Mimi Yanga lkn kwa hili LA kuvunja mkataba na kumdai niyozima fidia siko pamoja na yanga

mkatagogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2015
229
43
Mimi Ni mwanachama wa yanga naipongeza timu yangu kwakuchukua hatua dhidi ya wachezaji watovu wa nidham lkn kitendo cha kudai fidia nimepata shaka na viongoz wetu
 
Hakuna kesi hapo kwani wazaramo ni watani wa kila kabila hapa bongo.
 
Hivi Kisheria Ni Nani Ambaye Anayepaswa Kumlipa Mwenzake Kati Ya YANGA Ambayo Imetangaza KUUBOMOA Mkataba Au NIYONZIMA!!!!??? ALAFU Kusema Hawezi Kucheza Hadi Hiyo Iwe Imelipwa Tayari!!! Sio Kweli, Coz SHERIA Za CAF Na FIFA Mchezaji Hawezi KUKAA Nje Ya Uwanja Kwa Miezi 3 Mfululizo Bila Kucheza Mpira!! Hata Kama Ana Kesi Au Madai Na Timu Yake!!! Ataendelea Kucheza Wkt Masuala Yake Yakishughulikiwa!!!
 
Japo si mwanasheria niliposikia hili nimedharau uongozi wa yanga ina maana hawana mwanasheria? Mimi ningekuwa ndio yangu ningemuacha nisingempanga hivyo angesugua benchi hadi avunje mkataba mwenyewe.
 
Suala La Kucheza Kwa NIYONZIMA Halina Ubishi, Hata Kama YANGA Watakuwa Na Madai Yao!! Kama JUMA KASEJA Vile!!!
 
Hivi Kisheria Ni Nani Ambaye Anayepaswa Kumlipa Mwenzake Kati Ya YANGA Ambayo Imetangaza KUUBOMOA Mkataba Au NIYONZIMA!!!!??? ALAFU Kusema Hawezi Kucheza Hadi Hiyo Iwe Imelipwa Tayari!!! Sio Kweli, Coz SHERIA Za CAF Na FIFA Mchezaji Hawezi KUKAA Nje Ya Uwanja Kwa Miezi 3 Mfululizo Bila Kucheza Mpira!! Hata Kama Ana Kesi Au Madai Na Timu Yake!!! Ataendelea Kucheza Wkt Masuala Yake Yakishughulikiwa!!!

Upande mmoja ukipuuza au kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa mkataba ni wazi kuwa upande huo umevunja mkataba na hakuna mkataba tena kati ya pande hizo. Kitendo cha Niyonzima kushindwa kuitumikia Yanga kwa muda anaotakiwa kufanya hivyo ni wazi kuwa Niyonzima amevunja mkataba na Yanga hivyo ni jukumu la Yanga kutangaza rasmi kuwa hakuna mkataba baina ya pande hizo hivyo Yanga wanayo haki ya kudai fidia.

Katika kesi ya Yanga v Okwi (unreported case), Yanga ilikuwa inadai kuwa Okwi ni mchezaji wao hivyo asingeweza kusajiliwa na klabu nyingine wakati ana mkataba halali na Yanga, Okwi alithibitisha kuwa Yanga ilikuwa haijakamilisha malipo yake ya usajili kwa mujibu wa mkataba. Baada ya kupitia vielelezo na kuzisikiliza pande zote, TFF iliamua kuwa kwa kuwa Yanga haikutimiza matakwa ya mkataba ya kumplipa Okwi fedha za usajili zilizosalia, hapakuwa na mkataba halali baina ya pande hizo hivyo Okwi alikuwa huru kuchezea timu yoyote na hivyo TFF ikamwidhinisha Okwi kuchezea Simba. Maamuzi haya ni ya TFF na yana-apply kwa Niyonzima pia.
 
Hakuna mchezaji aliye juu ya Klabu.

Yanga SC ni kubwa kuliko hata huyo Niyonzima.

Yanga ilikuwepo Kabla ya Niyonzima, na Yanga itakuwepo baada ya Niyonzima.
 
Hakuna pesa niyonzima atakayowalipa Yanga hata ndururu. Yanga walipaswa kufikisha dai lao FIFA kumdai Haruna kwa kutotimiza wajibu wake kimkataba then kesi isikilize kama Yanga wana vielelezo vya kutosha hapo ndipo Haruna atawajibika kulipa. Lakini sio suala la kutamka hadharani klabu imevunja mkataba na huyu mchezaji kwa utovu wa nidhamu halafu iilipe klabu. wamekokotoa vipi hizo hesabu? Tanzania hatuna viongozi wa soka (wanaojua sheria za soka zilivyo).
Hili halina tofauti na issue ya okwi na etoile kipindi kile. Okwi alichelewa kurudi. Jamaa walipochoka wakapeleka claims zao FIFA kuvunja mkataba na kutaka kulipa hawakusema hadharani na kudai pesa.
Tetesi nilizozipata ni kuwa Haruna alionekana Escape 1 kwenye show ya Ali Kiba wadau wa Yanga wakamind likatengenezwa zengwe wakamtimua, pili kuna tetesi za muda mrefu kwenye games za Simba huwa anacheza chini ya kiwango. Otherwise tusubiri tuone
 
Niyonzima kwa kukiuka makubaliano ya mkataba, ni kama yeye ndo kauvunja huo mkataba, hivyo adaiwe tu!
 
Upande mmoja ukipuuza au kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa mkataba ni wazi kuwa upande huo umevunja mkataba na hakuna mkataba tena kati ya pande hizo. Kitendo cha Niyonzima kushindwa kuitumikia Yanga kwa muda anaotakiwa kufanya hivyo ni wazi kuwa Niyonzima amevunja mkataba na Yanga hivyo ni jukumu la Yanga kutangaza rasmi kuwa hakuna mkataba baina ya pande hizo hivyo Yanga wanayo haki ya kudai fidia.

Katika kesi ya Yanga v Okwi (unreported case), Yanga ilikuwa inadai kuwa Okwi ni mchezaji wao hivyo asingeweza kusajiliwa na klabu nyingine wakati ana mkataba halali na Yanga, Okwi alithibitisha kuwa Yanga ilikuwa haijakamilisha malipo yake ya usajili kwa mujibu wa mkataba. Baada ya kupitia vielelezo na kuzisikiliza pande zote, TFF iliamua kuwa kwa kuwa Yanga haikutimiza matakwa ya mkataba ya kumplipa Okwi fedha za usajili zilizosalia, hapakuwa na mkataba halali baina ya pande hizo hivyo Okwi alikuwa huru kuchezea timu yoyote na hivyo TFF ikamwidhinisha Okwi kuchezea Simba. Maamuzi haya ni ya TFF na yana-apply kwa Niyonzima pia.

Mkuu sio kila kukiuka mkataba ni kuvunja mkataba. Utoro au uchelewaji kazini ni kosa kubwa lakini lazima liwe limeshindikana hadi mkataba kuvunjwa. Nahisi Yanga wamefanya haraka kutangaza kumvunjia Niyonzima mkataba, labda iwe ni kwamba wameshampa maonyo mengi huko nyuma kwa maandisshi tena na adhabu kadhaa.

Lakini hata tukisema kuwa Yanga wako sawa, hili la fidia halipo. Huwezi kumpa mtu adhabu mbili kwa kosa moja. Kuvunja mkataba ni adhabu tosha labda ingeendana na kutolipwa chochote. Kudai fidia ni adhabu ya pili kwa kosa lile lile la kuchelewa kurudi kazini!
 
Nilidhani unajua kwamba hii si mara ya kwanza wala ya pili kwa Niyonzima. Wachezaji wengi wa kigeni hulidharau soka letu na kutenda watakavyo kwa kuwa huwekwa juu ya vilabu na mashabiki na viongozi mahaba niue. Wakati wengine wanafahamu kuwa kosa la Niyonzima ni kuchelewa kurejea, baadhi yetu tunajua kuwa aliondoka bila ya ruksa ya klabu (alitoroka na ni kawaida yake ), pia wakati timu ikiendelea na majukumu yake, alionekana akiponda starehe sehemu mbalimbali. Lakini hitimisho la yote ni pale alipodiriki kuvaa POP ili kuwahadaa viongozi. Hata alipotakiwa kupeleka utetezi hakufanya hivyo kwa sababu yeye ni mfalme. Nani wa kumgusa?

Okwi ma Etoile yake alikuwa na mgomo wa kudai malipo yake, hivyo si sahihi kabisa kulinganisha kesi hizi. Niyonzima alipaswa kuwepo eneo la ajira yake kama hitajio la mkataba. Pia ni vema mkaelewa kuwa kuna kipengele ndani ya mkataba kinachomlazimisha kurejesha fedha ya usajili iwapo atakiuka masharti ya mkataba.

Kifupi, Niyonzima kavunja mkataba. Yanga walichofanya ni kuthibitisha tu kwamba mkataba ni ukweli umekiukwa.
 
Mk

MkuU unaona aibu gani kujiita dodoma vijijini? Au shinyanga vijijini?

Yeye kakwambia ni Moshi Vijijini, wewe unamwambia anaona aibu kujiita Dodoma au Shinyanga Vijijini, tatizo lako ni nini? Mbona wewe unajiita Andoid na hakuna anayeku_mind, badilisha mtazamo!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom