Minada ya Korosho na ufuta kufanyika kwa njia ya Kieletroniki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,236
Katika kuongeza thamani ya zao la Korosho na ufuta hapa nchini serikali imesema katika msimu ujao wa uuzaji wa mazao hayo minada yake itafanyika kwa njia ya kieletroniki ambayo itaaanza mapema kabla ya minada kuanza.

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibiti, Twaha Mpembenwe aliyetaka kujua ni njia zipi zinatumiwa ma serikali katika kudhibiti mporomoko wa bei ya korosho na ufuta katika soko la dunia na kusababisha wakulima kupata hasara kwa kupata bei ndogo wanapouza korosho zao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vigezo vya ubora wa korosho hizo.

Bashe amesema mpango huo pia unakwenda sawia na kutoa elimu kwa wakulima wa korosho ili kuzingatia ubora wa korosho zisizokuwa na unyevuunyevu ambazo nyingi zimekuwa zikirudishwa kwa wakulima katika minada inayofanyika kwa sada na kuzua malalamiko mengi kwa wakulima kutokana na korosho hiyo kuharibika kabla haijafika sokoni.

Kutokana na hatua ya kuanzishwa kwa minada ya kieletroniki mpango huo utasaidia pia kupatikana kwa masoko mengi yakiwemo ya kimataifa.

ITV
 
Hii ni njia bora zaidi pamoja nakuweza kuweka rekodi vizuri na kuzifanyia analysis, pia hi ni Fursa kwa vijana wetu wa mitandao... Twendeni na mama sio yule alileta magari ya jeshi kwenda kugawa korosho bure
 
Suala sio njia ya kufanyika minada, suala ni kuwa Magufuli aliharibu soko la haya mazao Kwa ushetani wake na tabia zake za kishenzi zilizoharibu uchumi wetu. Msikilizeni Mama leteni wawekezaji wanunue hayo mazao, yatujali wananunua kwa njia gani!
 
Mnada wa kieletronik vp wakulima wa hali ya chini wanaaksesi ya hiyo mitandao?
 
Naomba nifahamishwe vema kuhusu minada hii ya kierectronic kunanufaisha vipi mkulima?? kulinganisha na mwanzo ilivokua sio electroniki?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom