MINJA na Ukiritimba katika upandishaji vyeo: {kitengo cha Utumishi Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Ufun | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MINJA na Ukiritimba katika upandishaji vyeo: {kitengo cha Utumishi Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Ufun

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pasco_jr_ngumi, Aug 23, 2012.

 1. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ina ukiritimba katika upandishaji vyeo na kubadilisha muundo wa utumishi.kutokana na utekelezaji wa waraka namba 1 wa mwaka 2011 kuhusu kuwabadilisha kazi/ kupandishwa vyeo wenye kumb. Na.PSC/TSD/FA.405/452/01/21 wa tarehe 13/1/2012.

  Kutokana na waraka huo baadhi ya Taasisi zimetekeleza wito huo na watumishi waliojiendeleza wamebadilishiwa muundo wao kulingana na waraka unavyosema. Kitendawili kipo katika kitengo cha utumishi katika wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Makao Makuu.

  Tangu waraka utolewe Januari hakuna kinachofanyika bali kila siku huitisha nyaraka hizi leo mpaka inafikia mwezi wa sita kwa jambo ambalo ni la kawaida na hakuna bajeti kuwa ataongezwa fedha . Kubadilisha muundo ni suala la mfumo iweje idara zingine mambo yote tayari isipokuwa katika kitengo hicho? Hapa kuna tatizo na hata kupandishwa vyeo ni mgogoro.

  Katika mfumo wa utumishi kitengo nyeti kama hicho anaachiwa Afisa mmoja kushughulikia maslahi ya kikazi. Kila ukienda katika ofisi hiyo namba 55c utaambiwa kasafiri au yupo kwenye shughuli maalum.

  Shughuli hiyo maalum ni ipi isiyoisha na kuwashughulikia walalahoi kutoka mikoani? Mbaya zaidi ofisi hiyo imekuwa mali ya mtu badala ya kuwa ofisi ya umma.

  Kuna watumishi wamepandishwa vyeo kutoka mfumo wa zamani wa kujiendeleza kwa kupata shahada na kupewa Afisa Elimu daraja la II TGTS D Kutoka Afisa Elimu Msaidizi mwandamizi TGTS F. Lakini cha kushangaza miongoni mwa walimu ambao walistahili kupelekwa katika mfumo huo njia fupi ilitumika na kupelekwa moja kwa moja TGTS G kama Afisa Elimu daraja la I.

  Kama kweli ni halali inawezekanaje kumaliza mafunzo ya shahada mwaka 2008 na leo hii kuwa katika ngazi ya TGTS G au H? Kapanda cheo kabla ya waraka huu mpya wa Januari 13, 2012. Ikiwa alipewa daraja la ngazi la TGTS D kwa miaka hii mitatu na nusu inawezekanaje afikie G au H kwani kila ngazi /daraja hutumikia kati ya miaka minne hadi mitano. Sasa kutoka D angefikia E mwaka2011 na kutoka E kwenda F angefika mwaka 2015.

  Kwa sasa watu hao wapo G wengine H kwa muda mfupi kweli vigezo vimezingatiwa wakati wengine wamemaliza miaka hiyo hiyo wapo kwenye D.

  Na kila kukicha huambiwa leta hiki mara kile. Nionavyo kuna aina Fulani ya upendeleo kama kweli vyeti na vielezo vyote vipo kwenye mafaili ya kieletroniki kwanini zoezi hili liende kwa namna hii? Hapa kuna kitu , na huyo anayehusika na uandikaji na upandishaji huonekana mungu mtu katika kitengo chake.

  Kwa mfano, kwa hivi sasa wizara imepungukiwa na mzigo wa watumishi wa kuwahudumia kupandishwa madaraja baada ya walimu wa sekondari kuhamishiwa TAMISEMI.

  Watumishi wachache tu waliobaki kwa katibu mkuu kama vyuo takribani thelathini na tano , ukaguzi na ndani ya wizara yenyewe. Sasa kitendawili hiki tangu waraka unatolewa Januari inachukua miezi mingapi kutoa hizo barua? Hali hii ndiyo inayosababisha madeni kwa watumishi kwa kuchelewesha kutoa barua kwa wakati .

  Ofisi kuu inayohusika na Utmishi iliangalie suala hili kwa jicho pevu kuwa kuna uzembe wa aina Fulani na upendeleo wa aina yake katika kupandishana vyeo. Kama kweli yupo pekeyake waongezwe wengine ili zoezi liende haraka.
   
 2. m

  mama visa Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :flypig:hiyo ni kweli kabisa wasomi tukomae madaraja yabadilishwe kihalali na si upendeleo
   
 3. hendeboy

  hendeboy JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  haya yote madhara ya ccm jamani tujitahidi 2015 wasirudi
   
 4. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  haaaaa........... yaani huyu MINJA NA BAKARI wameifanya wizara kama yao!!!
   
Loading...