Songambele
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 4,695
- 2,553
Da labda kwanza tukupe pole mtoa mada , inawezekana kabisa hujui mengi ila Daktari kayakanyaga mwenyewe mwishoni kabisa kwa kuonyesha nia ya kuisigina katiba ili aurithi ufalme, yaani kama Mchonga angekuwa presidaa daktari saa hizi alitakiwa awe detention kama Shekh Jumbe. Mama ana dini kaona kiroho safi wampeleke mjengoni.Mabibi na mabwana kwa yanayotokea huko CCM kwa wengine kina sisi, hayo ni mambo ya Ngoswe.
Hata hivyo kama binadamu ambapo wengine huwa hawana huruma, wengine tumeumbiwa na roho za huruma. Ashukuriwe mola muweza wa yote.
Ni ukweli ulio wazi kuwa mh. Dr. Bashiru, Pole pole na vigogo wengine mliokuwa vinara kwenye awamu ile, tokea kuondoka kwa mwendazake kama mlikuwa hamjui, tathmini ya utendaji wenu na hata kukubalika kwenu katika jamii ndiyo hii mnayoiona sasa.
Bila ya shaka mtakuwa sasa mmejielewa vyema na pasi na shaka yoyote. Kwamba sasa mambo ni hadharani. Hakuna cha unafiki wala nini. Hii ni timamu kabisa ndani na nje ya CCM.
Ukweli mchungu:
"Ni wazi kuwa hamkuwa mkipendwa wala kukubalika kwenye chama wala katika jamii. Mlikuwa wababe mliopitiliza, mliokuwa mmejisahau. Hamkuukumbuka hata ule usemi wa kuwa - Dunia Mapito."
Kwani ni lini basi mwenye macho alisubiri kuambiwa tazama? Au ni lini afukuzwaye aliwahi kuambiwa toka? Labda kama ni mgeni na imegonga hadi siku ya kumi!
Ukweli mchungu zaidi ni kuwa, enyi machampioni kabisa wa awamu ile katika serikali na katika CCM, hamkuwa mkikubalika kabisa, kiasi kuwa katu hamuwezi kutosha tena kwenye awamu ya sita.
"Ni vipi awaye yote aweze kuwa rafiki wa Mungu na Shetani kwa wakati mmoja? Hii ndiyo changamoto ya wazi inayowakumba sasa."
Si mnamwona wanayemwita katelefoni anavyokuwa kama kanyeshewa mvua?
Muda wa kutumia busara zenu za kisomi ulikuwa sasa, kujiengua wenyewe kwa maslahi ya nchi na chama hiki, kama kweli mlivipenda.
Zaidi sana kama kweli mnadhani mliyokuwa mnayasimamia kwenye awamu ile yalikuwa na mashiko, bora mngefikiria kuanzisha hata chama chenu cha siasa chenye agenda hizo mkapata kuendelea kuzipambania.
Wakuu, kunyong'ong'onyezwa hivi mpaka mnatia huruma hadi lini? Hamjionei huruma wenyewe? Hata hamshauriani wenyewe kwa wenyewe?
View attachment 1771352
Mbona mko wengi wa kutosha mkisheheni hadi maaskofu wafufua wafu kwenye hilo ambalo leo linaitwa kuwa ni genge lenu?
Mh. Dkt Bashiru, pole pole na timu yenu, mbona kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi?
Wapiganaji wanasema "Aluta Continua." Kazi inapoendelea, hebu mapambano na yakaendelee!
Ninawasilisha.
Hawa watu ni wakatili sana kuliko unavyojua na ungewajua hawatakiwa hata kutajwa manake jalali ndio ameamua kuwe na mabadiliko haya baada ya kuona nafsi katili za viumbe hawa.