Mimi sio mzalendo: Kuna haja gani ya kusajili line kwa vitambulisho vya NIDA kama sio kuchosha tu watu

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,990
17,879
Bora nisiwe mzalendo kama tunaishi chini ya mambo ya hovyo hovyo tu

Tuna kitambulisho cha mpiga kura na kinatambulika vizuri tu sasa shida iko wapi mpaka iwe ni lazima kutumia vya NIDA? Kama sio kuchoshana tu na kuwaumiza na kuwakamua wananchi?

Hii nchi ina mambo ya hovyo hovyo tu yanayotendwa na awamu hii ambayo sio lazima bali upotevu wa muda tu na rasilimali

Hivi kweli kuna haja gani kama mtu keshasajili line na kitambulisho chake cha mpiga kura uje umuhangaishe tena sijui na alama za vidole na NIDA?

Mambo mengine ni ya hovyo tu na kuchoshana

Jambo lingine niloshangaa ni kipindi kile tcra wanahangaika kuzima simu feki?hapa walinufaika na nini na kama sio misifa tu na kupoteza muda

Halafu anajitokeza mtu ananiambia niwe mzalendo!!!

Uzalendo gani?my foot!!!
 
Ukimuona yule sijui ndio waziri wa mawasiliano jinsi anavyoshupalia usajili wa vidole mpaka unabaki kucheka tu!

Nchi masikini hii ya watu wanaokula funza na viwavi jeshi unahangaisha watu na fingerprints ili iweje?
 
Hata mm nashangaa
 
Back
Top Bottom