Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,906
- 22,036
Nilihisi mapepo yako bungeni Dodoma tu kumbe hadi Ufaransa? Kazi ipo
TUMEZOEA KUMWONA MH KOMBA AKISINZIA NA KUKOROMA DODOMA SASA HUYU SIJUI TUMWITE JINA LA MNYAMA GANI
TUMEZOEA KUMWONA MH KOMBA AKISINZIA NA KUKOROMA DODOMA SASA HUYU SIJUI TUMWITE JINA LA MNYAMA GANI
Jamani,
Hiyo ni Kamera tu alikaa upande akachukua wakati mheshimiwa ameinama. Au wakati anapiga kope (eye twinkling). Thread inataka kuleta uchochezi usio na maana. Swala la kujadili ni hili lifuatalo:
Raisi Kikwete akifuatana na Membe (MB) na Ngeleja (MB) walienda Ufaransa kuhudhuria mkutano ulioandaliwa na EITI (Extractive Industries Transparency International) yaani mtandao wa kimataifa unaotetea uwazi kwenye mapato yatokanayo na rasimali chimbwa yaani Madini, vito, gasi na mafuta. Mzee Bomani ndiyo anayosimamia chapter ya Tanzania.
EITI Tanzania kama itasajiliwa kisheria watatakiwa kila mwaka kutangaza (to publish) na kuanisha mapato yote yanayotokana rasilimali chimbwa inayopata nchi. Sasa hivi tuko kwenye mchakato wa Tanzania kuwa mwanachama wa EITI kama tutatimiza masharti ya kuwa wazi kwenye mikataba na mapato.
Mwaka jana bunge lilipitisha sheria ya madini iliyopingwa sana na upande wa upinzani kwa sababu ya vipengele vya usili katika mikataba na sector hii. Lakini kwa sababu wabunge wa chama chetu ni wengi ikapitishwa. sheria inatoa hata adhabu kwa yule atakaye divulge siri zinazohusiana na mikataba hii. Hivyo basi kabla ya JK kwenda Ufaransa alitakiwa kwanza kuyafanyia mambo haya ya msingi kwanza ili watanzania wawe huru kua access mikataba hii na kujua hasa nini kimewekwa humu. Ngoja niwamegee kidogo tu mapato tuliyopata kutokana na rasilimali chimbwa so far:
Aina ya mapato kwa nchi Shilingi za kitanzania Revenue collected on behalf of the government (hizi ni PAYE na NSSF) 66,129,144,000.00 Total Taxes (yaani Corporate tax, withholding tax, SDL (Skill development levy), import duty, fuel levy ni zero yaani hawalipi na sector specific taxes yaani (loyalties - Mrahaba wa aslimia tatu kama matusi vile?, License na permit fees, mineral concessions, kaprofiti wanakopata TPDC, Local government levy - Zile dollar laki mbili wanazolipwa kule Tarime, Geita na Kahama na devidends inayopata serikali kwenye makampuni kwa sasa hivi ni sifuri) 62,293,938,000.00 Jumla kuu 128,423,082,000.00 Asilimia ya mapato kutoka na kodi ya wafanyakazi wa rasilimali chimbwa 51% Mchango wa kodi za makampuni moja kwa moja 49%
*data hizi ni kwa mwaka 2008: nazo zimepatikana kwa taabu kweli
*Kile wanachodai makampuni wamelipa kwa serikali na kile serikali inachokiri kulipwa vinatofautiana. Sijui wamekunywa? Mtajaza wenyewe, sie tunasonga mbele. Naomba kuwasilisha wana JF.
* Yaani kodi ya wafanyakazi wa migodini na kwenye gas eti ndiyo tegemeo kubwa la mapato ya serikari.
Kwenda ufaransa ni aibu tupu, sijui wanafukuzia masurufu ya safari tu hawa!