Mimi simwamini Kikwete na vikao vyake anavyovifanya na Viongozi wa Chadema! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mimi simwamini Kikwete na vikao vyake anavyovifanya na Viongozi wa Chadema!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mhabarishaji, Jan 24, 2012.

 1. M

  Mhabarishaji JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,001
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Sina imani na JK, na vikao vyake anavyovifanya na Viongozi wa Chadema. Kwa maoni yangu, Kikwete anafanya vikao hivyo, kwa sababu kuu mbili. Kwanza, ni kuwadanganya "International Community" ili wamwone kwamba, ni Kiongozi anaye-relate vizuri na Upinzani, katika suala la Katiba, wakati ni mnafiki.

  Pili, anavitumia vikao hivi, kufanya "delaying tactics". Lengo hapa, ni kuwapa matumaini ya uongo, Viongozi wa Chadema, na kuwachelewesha kupanga "alternative way forward". Sina sababu ya kumwamini mtu huyu, ambaye uongo kwake, ndiyo siasa.

  Nitamwaminije yeye ambaye hata hakumbuki alivyoipigia debe, Ari mpya, Nguvu mpya, na Kasi mpya? Yeye aliyesema ataleta maisha bora kwa kila Mtanzania, na kuifanya Tanzania, kuwa nchi iliyojaa neema? Aliyetoa ahadi za uongo, bila aibu; za meli kubwa katika maziwa yote makubwa, Viwanja kedekede vya ndege, vya Kimataifa; Tanga kuwa Jiji la Viwanda, Kigoma kuwa Dubai, barabara za juu DSM, kuwaleta Waisraeli Ruvu kulima mbogamboga na matunda n.k. !?

  Ninaota ndoto kwamba Wapiganaji wetu, wanachezewa shere! Wapiganaji, mnafikiri kwamba watawala wa Kiafrika, waliotawala kwa miaka 50, na kusema hadharani kwamba, watatawala milele, wanaweza waka-engineer process ya kupata Katiba mpya iliyo bora; kwa amani, kirafiki, na kwa urahisi hivyo? FORGET ABOUT IT! Ilitokea wapi hivyo, Afrika? Experience inaonyesha kwamba kote Afrika, Katiba bora, huvitupa nje vyama vilivyotawala kwa miongo mingi, toka Uhuru. Nani akubali kukupa Katiba bora katika kisahani, itakayommaliza mwenyewe; bila fight?

  MY TAKE: Mikakati ya kuingia mitaani, iingie haraka katika hatua ya Utekelezaji. We have to be time-sensitive, 2015 is around the corner!

  Nawasilisha!
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Possibly true,extra care needed...infact he is a champion of proving unfulfilled promise.
   
 3. g

  gumegume JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 1,060
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  This is food for thought! In some cases, it is sometimes safer, not to be extremely optimistic!
   
 4. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Machalea yamekucheza vyema,
  Lakini huyu mkulu hapa hana cha kupoteza 2015, hivyo inawezekana anafanaya kweli ili aonekane alikuwa mwema na kipatikane kitu cha kumkumbuka atakapoondoka madarakani,
  But kwa upande mwingine haaminiki huyu mkulu! Duuh!
   
 5. M

  Maneno Anania Member

  #5
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumshukuru japo kwa hatua ya kukutana na viongozi wa upinzani Ikulu. Maana huo uamuzi yataka moyo wa ujasili na ninajua wengi wetu tungekuwa nafasi ya JK leo tusingeruhusu hata kuwaona!

  Kilicho kubaliwa na kisitekelezwa baada ya hapo anastahili kulaumiwa lakini kwa sasa it is too early!
   
 6. M

  MPG JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2012
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikwete Tapeli sana alitudanganya Kigoma ataifanya kuwa Dubai.
   
 7. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Huyu Jk si wa kuaminika duniani wala ahera. Mtu ambaye alikana hadharani kwamba hamfahamu Richmond wakati alihusika na mchakato wa kumuingiza nchini (Refer EL), ni wa kuogopwa sana kama ukoma!
   
 8. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Tatizo si la Kikwete bali tatizo ni letu watanzania kwa kuchagua Rahis badala ya Rais.
   
 9. s

  smirna Senior Member

  #9
  Jan 24, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  As the saying goes, "You can say that again!"
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  binadam mwenye ngozi nyeusi mzigo sana,hivi mnataka kikwete awanyie nini watanzania ndo mumshukuru????????????mmepewa uhuru wa kutukana mnalalamika,mmejengewa shule kila kata maneno,barabara nchi nzima maneno,hii ni dalili ya kufilisika kimawazo.watu wanaumiza vichwa kutafta shilingi,wewe unahangaika na kikwete,utakufa maskini,BADILIKA TAFAZALI.
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mleta mada ni wa kupuuza tu,hana sera ni wivu tu.nina wasiwasi na usalama wake katika serikali ya ubongo wake.
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kwanza ujue kuwa kafanya uungwana wa hali ya juu ku intertain kuwakaribisha hao jamaa kwenda kunywa juice pale mjengoni kwa sababu hayo masuala ya katiba yalipaswa kuzunguzumziwa bungeni.kikwete ni mtu wa huruma na msikivu sana,ingekuwa mimi nisingekaribisha huo uchafu wa mazungumzo kama hayo ikulu,watanzania wanawalipa wabunge kwa kodi zao,wanazitumia kwa kususa susa,leo tena unawaita ikulu,who are they???????????????????????????????????????????
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hii thred ni ya kimbea mbea sana,walioenda kumuona ndo wanajua wanachokifanya,we baki na upupu wako kichwani na mawazo yako ya kufikirika,utapata wa kuwadanganya hapa jf ambao hawashughulishi akili zao kufikiria hata kidogo.
   
 14. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #14
  Jan 24, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Mimi siwaamini wote walioshiriki hayo mazungumzo kwani hata huo upande wa pili unapotoka unakuja na stori zisizoeleweka. Mara wamo mara hawamo. Jk Msanii, CDM hawana msimamo!
   
 15. m

  mwikumwiku Senior Member

  #15
  Jan 25, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilishasema hapa kwamba ss hatuhitaji kuona picha walizopiga na Rais bali wanachozungumza huko!
   
Loading...