tanzania kuanza kuexport kuliko Kenya.

Wakenya wanalijua hili ndiyo maana wanataka mipaka iondolewe ili viwanda vyao vilivyoamia Tanzania kwasababu ya kufuata malighafi viweze kurejea Kenya.

Shirikisho la afrika mashariki kuanzishwa kwake kunategemea zaidi kupata maliasili za Tanzania na soka la bidhaa za Kenya kwa nchi zote wanachama.Wakenya wamejaribu kuingiza vipengele kama ardhi wameshindwa sasa wanataka tuondoe mipaka ya ziwa Victoria hivi wanafikiri Tanzania hatuna uwezo wa kufikiri ?.

Tunapaswa kukataa kwa nguvu zetu zote kama tulivyofanya katika suala la ardhi na makazi ya kudumu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom