Mipaka ya kazi kati ya Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,338
5,263
Nadhani kuna tatizo hapa la kutoelewa mipaka ya kazi kwa kila mmoja wao, na hasa kwa upande wa Msigwa ambaye kadri siku zinavyosonga mbele anaanza kuwa na tabia kama za Cyprian Musiba ama za Bashite.

Nasema hivyo kwa sababu kwa kiasi kikubwa sasa ukifuatilia accounts za Msigwa social media mambo mengi anayopost ni maoni yake binafsi na wala siyo "MAWASILIANO YA RAIS", na wala siyo MAWASILIANO YA IKULU".

Kwa kiasi kikubwa namwona pia anadandia kazi za Dr.Abbas, Msemaji Mkuu wa Serikali ama kazi za Humphrey Polepole, Msemaji wa CCM.

Kwamba kuna daraja limejengwa Kamachumu ama Serengeti ama Mayanzani kule kwa Mwigulu hayo si mawasiliano ya Rais ama Ikulu, unless Rais alikuwa na kazi ya kufanya maeneo yale ama somehow aliyataja madaraja ama miradi mingine ya huduma za kijamii iliyokamilishwa na serikali katika maeneo hayo.

Msigwa anapaswa kutuwasilishia kazi za Rais na si kazi za serikali kwa ujumla wake, HE HAS TO BE PROFESSIONAL, aache uzuzu!
 
Amucha waa waungwana.

1.Kuna tofauti gani kati ya Msemaji wa Serikali na msemaji wa Ikulu?

2. Je kati ya Gersoni Msigwa na Hassan Abbas, ni nani mkubwa au anawajibika kwa mwezake katika mgwanyo wa madaraka na utendaji?
 
Wa ikulu ana report issue zinazo muhusu Mh Raisi, Makamu wa Rais.

Wa Serikali ana report Issue za wizara, Sector , na taasisi za serikali.

Ntizamo wangu tu huo.
 
Unapozungumzia Ikulu unazungumzia muhimili mmoja wa Rais na wasaidizi wake. Lakini unapoongelea serikali unamaanisha mihimili mitatu yaani bunge, mahakama na Taasisi ya urais.

Hivyo Dr. Hassan Abbas is the bigger than Greyson.
 
Unapozungumzia Ikulu unazungumzia muhimili mmoja wa Rais na wasaidizi wake. Lakini unapoongelea serikali unamaanisha mihimili mitatu yaani bunge, mahakama na Taasisi ya urais.

Hivyo Dr. Hassan Abbas is the bigger than Greyson.
Sawa mkuu
 
Back
Top Bottom