Mimi sio mfuasi wa Gwajima lakini kumshambulia Pengo alikuwa sawa. Wapinzani acheni unafiki

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,980
4,451
Kweli naamini mpinzani mpinzani tu,hata anaweza kupingana na mama yake kuhusu baba yake halisi.

Mimi sio mwanasiasa,sina chama ni staff. Tujikumbushe Gwajima alikua wapi wakati anamshambulia mzee Pengo,katika utawala wa Kikwete Gwajima alikua mnazi haswa wa upinzani. Kilichofanya amshambulie Pengo ni kwenda kinyume na makubaliano ya maaskofu wote Tanzania.

Kilikaa kikao kuhusu waraka mzito kwenda kwa serikali iliyokuwa chini ya JK baada ya kuafikiana ikaonekana askofu Pengo ni msaliti ndipo Gwajma akamchana live.

Kitendo kile kilifurahisha sana wapinzani waliokuwa wanategemea viongozi wa dini kufikisha kilio chao serikalini. Leo wapinzani mkimshambulia Gwajima nitashangaa sana au kisa yuko upande wa pili?
 
Shaur yao nliwaambia mapema Waache hiyo tabia hawakusikia kila mtu apambane na Hali yake Karibuni Norway tule maisha hapa
tapatalk_1593170591611.jpeg
 
Ngoja nikuulize, hoja zilezile alizozisimia Gwajima dhidi ya Pengo leo hii yuko ccm, anaweza kuzisimamia vilevile?
Kama hoja zake ni tofauti basi na shambulio la Pengo halina mantiki tena. Labda musimamie hoja ya Sunday school.
 
UNAFIKI Mkuu kwa baadhi ya Watanzania ni tatizo kubwa sana. Wanayumba sana ili kuganga njaa zao.

Ngoja nikuulize, hoja zilezile alizozisimia Gwajima dhidi ya Pengo leo hii yuko ccm, anaweza kuzisimamia vilevile?
 
Alikuwa na kadi ya chama gani huko upinzani na aliirudisha lini akachukua ya ccm
Hata kama hakua na kadi alikua ni mrengo wa upinzani. Kakobe ana kadi?
 
Tangu lini Gwajiboy akawa mnazi wa upinzani?
Ni mambo gani tangible aliyofanya akiwa upinzani?
 
...Kitendo kile kilifurahisha sana wapinzani waliokuwa wanategemea viongozi wa dini kufikisha kilio chao serikalini. Leo wapinzani mkimshambulia Gwajima nitashangaa sana au kisa yuko upande wa pili?
Nadhani utakuwa mgeni wa siasa. Yaani unashangaa upande mmoja kuushambulia upande mwingine kwa kuwa tu anayeshambuliwa aliwahi kusifiwa?
 
Rudisha kumbukumbu zako. Ule waraka wa TEC ulikuwa ni kwa utawala wa Magufuli. Ulikuwa ni waraka wa kumlaumu Magufuli kwa kulea na kuwalinda wasiojulikana na kutochukua hatua dhidi ya washambuliaji wa TL.

Baada ya waraka ule Rais alijenga chuki dhidi ya Kanisa. Katika kujiweka karibu naye, kwa namna ya kushangaza, maaskofu wa TEC wakaamua kumchagua Nyaisonga, rafiki binafai wa Magufuki kuwa Rais wa TEC ili kuweka mahusiano mazuri. Baada ya hapo Kanisa Catholic halijawahi kukemea maovu yoyote ya serikali ya Magufuli.

"Tulikuwa hatuna namna zaidi ya kumchagua Nyaisonga kuwa Rais wa Baraza la Maakofu ili kuwa karibu na Serikali", yalikuwa maneno ya Askpfu mmoja, akiongea kwa masikitiko kuwa badala ya kuangalia merit ilinibidi kuangalia mtu atakayerudisha mahusiano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli naamini mpinzani mpinzani tu,hata anaweza kupingana na mama yake kuhusu baba yake halisi.

Mimi sio mwanasiasa,sina chama ni staff. Tujikumbushe Gwajima alikua wapi wakati anamshambulia mzee Pengo,katika utawala wa Kikwete Gwajima alikua mnazi haswa wa upinzani. Kilichofanya amshambulie Pengo ni kwenda kinyume na makubaliano ya maaskofu wote Tanzania.
Kilikaa kikao kuhusu waraka mzito kwenda kwa serikali iliyokuwa chini ya JK baada ya kuafikiana ikaonekana askofu Pengo ni msaliti ndipo Gwajma akamchana live.

Kitendo kile kilifurahisha sana wapinzani waliokuwa wanategemea viongozi wa dini kufikisha kilio chao serikalini. Leo wapinzani mkimshambulia Gwajima nitashangaa sana au kisa yuko upande wa pili?
Mbona umeshajijibu mkuu. Aliyebadili msimamo ni Gwajima, hoja yako ingekuwa na mashiko kama hao wapinzani wangemfuata Gwajima huko alikokimbilia. Wewe ni Gamba tu.
 
Yani Gwajima alimshambulia Pengo,wapinzani wakafurahia kwa kitendo hicho cha Gwajima kwa maana kilikuwa sahihi na hawakumuona kama Gwajima ni mnafki tu. Ila sasa wapinzani hao hao wanatumia kitendo kile kile cha Gwajima(walichokisifia) kumshambulia Gwajima.
 
Inasikitisha sana
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom