Mining sector is time bomb

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,825
287,847
Mining sector is time bomb
DAILY NEWS Reporter
Daily News; Wednesday,July 09, 2008 @20:03

THE Presidential Committee on Mining Review has warned of potential instability in the near future should the government fail to address the effects of mining activities on the lives of people.

“People who have been affected by mining activities should be given consideration and the government should work hard to improve relations between locals and mining companies”, the committee recommended in its report.

The committee also warned in their report that there would be trouble if the mining sector does not contribute to the improvement of people’s welfare.

“Matters such as insufficient compensations, misplacing people from mining areas without resettling them in alterative areas and bad neighbourliness has caused a lot of tensions, which need to be resolved quickly”, the report states.

“People have started losing faith in their government and the only way to restore confidence is by making sure that all matters affecting the lives of people due to mining activities are dealt with once they happen.

“The only way to ensure peace and stability in mining areas is by finding ways of resolving all issues concerning the welfare of people living in those areas,” the report emphasizes.

The report also recommended that the employees of Buhemba mine and Kiwira coal mine be paid immediately.

“The Buhemba mine stopped operations on short notice without considering the welfare of its workers and they should be paid immediately”, the report recommends.

Of the Kiwira coal mine, the report states that the mine was privatized in 2005 but some of its former employees are yet to be paid their entitlements.
 
Hii habari haina mpango kwani inazungumzia compasations za watu kuhamishwa!
Tunataka compesations za kimaendeleo kama maji hospitals,schools,medicine,food,raods etc etc!
Na si eti wanaohamishwa!

Madini ni ya Taifa na wala si kijiji peke yake licha ya kwamba hata wanakijiji hao ndio wanatakiwa kuwa wa kwanza kunufaika na pia kupata ajira na mambo mengine ya kimaendeleo.

Eti people are affected kwa ajili ya mazingira yao!

Nani hajuwi kuwa madini wanayochota ni UTAJIRI USIO KIFANI!

People are affected kwa umasikini unaosababishwa na MFISADI!

HII NI PROPAGANDA NA I GOT SOME GOOSE BUMPS KWANI KAMA WANA RIPOTI YA MADINI NDIYO HIKI WALICHOKIFANYIA KAZI...Then Zitto apone mara moja na aje atueleze kama haya ndiyo aliyomo ndani ya Ripoti ya kamati!
 
Tunasubiri utekelezaji wa ripoti ya Kamati ya Madini
Mhariri
Daily News; Wednesday,July 09, 2008 @20:01

JUZI, baada ya kuwasilishwa bungeni kwa makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini, Serikali iliweka pia hadharani taarifa ya Kamati ya Rais ya Kuishauri Serikali kuhusu Usimamizi wa Sekta ya Madini.

Ripoti hiyo ambayo ilikuwa inasubiriwa na wengi kutokana na unyeti wa sekta ya madini, imebainisha masuala mengi, imezungumzia kwa kina utajiri wa kina ambao Tanzania inao lakini inasikitishwa na jinsi ambavyo watu wake hawajafaidika nao na zaidi jinsi wasivyoisha kulalama wanapoona utajiri huo unawanufaisha wageni.

Kwa mfano, ripoti hiyo imetaka Serikali ichukue hatua za haraka katika kuchunguza uhalali wa taratibu zilizotumika kubinafsisha mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya ambao unadaiwa kufanywa kwa upendeleo na kwa bei ya chini kupindukia wakati Serikali ilitumbukiza katika mgodi huo mabilioni ya shilingi.

Pia Kamati haikuwa na kigugumizi katika kuihoji Serikali umiliki na uanzishwaji wa kampuni za Tangold na Meremeta malipo ya takriban Sh bilioni 160 yaliyowahi kutolewa na Benki Kuu ya Tanzania yakihusishwa na Meremeta.

Mengi yameibuliwa na Kamati hiyo ambayo ilishirikisha wajumbe wa aina mbalimbali wakiwamo wanasheria, wabunge wa CCM na vyama vya upinzani, wataalamu wa madini na kodi.

Kwa kuelewa kwamba Wanakamati hao na Watanzania kwa ujumla wana imani kuwa mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti hiyo yatafanyiwa kazi katika kipindi kifupi iwezekanavyo, tunaamini kwamba Serikali imefanya uamuzi sahihi katika kuiweka hadharani.

Kwa kunukuu maneno ya Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo (UDP) ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati hiyo, kutolewa kwa ripoti hiyo ni ushahidi kwamba Serikali inafanya mambo yake kwa kufuata taratibu na haifichi taarifa zake kwa kuwa haina maovu.

Kila la heri katika utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti hiyo ili hatimaye sote tufaidi matunda ya rasilimali ya madini tuliyojaliwa na Mwenyezi Mungu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom