Minati za Kikao cha waheshimiwa Nyani katika msitu wa Nyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Minati za Kikao cha waheshimiwa Nyani katika msitu wa Nyika

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Graph Theory, Dec 6, 2011.

 1. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Ilikuwa kipindi cha masika msitu ukiwa kijani tupu ndipo kikao kilifanyika. Wajumbe wote katika kikao kile walitakiwa kujifunga majani, yaani walipaswa wote wawe wa kijani ili iwe ngumu kutambulika na jamii nyingine ndani ya msitu huo. Jina la msitu huo uliitwa Nyika. Lengo halisi la kikao kile lilikuwa ni kujadili juu ya tukio la nyani mwenzao kuiba mtoto wa binadamu aliyefahamika kwa jina la "Rich Of Mondu". Kikao hicho kilifunguliwa mnamo mida ya saa tatu kamili kwa mwenyekiti kuwaomba wajumbe kuanza kuchangia. Nyani wa kwanza alikuwa ni nyani aliyeiba mtoto, alianza hoja zake kwa kukumbushia namna alivyomuiba yule mtoto na alisema kama ifuatavyo. Mh m/kiti nakumbuka siku ya tukio wewe ulikuwa umeenda msitu wa Tanga uliopo jirani na msitu wetu wa Nyika, nikiwa katika majukumu ya kusaka chakula kwenye mashamba ya binadamu, ndipo nilimuona mwanamke akilima huku kamuacha mtoto peke yake, nilituma ujumbe kwako kuulizia kama nimuchukue yule mtoto nawe ulinijibu kuwa nisubiri mpaka wewe urudi. Kwa kuwa wewe una spidi kubwa ya kuruka kwenye matawi haikuchukua muda mrefu ukawa umefika, nawe ulipouona uzuri wa yule mtoto na faida ambazo nyani tutapata kwa kukaa na mtoto wa binadamu uliniamrisha haraka sana nimchukue yule mtoto. Nasikitika sana leo hii na kujuta kufanya ushirikiano na wewe kwani baada ya nyani wenzetu kubaini sehemu tulipomficha yule mtoto na hivyo kusababisha kila nyani kuanza kuulizia mtoto yule katoka wapi ilihali si wa jamii yetu, na ulipoona mambo yanazidi kuwa mabaya kwa upande wetu ukanigeuka na kuiaminisha jamii kuwa mimi ndize nilifanya tukio hilo la wizi ilihali tulishirikiana na hiyo kupelekea hata kufukuzwa kwa kazi niliyokuwa nafanya hapa msituni. Laiti huyu mtoto kwa jina la "Rich Of Mondu" nisingekushirikisha masaibu haya yote yasingenikuta najuta. Huo ndio ulikuwa mwisho wa utetezi wa nyani aliyemuiba "Rich Of Mondu"
  Nikiripoti kutoka msitu huu wa nyika nilipokuwa nimejificha karibu na sehemu ya kikao, mimi ni Handsome wa Mama wa Jf.
   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Mamaa mbavu zangu...
  Eti 'Rich of Mondu'!
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  ntaprint kesho nsome
   
 4. libent

  libent JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  umenikosha nimezidisha siku za kuishi
   
Loading...