Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Mar 3, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,309
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Naangalia TBC Live, Rais Jakaya Kikwete yuko hewani!
  Miongoni wa mazuri ya JK, ni having a good sense of humour, akiongea, huchoki kumsikiliza!.
  Alipokuwa akiongelea kilimo cha ndizi kijijini kwao Msoga, Bagamoyo, akasema wakulima wana bananisha migomba mingi kwenye shina moja, matokeo yake kila mgomba unatoa kichane kimoja au viwili ya vindizi vilivyokondeana!.

  Akasema wanakijiji wale wanalima hivyo kwa sababu hawajui kuwa kama wakiacha mgomba mmoja kwenye shina moja, mgomba huo utatoa mkungu mkubwa wa ndizi, na ndizi zenyewe zitakuwa ni ndizi za shibe kama "Mrisho Mpoto"!. Ukumbi mzima ulizizima kwa vicheko, watu hawana mbavu!.

  Kuwa na 'good sense of humour' ni kipaji na ni miongoni mwa mambo mazuri machache ya rais wetu Jakaya Kikwete, besides good looking!.

  Kwa wale wenye kumbukumbu ya hotuba za Mwalimu, ukiondoa ile hotuba yake ya kutangaza vita, hotuba za Mwalimu, watu walikuwa wanacheka na hutamani amalize kuzungumza!.

  Hii ni thread ya miongoni mwa mazuri ya JK, kama na wewe unalo zuri lolote la JK ambalo unalijua, unaweza kuliweka.

  Kwa vile tunazungumzia mazuri, ningeomba wale ambao hawana zuri lolote la kuzungumzia JK, sio lazima mchangie, wala zuri hili la "good sense of humour", haimaanishi JK sasa ndio rais bora kwa Tanzania, wala haina maana ndio hana mabaya yake!, leo tuzungumzie mazuri yake!

  Angalizo:
  Wanabodi wenzangu, tunajukumu la kujimoderate sisi wenyewe kulinda hadhi ya jukwaa letu, haiwezekana kila siku sisi tukawa ni watu wa kulalamika tuu, au kubonda tuu, mara moja moja kwenye mazuri, pia tutoe sifa pale panapo stahili!.

  Natanguliza Shukrani kwa kunielewa!

  Asanteni!

  Paskali

  Note: Paskali sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali ni muumini wa ukweli "seek the truth, and the truth will set you free"!. Kwa wale wanaofikiri Paskali ni mshabiki wa CCM, tafuteni thread yangu ya "CCM Imechokwa" !.


  --------------------------------------------
  Hoja Nyingine za Thread ya kibananhukhu iliyounganishwa #148
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  we have a very outgoing president, no doubt about it...but what about other leadership issues?
   
 3. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Jk ana moyo wa subira sana hata kwa yale anayozushiwa ana uvumilivu wa kukaa kimya bila kuwatisha wazushi,uhuru wa kujieleza sasa upo juu kuliko kipindi chochote tangu mungu kaumba dunia hii!!,mgogoro wa Znz kaumaliza bila ya watu kutegemea,wanafunzi hata wa div 3 sasa wana uhakika wa kupata shahada, kaikumbuka sana mikoa ya magharibi kuliko Rais yoyote wa Tz kabla yake.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,309
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ndahani, hiyo "outgoing", nayo ni sifa, huko ndiko kuwa "mtu wa watu"!. mimi nimeziweka mbili, hiyo ya good sense of humour na good looking!, hizo nyingine, naomba uzireserve kwa thread yake, kwa sababu hizi nilizoziweka mimi ndio inawezekana zilizotufanya tumchague in the first place!, kwani imefanywa research yoyote kuangalia Watanzania wanachagua nini, au wanaangalia nini ndipo wachague?!. Njua research iliyofanywa Marekani, wakagundua wanawake wengi wanapenda kumchagua mtu kutokana na "good looking"! na "the way he speaks"!, kwa vile huku hatujafanya utafiti rasmi, miongoni mwa sifa za kuteuliwa CCM, ni jee mgombea, unauzika?, anakubalika?, anatazamika?, anachagulika?, unapitishwa!, sinauhakika kama wanaangalia, jee ana uwezo?!.
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Can mods make this thread sticky even for one day? Obviously no!!
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,309
  Trophy Points: 280
  Mkuu Songoro, hiki ndicho ninachokisema kulinda hadhi ya jukwaa letu, pamoja na mabaya yake, pamoja na ubovu wa time yake, pamoja na madhaifu yake kama binadamu yoyote, pia anayo mazuri, anayo mema, etc, mara moja moja kwenye mazuri tukubali kuyakubali na tusifie, na kwenye uborongaji tuendelee kuwabalasa ili wafanye kila walivhopaswa kufanya!. Humu jf, tuna wenzetu wengi wana ugonjwa unaitwa "hate" bila wao kujijua, hivyo kujikuta wanaishia kuwa "hate preachers", kwao hakuna jema, ni chuki tuu kwa kwenda mbele!.
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Yeah, sense of humour na kujionyesha kuwa karibu na watu lakini sera zake zinawakumbatia zaidi wanyonyaji na mafisadi.
  Afadhali hata angekuwa comedian badala ya kuwa kiongozi wa nchi.
   
 8. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pasco

  leo umeleta thread ya maana hebu tujaribu kuzungumzia japo mazuri machache ya Jk. Hakuna binadamu asiye na zuri hata moja

  Mimi nitamkumbuka kwa kutununulia Panton la magogoni - Kigamboni. kabla ya hapo ilikuwa ni mateso.

  Panton kubwa Afrika Mashariki na kati hadi Mwai kibaki alikuwa kuliona alipotembelea Tanzania na akaahidi kuwanunulia wakenya

  Linabeba magari 60 na abiria 2000

  Na sasa ujenzi wa daraja la Kigamboni umeanza
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  nakubaliana na wewe Pasco...tuliocheza chipukizi tunaelewa unamaanisha nini. Ndo maana enzi nilikuwa naamini kwenye ukubwa na uzuri wa iliyokuwa USSR. Kwa hili la kilichotufanya tumchague ni kipi, kimenifanya nifikiri tofauti na kwa kuanzia nimeamua kukumbuka ule wimbo wetu maarufu ulioonyesha ukuu wa USSR, National Anthem of USSR - YouTube.
  President wetu angelikuwa ni mmoja ya watu vipenzi wa watanzania maana alituvutia kwa mengi, lol!
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280

  Jasusi, mtoa mada anashauri tujadili kwanini alichaguliwa kwa "kishindo". Ingawa inawezekana kukawa na kufeli kwa "kishindo vile vile"
   
 11. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nitamkumbuka Jk kwa


  katiba mpya.
  kwa chuo cha Dodoma
   
 12. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,110
  Likes Received: 10,462
  Trophy Points: 280
  nitamkumbuka jk kwa kucheka cheka kwake kwani ni rais pekee anayeongoza duniani kwa kukenua hata kama niwakati ambapo hatakiwi kukenua. Pia hilo ni jambo zuri jk alilo jitahidi kulifanya nitamkumbuka sana.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,309
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jasusi, kwani Watanzania huwa wanaandaliwa kuchagua nini?. Kama kuwa karibu na watu, ku smile nao,kufurahi nao kwa kuwachekesha (sense of humour) kunakufanya upendeke na kuchagulika, then why not?. Hii inamaana hiki ndicho Watanzania tulichotaka!.

  Mimi nilitanguliza fani ya habari ndipo baadae nikaenda UDSM, nikiwa mtaani niliona jinsi magazeti ya udaku, yanavyonunuliwa kwa wingi!. Nilijiaminisha kuwa magazeti hayo ya udaku yana nafasi kubwa mitaani nikijifariji kuwa washabiki wakubwa wa magazeti ya udaku ni hawa wenzetu walioishia darasa la saba!. Nilipofika UDSM, sikuamini nilipokuta ni magazeti hayo hayo ya udaku ndio yanayoongoza kwa mauzo pale UDSM!. Nimeishi Mabibo hostel miaka 4, ikifika saa mbili usiku TV zinahamishiwa Channel Ten kuangalia "muziki"!.

  Ninahudhuria sana mikutano mingi ya kampeni, burudani na Ze Comedy ndio wanaochukua muda mrefu zaidi na burudani zikiisha, ukifika muda wa kumwaga sera, makundi makubwa ya watu, hujiondokea!. Hii inamaanisha hicho ndicho Watanzania wanachotaka!.

  Kwa mfano msomi mzuri mwenye Ph.D ya kuondoa umasikini akigombea ubunge wa Temeke na Juma Nature, unadhani nani atachaguliwa?!. Lets appreciate baadhi ya mazuri ya rais wetu na tuache kubeza kila kitu!.
   
 14. n

  ngwini JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nitamkumbuka kwa kupata CPA na faida za kuwa m2mishi wa Umma nikiwa kijana na kupewa u-chief accountant..maana bila CPA hauwez kuwa chief
   
 15. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Fundi sana wa kuwahadaa wananchi; he never takes things seriously!!
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sawasawa. Ngoja na mimi nichangie ninayoyajua kwa nini Kikwete alipata 80% supposedly katika uchaguzi wa 2005.

  Ukiangalia tulikotokea tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa (1992) ni CCM peke yake ndiyo iliyokuwa na ujuzi na uwezo wa kucheza mchezo wa uchaguzi wa kura. Mwaka 1995 Mrema alikuwa maarufu sana lakini alichezewa rafu na CCM kwa sababu upinzani haukujua mchezo wa kushinda kura.

  Come 2005 Kikwete aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania lakini nina hakika Watanzania hawakujua Kikwete ni mtu wa aina gani, personality wise and leadershipwise. Kwa sababu kama Kikwete angekuwa mtu anayejiamini hakuwa na sababu ya kununua waandishi wa habari kumpamba kwamba ni mwanasiasa mkomavu wakati ukomavu wake hata haujathibitika. Kikwete hakudebate na mgombea yeyote kwa hiyo uwezo wake wa kujenga hoja na kujieleza haukuwa challenged. Ni kama vile alipata free pass.

  By 2005 Watanzania wengi waliamini kuwa CCM peke yake ndiyo inayoweza kutoa kiongozi makini kwa sababu baada ya kufifia kwa Mrema upinzani haukuwa na mtu yeyote ambaye angeweza ku challenge CCM. Hiyo ndiyo sababu Kikwete alishinda kwa kishindo.

  Sasa miaka mitano baadaye Watanzania walishagundua ubabaishaji wa Kikwete, kwamba si mtu mwenye uwezo wa kushughulikia matatizo ya nchi, ni mbabaishaji, na anapenda kuzungumza tu bila kuchukua hatua. Na kadri ninavyoona, ni huo huo ubabaishaji wa Kikwete ambao umesababisha/utasababisha kupungua kwa umaarufu wa CCM come next election.
   
 17. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  That's very true, everytime he speaks, he always find ways to make people laugh.
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  JK angekuwa the best ever president kama tu
  'angebahatika' kuwa na the best and the brightest around him
  na angekubali kuwa 'hajui'
  na anahitaji kusaidiwa......kwa sababu ana sifa nyiingi mno za kiongozi wa kuwa kiongozi bora...

  1.kwanza anapenda sifa ya kuonekana anaweza
  2.pili ni msikivu na mvumilivu na hana papara
  3.ana personality ya a 'movie star'
  watu wanampenda tu hata kama wanajua hawezi
  4.anapenda watu.....haoni tabu kuchanganyika na watu
  5.anapenda anasa,hii angeweza kuitumia kwa faida.mfano anapenda kuvaa suti za gharama
  basi angehakikisha tuna viwanda vya nguo za quality anayotaka

  but too bad mshauri wake mkuu ni Yussuph Makamba
   
 19. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  mie tabasamu lake kila na popote pale akikunja uso kuonesha hasira n secunde tu utaona tabasamu... sijawahi ona akitoa hutuba ikanifurahisha kwani zote sio za kweli
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu wamekusikiliza!
   
Loading...