Kikao kilikuwa cha mawaziri Kikwete kwa kupenda sifa akajikaribisha kuna siku atakuja kukosa kiti asimame kama wale jamaa nyuma.Sorry, naomba nitoke nje kidogo. Of course hata huyo asiyesinzia naye amelala tu si unaona kabisa anaangalia picha tu. Well, nitaomba kusaidiwa in case hii obsrvation yangu si sahihi.
Kwa haraka haraka simwoni rais mwingine zaidi ya our cheap president. Hivi kwanini hakumwacha huyo anayelala hapo aende peke yake? Hiki kikao si cha marais I'm sure waandaji hawakumtarajia ndio maana unaona wamemrundika hapo maskini. Its high time rais wetu awe na aibu kidogo mbona alishasafiri sana alipokuwa minister hachoki tu? Mbali ya hasara tunayopata lakini pia tunonekana hamnazo sisi wote inakuwaje rais anakuwa na muda mwingi hivi wa kuzurura?
Hii nchi inaoboa sana.
Nafikiri akili yako iko obsessed kwa ushabiki mtu anaonekana kabisa amelala wewe unasema anapiga kope duh.Jamani,
Hiyo ni Kamera tu alikaa upande akachukua wakati mheshimiwa ameinama. Au wakati anapiga kope (eye twinkling). Thread inataka kuleta uchochezi usio na maana. Swala la kujadili ni hili lifuatalo:
Mkao huu unaonyesha wazi kabisa ni conference ya kawaida ambayo hata wahudhuriaji wake si mawarais au mawaziri bali executives wa taasisi, na sitoshangaa kuwa they are not even senior executives. Ingekuwa ni marais ingekuwa Summit na mkao wake usingekuwa wa namna hii kama vile watu wanavunja kamati ya harusi.
Nimejaribu kumwangalia Ngeleja strait kati ya ngeleja na jamaa aliye kushoto kwake kuna mzungu kama vile anamwangalia JK, sijui jamaa anawaza nini, kumwona rais wa nchi kubwa kama TZ eti anahudhuria kikongamano cha junior officers kama hicho. Jk is not even there, hicho kitabu anachosoma ........ni kama hakihusiani na mkutano huo maana hakuna mwingine aliyeshikilia kitabu kama hicho.
Ngeleja seems to be bored, alichokikuta sicho alichotegemea. Imagine waziri unaambiwa utakutana na maprofessor badala yake unakutana na wahudumu wa ofisi. Ndicho anachowaza poor Ngeleja, wala hajasinzia hapo. anajisikia aibu mno maana inaonekana hakuna hata waziri mwingine yeyote kutoka nchi zingine, ni yeye tu. Poor him
ngereja ndo kapiga mbonji kabisa.. alafu mbayuwayu anazuga na kijarida... i gues kitakuwa cha katuni
no mater what hat mimi ninamtetea Ngereja hapoa hajalala jamani,labda anatafakali tu giza lililopo huku Bongo,kweli wana tukera ila jamani tuwe realistic hapo Ngereja hajalala
Bobby....Sio kweli kwamba mkwere hakupaswa kuhudhuria hii yeye pia anahusika.....soma hii The 5th EITI Global Conference in Paris is now underway. Heads of states, government leaders, companies and civil society organisations are gathered today and tomorrow at the OECD in Paris to share how EITI has led to improvements in their country and how to shape the future of the EITI.
As an international forum, the Conference is a platform where EITI Board Members, International Secretariat and EITI stakeholders can discuss key issues with each other, the broader international community, while engaging new countries to join the effort in transparency over financial revenue in the extractive sectors. Source ya hii habari ni Paris 2011 | Extractive Industries Transparency Initiative
Kama mawaziri ndio wanalala hivi kwenye mikutano kumbe basi ndiyo maana Mkwere anakwenda kuwakilisha mwenyewe. bure kabisa!
Nadhani pamoja na mapungufu ya jk na waziri wake, jambo la kujadili ni hili hapa juu. Kwa muonekano tu tuna hali ngumuJamani,
Hiyo ni Kamera tu alikaa upande akachukua wakati mheshimiwa ameinama. Au wakati anapiga kope (eye twinkling). Thread inataka kuleta uchochezi usio na maana. Swala la kujadili ni hili lifuatalo:
Raisi Kikwete akifuatana na Membe (MB) na Ngeleja (MB) walienda Ufaransa kuhudhuria mkutano ulioandaliwa na EITI (Extractive Industries Transparency International) yaani mtandao wa kimataifa unaotetea uwazi kwenye mapato yatokanayo na rasimali chimbwa yaani Madini, vito, gasi na mafuta. Mzee Bomani ndiyo anayosimamia chapter ya Tanzania.
EITI Tanzania kama itasajiliwa kisheria watatakiwa kila mwaka kutangaza (to publish) na kuanisha mapato yote yanayotokana rasilimali chimbwa inayopata nchi. Sasa hivi tuko kwenye mchakato wa Tanzania kuwa mwanachama wa EITI kama tutatimiza masharti ya kuwa wazi kwenye mikataba na mapato.
Mwaka jana bunge lilipitisha sheria ya madini iliyopingwa sana na upande wa upinzani kwa sababu ya vipengele vya usili katika mikataba na sector hii. Lakini kwa sababu wabunge wa chama chetu ni wengi ikapitishwa. sheria inatoa hata adhabu kwa yule atakaye divulge siri zinazohusiana na mikataba hii. Hivyo basi kabla ya JK kwenda Ufaransa alitakiwa kwanza kuyafanyia mambo haya ya msingi kwanza ili watanzania wawe huru kua access mikataba hii na kujua hasa nini kimewekwa humu. Ngoja niwamegee kidogo tu mapato tuliyopata kutokana na rasilimali chimbwa so far:
Aina ya mapato kwa nchi Shilingi za kitanzania Revenue collected on behalf of the government (hizi ni PAYE na NSSF) 66,129,144,000.00 Total Taxes (yaani Corporate tax, withholding tax, SDL (Skill development levy), import duty, fuel levy ni zero yaani hawalipi na sector specific taxes yaani (loyalties - Mrahaba wa aslimia tatu kama matusi vile?, License na permit fees, mineral concessions, kaprofiti wanakopata TPDC, Local government levy - Zile dollar laki mbili wanazolipwa kule Tarime, Geita na Kahama na devidends inayopata serikali kwenye makampuni kwa sasa hivi ni sifuri) 62,293,938,000.00 Jumla kuu 128,423,082,000.00 Asilimia ya mapato kutoka na kodi ya wafanyakazi wa rasilimali chimbwa 51% Mchango wa kodi za makampuni moja kwa moja 49%
*data hizi ni kwa mwaka 2008: nazo zimepatikana kwa taabu kweli
*Kile wanachodai makampuni wamelipa kwa serikali na kile serikali inachokiri kulipwa vinatofautiana. Sijui wamekunywa? Mtajaza wenyewe, sie tunasonga mbele. Naomba kuwasilisha wana JF.
* Yaani kodi ya wafanyakazi wa migodini na kwenye gas eti ndiyo tegemeo kubwa la mapato ya serikari.
Kwenda ufaransa ni aibu tupu, sijui wanafukuzia masurufu ya safari tu hawa!