Minada ya Tanesco wizi mtupu

Pics

JF-Expert Member
May 21, 2020
241
181
Nimebahatika kushuhudia minada ya vifaa chakavu vya TANESCO. Masasi na Tunduru ambayo pia imefanyika Lindi. Na inaendelea Songea, Njombe nk. Kiuhalisia hakuna mnada Ni wizi, kinachofanyika washiriki wa mnada wanakutana na kukubaliana Nani anunue kwa makubaliano. Siku moja kabla wanathathimini anayeubali kuwalipa washiriki wa mnada kiasi kikubwa anaachiwa mzigo akibaliana Bei gani anunue mnadani, wanakuwa wasindikizaji tu kwenye mnada.

Wanazunguka minada you na utaratibu Ni huuhuu. Inaweza tokea wanunuaji wakaongezeka lakini makubaliano Ni hayahaya. Hili linawezekana kwa sababu ya masharti ya mnada lazima uwe na vibali vya NEMC. Inapelekea washiriki kuwa wachache sana tofauti na minada mingine, hii inakosesha mapato Tanesco na Serikali kwa kuondoa ushindani wa haki. Mali ambazo Tanesco ingeweza kupata badala milioni 100 inaambulia milioni 4.

Mnunuzi anawalipa washiriki wenzake biashara imeisha. Ukifuatlia utaona hii minada washiriki Ni walewale, wengi wao hawana uwezo wa kununua wameomba vibali kwa wenye vibali vya NEMC wanashiriki kuharibu minada kwa kulipwa na mnunuzi halisi. Kumbuka hivi vibali kukata Ni Zaid ya milioni 20 (Nemc)kabla ya TRA, halmashauri. Wengi ni wenye viwanda na wanunuzi wakubwa Dar ambao hawaendi minadani .

Ushauri Tanesco jaribuni kuweka mnada wa wazi mtaona tofauti kubwa. Watu walio katika maeneo inayofanyika minada wana uwezo wa kununua kwa Bei kubwa itakayofaidisha Tanesco. Kikwazo vibali vya NEMC (mazingira)kihalisia hakina umuhimu mpaka mtu anayesafirisha.
 
Shiiiii, taratibu bhana awamu ya kulamba asali hii...nawe tafuta kibuyu chako ulambe acha wivu ebo!.
 
Wao wanaweka mazingira magumu ili wapate chakula wakitoa hivyo vipengele hawapati kitu na lengo lao sio kwamba wanataka Shirika la Tanesco lipate kitu ni wao wapate chochote ndio maana wapo radhi wauze kwa bei yeyote wakiwa washalambishwa asali Mkuu...
 
wenzetu minada yote inafanyika online. Watu wanabid kwa uwazi. Bidhaa zote zinaonyeshwa hapo na namna ya kwenda kuangalia kama mtu anataka akakague. Lakini hawa wezi hawawezi kubali kitu kama hicho.
 
Hiyo minada mpaka ufike eneo la tukio ni ya uongo sana sana...wasingeita Mnada watafute jina lake sahihi maana wananunuzi wanajulikana tayari...
 
Nimebahatika kushuhudia minada ya vifaa chakavu vya TANESCO. Masasi na Tunduru ambayo pia imefanyika Lindi. Na inaendelea Songea, Njombe nk. Kiuhalisia hakuna mnada Ni wizi, kinachofanyika washiriki wa mnada wanakutana na kukubaliana Nani anunue kwa makubaliano. Siku moja kabla wanathathimini anayeubali kuwalipa washiriki wa mnada kiasi kikubwa anaachiwa mzigo akibaliana Bei gani anunue mnadani, wanakuwa wasindikizaji tu kwenye mnada.

Wanazunguka minada you na utaratibu Ni huuhuu. Inaweza tokea wanunuaji wakaongezeka lakini makubaliano Ni hayahaya. Hili linawezekana kwa sababu ya masharti ya mnada lazima uwe na vibali vya NEMC. Inapelekea washiriki kuwa wachache sana tofauti na minada mingine, hii inakosesha mapato Tanesco na Serikali kwa kuondoa ushindani wa haki. Mali ambazo Tanesco ingeweza kupata badala milioni 100 inaambulia milioni 4.

Mnunuzi anawalipa washiriki wenzake biashara imeisha. Ukifuatlia utaona hii minada washiriki Ni walewale, wengi wao hawana uwezo wa kununua wameomba vibali kwa wenye vibali vya NEMC wanashiriki kuharibu minada kwa kulipwa na mnunuzi halisi. Kumbuka hivi vibali kukata Ni Zaid ya milioni 20 (Nemc)kabla ya TRA, halmashauri. Wengi ni wenye viwanda na wanunuzi wakubwa Dar ambao hawaendi minadani .

Ushauri Tanesco jaribuni kuweka mnada wa wazi mtaona tofauti kubwa. Watu walio katika maeneo inayofanyika minada wana uwezo wa kununua kwa Bei kubwa itakayofaidisha Tanesco. Kikwazo vibali vya NEMC (mazingira)kihalisia hakina umuhimu mpaka mtu anayesafirisha.
Hawa Tanesco ni wa ajabu sana, kuna vyuma vya nguzo wanazojenga vimetupwa Chalinze na Morogoro miaka sijui ni kwanini havikuwekwa store ili vitumike kama vipuri mbele ya safari na leo watasema ni vyuma chakavu wavinadi
 
Kwani hao TANESCO wanauza hizo nguzo au transfoma?

TANESCO ni miongoni mwa watu wa ajabu maana mtu anapiga suti na tai na perfume juu halafu anaenda kukata umeme
 
Back
Top Bottom