Mkuu unauhakika na hilo Jina ulilolitaja hapo juu??? si-dhani kama huyo jamaa aliwahi kuajiriwa na Masha Advocates.kama KWELI ulikwenda kudondosha CV hapo mahala,basi hebu tupe Jina sahihi!!Huyu jamaa ni mwongo mkubwa kabisa.....
moja Masha kalidanganya Taifa kuwa kila mwaka wanaajiri wanafunzi watano wanaofanya vizuri hapo kwenye hiyo firm yao, huo ni uongo kabisa, mimi nilikuwa mmoja wa watu niliyekwenda hapo na Ridiwani, mbona mlimchukuwa Ridhiwani peke yake????
.... sasa iweje kuwa eti Ridhiwani aliajiriwa kabla hata ya baba yake kuonyesha dallili za kuwa President???
Mwisho, usijisifie sana wewe, umeongoza kampuni toka 1991, kwa ufisadi na mmekuwa wezi mkishirikiana na Kikwete kuujumu uchumi na kupeana nafasi kwa kujuana, hivyo sio kwamba wewe unachapa kazi, lo, jamaa analipa fadhila
mh. waziri ameeleza kwamba huyu bwana aliingia kama intern na baadae wakamuajiri. sasa nini tatizo wakati unaambiwa kwamba ni sera ya kampuni kuajiri huku kipaumbele kikitolewa kwa wale intern .nashindwa elewa kwamba watu wana lalamika kuwa kaajiriwa pale...nyie mlitaka nini?
ni vigumu kuwaelewa au kuwaeleza lakini wengi mnajua tunao uhuru wa kutoa mawazo lakini sio kuhukumu moja kwa moja au kutoa tafsiri ya jambo.ukweli ni kwamba ridhiwani anafanya kazi immma kama muajiriwa na immma ni kampuni ambayo inawaajiriwa wengi zaidi ya 20 na maboss zao ni wako wanne. hakuna shaka katika ili kwamba anafanya kazi lakini sidhani kama kufanya kazi pale kunaweza mfanya naye fisadi. kama hii ni maana basi tuangalie BOT,Wizara ya maliasili na utalii, wizara ya miundo mbinu,n.k.waajiriwa wote pale ni mafisadi.
hivi huyu kijana anatakiwa afanye nini?maana akifanya jambo lolote mtasema. hadi lini.basi tumsaidieni mawazo nini afanye?
kweli inasikitisha ndg zangu maana sasa itabidi watu tuanze angalia kampuni ambazo hazina historia ya ufisadi bila kuangalia namna kazi inavyo fanyika. vigumu kutambua lakini inawezekana kabisa.
mwisho nisingependa kwenda kwenye sheria maana mie sio mwanasheria ila nataka sema kitu kimoja. ninavyojua mimi,moja ya kazi ya wanasheria ni kusajiri kampuni na pia kulipwa gharama fulani za kazi baada ya usajiri. mh. waziri amezungumza wazi na kwamba sidhani kama kuna tatizo.kama lipo nafikiri tumtafute yule mwengine alisemwa kuwa ni msimamizi au muongeaji wa kampuni, atayasema. vipi kuhusu kuhusika kwao.
ninavyofikiri au kushauri mimi haipendezi kufanya personal attack kwa mtu.ukweli wa mambo utajulikana.
lakini pia tusisahau kuna usemi wa wahenga unasema......chokochoko uzaa jambo.tusikilize nini kinakuja.
nakaribisha mawazo .aksante sana.
kwa elimu yake na sifa nilizowahi kuzisikia kutoka kwa watu wanaodai kumjua, sikutegemea yeye kama waziri kuitisha press conference na moja ya ajenda ni kuijibia maswali kampuni binafsi ambayo alidai ilishajing'atua kwenye shughuli za uendeshaji wa kila siku pindi alipoingia siasa. kaeleza yote mpaka hatua za kulitia adabu hilo gazeti, mbaya zaidi, mwisho anasema yeye sio mtendaji wa hiyo firm kwahiyo anawaachia watendaji. hv hii firm haina PR? hivi alikua anaongea kama masha au waziri, au vyote kwa wakati tofauti.
otherwise nampa salute kwa kuwa mbali na richmond, ufisadi mwingine siujui ingawa ana hisa tanzaniteone ambayo inatandika risasi wana apollo kila uchao.
Mkuu unauhakika na hilo Jina ulilolitaja hapo juu??? si-dhani kama huyo jamaa aliwahi kuajiriwa na Masha Advocates.kama KWELI ulikwenda kudondosha CV hapo mahala,basi hebu tupe Jina sahihi!!
Mkuu Babah,
Heshima mbele, hii haijakaa sawa, mengine sina uhakika,
1. Masha, alishwahi kuwa Secretary wa Shirika la Oxygen, na baadye akawa director wake, kama kweli ni fisadi basi tungesikia toka akiwa huko ufisadi wake.
2. Amekuwa waziri mdogo wa Nishati, nafikiri hapo ndipo tungemsikia kwenye Richimonduli, lakini Mwakyembe hakumgusa kabisaa meaning kuwa yuko safi.
3. Toka awe waziri kamili wa ndani, hata mwezi hajamaliza, sasa hizi tuhuma zako mkuu mbona nzito sana na hazilingani na Masha kabisaa mkuu.
4. Huko IMMA, ninakubaliana naye kuwa huwa wanaajiri wanafunzi mbali mbali, ninawafahamu wengi waliowahi kuajiriwa hapo ambao baba zao wala sio wakubwa wa nchi.
Ninaomba niseme hivi, Masha ni kijana mdogo sana mwenye shule ya kutosha, na pia ameonyesha uwezo wa kuongoza na ni kichwa pia, maana kijana ana Masters ya sheria ya Georgetown DC, na anayo Bar ya sheria ya New York ambayo hata mtoto wa JFK ilimshinda aliirudia mara tatu lakini huyu kijana Masha aliifanya mara moja tu, hivyo angeweza kubaki huko na kuwa Lawyer mkali na kuishi maisha mazuri kuliko anayoishi sasa, lakini akaamua kurudi nyumbani kulijenga taifa lake,
I mean sina uhakika na base ya mashambulizi yako kwake, lakini nina wasi wasi kuwa humtendei haki kabisa mkuu, I know the kid bro inasikitisha sana kuona kijana mchapa kazi na muadilifu kama huyu, akishambuliwa namna hiii, huku ripoti ya Mwakyembe ikiwashika mpaka katibu wa Nishati, lakini yeye waziri mdogo akiachiwa bila ya kuguswa kabisaa, ninasema mara nyingi kuwa viongozi wazuri na wadilifu tunawafahamu, na mafisadi pia tunawajua, tusiowajua habari zao ziwekwe kwa uwazi na ukweli,
Unless, kuna habari zingine zaidi za ubaya wa Masha, kwa kweli mkuu hizi charges zina walakini mkuu, kulingana na hukumu nzito ulizomhukumu hapo juu, kwamba ati ni mwizi au amepewa kazi kwa kujuana, kwenye hayo naomba kutofautiana na wewe mkuu, Masha ni mbunge wa Nyamagana, uwezo wa uongozi anao maana amekuwa kiongozi akiwa na umri mdogo sana, na hata sasa bado ni kijana mdogo sana, na anaonyesha kuwa atatusadia sana kitaifa na mawazo yake ya kimaendeleo na hasa sera za ki-capitalism, ambazo anaoneakan kuzi-master sana, kwa hiyo mkuu tumpe tu nafasi atuongoze na akosolewe pale akikosea.
Ahsante Mkuu.