Elections 2010 Mimi Sijaandika Hata Neno Moja Hapa...

Mdau

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,789
470
From CCM yazuia JK kushiriki mdahalo

Comments

#46 CAROLINE 2010-09-12 19:57
Doctor wa miujiza amekataa kuingia kwenye mdahalo kwani majini ya Muuguzi wake Shehe Yahya Hussein hayajakamilisha
kazi zake.JK bigwa wa ahadi ameahidi kujenga viwanja vya ndege vitatu na viwanda kibao Tanga wakati hajui hata fedha atapata wapi?.Mimi nimemshangaa mtu anatoa ahadi ya viwanja vya ndege 3 wakati alivyo navyo haviwaki hata taa.
Warusha ndege wanaruka kwa kubahatisha.


#45 Msemakweli 2010-09-12 19:54
CCM acheni uswahili na polojo kwa kutoa sababu sizizo na msingi za kukataa kushiriki mdahalo. Huo ni uoga na hiyo ni njia ya kuendelea kuficha maovu yenu. Sidhani kama huko majukwaani kuna muda wa kuuliza wagombea maswali, kwa sababu tunataka tujue kwamba JK atatumia mbinu gani ambazo hakutumia miaka mitano iliyopita kutimiza hizo ahadi lukuki anazotoa kwa wananchi. Kwa hiyo tafadhali CCM tunahitaji hayo maswali yajibiwe kwenye mdahalo, mnatia aibu kuona kwamba hamjiamini kiasi hicho. We real miss Mkapa, pamoja na kwamba inasemekana kwamba naye alichota dakika za mwisho, lakini leadership tuliiona, lets hope kwamba Dr. Slaa atafanya zaidi ya hapo hasa katika suala la mafisadi.


#44 sele 2010-09-12 19:49
MAKAMBA' KINANA' NA MGOMBEA WENU INGIENI KWENYE MDAHALO HALAFU NDO MSEME HAYO.


#43 CHADEMA DAMU! 2010-09-12 19:44
Tulisema mapema CCM hawana jipya CHADEMA oyeee oyeee KIKWETE aogope hivyo hivyo sie tunapeta jana MWANZA ILILIPUKA KWA WINGI WA WATU WALIOJITOKEZA KUMSIKILIZA DR.SLAA,DALADALA Zilibeba watu bure kwenda uwanjani BUREEE na watu wa MWANZA URAIS ni kwa CHADEMA - KIKWETE HAWEZI HATA ROBO KUJENGA HOJA MBELE YA SLAA,hata sikumoja huwezi kumkalisha MSOMI na MC,lol lol lol


#42 emanuel mikomangwa 2010-09-12 18:43
Ah hii ni kali majibu ya Kinana ni ya Kariakoo!Hivi katika vita mtu anachagua silaha ya kutumia kweli au ikibidi hata jiwe anatumia mradi ashinde!Mbona Mkapa aliutumia Mdahalo kujijenga japo alikuwa hafahamiki tukaona uwezo wake wa kujenga hoja na kweli akashinda!Kuna sababu mbili tu za J.kiwete kukataa mdahalo!

1) Uwezo wake umedhihirika wazi ni mdogo sana anaweza kuongea na wazee wa Dsm tu ambao hawajui kitu isipokuwa kunywa kahawa!huu Udakta wa Bagamoyo ni wa kuogopa zaidi ya kifo.Rais anakuwa mwoga namna hiyo??Why should he not seize this opportunity to convice elites that he is capable of correcting his mistakes.
2)Maovu aliyoyafanya na ahadi hewa Wananchi wanazifahamu fika na ahadi anazotoa hivi sasa hazitekelezeki ni usanii mtupu hawezi waambia watu wenye ufahamu wakamwelewa na wakimuuliza maswali hataweza kuyajibu ni contradiction tupu.

Kwa kweli Jakaya amekiaibisha chama na washikaji wake hii ni CCM kweli nayoijua mie.CCM jifunzeni acheni kuweka viongozi dhjaifu namna hii kwa uswahiba mnaona anavyowaponza na maswahiba wake.Lt Makamba.Brig Kinana,Lt Col Kikwete wanajeshi tangu lini wakaweza kunyambulisha mambo wamezowea amri na ndio maana wanajazba wote hao kwani hamzioni kauli zao?

VIVA Lipumba,VIVA Slaa ninyi ni wasomi wa kweli uelezeni UMMA hata kama usipowachagua mimi nimekwisha heshimu Elimu na ufahamu wenu kwani mmediliki!

You may fool a person for sometime but not all the time tumekwisha wang`amua ambao hawajang`amua wana Upungufu akilini mwao!

Kikwete alipata gentleman degree atamudu mdahalo na Madaktari wa kiukweli?? majibu yako wazi msitafute mchawi Kikwete ndo anaogopa mdahalo ngoja akaanguke majukwaani kwa woga wake alionao ni kheri angehudhuria Mdahalo akiwa amekaa!


#41 ASNATH 2010-09-12 17:53
kikwete unaogopa nini.. au utashindwa kutetea uozo wa serikali yako.. serikali inayotoa muda kwa wezi wa mabilioni kurudisha pesa na kusamehewa wakati mwizi wa kuku anafungwa miezi sita na mahakama ya mwanzo. BE A MAN AT LEAST ONCE IN YOUR LIFETIME. shiriki mdahalo kama kweli unajua unachokizungumza.

#40 LENGAI 2010-09-12 17:32
Kwa nini Doctor Jakaya Mrisho Kikwete anakwepa mdahalo na kina Prof Lipumba na Dr Slaa kwenye huu uchaguzi wa Kidemokrasia Tanzania au Elimu ya Udakrati wa kuchakachuaaaaa aaa!

#39 DAUDI 2010-09-12 17:21
Kinana una bahati sana kwa kuwa muadilifu kwa serikali na chama cha CCM vinginevyo wangekuwekea zengwe kuwa wewe sio mtanzania ni msomali

#38 mdau 2010-09-12 16:32
Kwa nini wanamnyima Dokta Kikwete nafasi ya kuwaeleza Watanzania mafanikio yake kwa miaka mitano iliyopita pamoja na mambo atakayofanya kama akipewa miaka mitano mingine sambamba na wanaotaka kuingia Ikulu? Kinana mwenyewe umesema wenzetu (mataifa kumi) wanafanya hivyo.


#37 afp607 2010-09-12 16:17
Well said guys. CCM imepitwa na wakati na haiwajali wananchi. Kukimbia mdahalo ni aibu na dhihirisho la kuwa wametenda makosa mengi sana hadi wanashindwa kupata cha kujitetea. E bwana hilo swala la kuwa makini na mawakala liko sawa sana. Tena ikiwezekana waanzishe internet site maalum ambapo watakuwa wanapost matokeo kila yanapotangazwa katika kila kituo ili yawe public zaidi. Kukiwa na redio na magazeti kama haya yatakayojitolea kufanya kazi hiyo itakuwa safi sana pia.


#36 Joel Kimbisa 2010-09-12 15:03
Kikwete hajazuiwa na mtu yeyote kufanya mdahalo. Ameogopa mwenyewe. Yeye ni mwenyekiti wa Chama, anawezaje kuzuiwa na watu walio chini yake? Akijitokeza atashindwa vibaya kwa sababu serikali yake imeoza kwa wizi na yeye mwenyewe ni mwizi wa hali ya juu!


#35 Expedito Mduda 2010-09-12 14:40
Hivi katika akili ya kawaida tu, we makamba na mwenzio kinana hamuoni mnakiua chama chenu? Kadri yenu mnafikiri watanzania bado ni wale wa kudanganyika! Hapana, mmekosea! Nendeni mdahaloni haraka!!!


#34 CCM Damu 2010-09-12 14:40
Mimi ni CCM damu, lakini hatua hii imenisikitisha. hii ni nidhamu ya uoga isiyoambatana na nyakati za uwazi na ukweli. Kwa hili Mzee Mkapa amekuwa mfano wa kuigwa. nina imani kubwa na uongozi wa Mh Kikwete na ninatumaini kuwa uamuzi huu wa kuturudisha nyuma utabadilishwa, nasi wananchi tupate fursa ya kutambua yale waliyodhamiria viongozi wetu wa CCM.. bila kuhudhuria mikatano yote.. huu ni uwazi na ukweli.. na kila fursa ya kujieleza yale tuliyodhamiria itumike bila woga, bila kificho... fikra za kale zisizoendana na mbinu mpya tuepukane nazo. Hiki ni chama cha wengi Tanzania na ukweli huu ni haki yetu.. kwa heshima na taadhima nauomba uongozi makini wa CCM uondokane na uoga huu na tutumie vilivyo vyombo vya maaendeleo tuliyoyaleta wenyewe... ni kama kuogopa kupanda gari kwa kisingizio cha kuwa tutafika kwa baiskeli.. tunachelewaaaaa aaaaaaaaaa!

#33 habib hasani 2010-09-12 14:16
uyo kikwete, makamba, kinana sizani kama wana nia nzuri na nnchi yetu. yani mnaogopa mdahalo mimi shabiki mkubwa ila kuanzia leo najitoa ccm mana sioni jipya. nawashauri wa watanzania wenzangu mwenye nia nzuri na sisi ni DR Slaa tumpe kura zote yeye.


#32 Nkulikwa Kassimu 2010-09-12 13:43
Ni wazi kuwa kusema vyama vingine havina sera ni kudannganya umma wa Watanzania na kuwafanya kuwa ni watu [NENO BAYA] wasiojua kusoma na kuandika, ni [NENO BAYA] kwa wapiga kura.Kwa mfano kupunguza mishara ya Raisi kwa asilimia 20 na wakuu wa mikoa. Kupunguza mishahara ya wabunge kwa 15%, ambayo mimi naona ingepungua zaidi. Huwezi kutamani kingi wakati huzalisha kingi, huwezi kuwa omba omba ukaishi kama si omba omba. Taifa linalotegemea misaada kuendesha nchi halitakiwi kuwa hata na Bunge maana ni taifa mfuu.

Mwalimu Nyerere alisema kama mchwa wanajenga daraja iweje sisi Watanzania tushindwe hata kutengeneza sindano ya kushonea? Ni aibu kwa nchi ya Tanzania kuwa kama ilivyo, ni aibu hata kwa Raisi wake. Hata usafi tunataka misaada, ovyo na u[NENO BAYA] mkubwa wa fikra na u[NENO BAYA] wa mawazo. Wanatia aibu hata mbele za Mola ni wale ambao hukaa ki[NENO BAYA] na kuombaomba kwa watu. Na utegemezi mkubwa ni utegemezi wa akili, anaishi kwa kuomba omba ni mfu hata kama anatembea. Ni aibu hata kusimama mbele ya wananchi kuwa wahisani watatusaidia hiki au kile.Kukimbia mdahalo ni ishara ya kuishiwa fikra, ni ugonjwa wa kisiasa na ni upungu wa kinga za kifikra kwenye ubongo.Tumekuwa maskini kwa kujitakia.

Tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha, ni wakati wa kusimama na kusema imetosha. Wengi wanaosifu CCM ni wale wanaofaidika kwa kuiba, ni wale ambao wanaangalia biashara zao na matumbo yao, hata Kikwete hawampendi, ni kupe na ndorobo wa kisiasa.Ni funza wa maendeleo yetu! Ni wale wasio na utashi wa aibu na mishipa ya aibu kwao imekatika. Huwezi kuwa muumuni na ukawa sehemu ya CCM, huwezi kumpenda Mungu na kuipenda na kuipigia kura CCM, maana utakuwa unashiriki katika wizi na imeandikwa usiibe.

Kuna wakati namuonea huruma Kikwete maana amezungukwa na wezi tena wezi, wasiojali nchi ila matakwa na matumbo yao. Ni kweli Tanzania bila CCM inawezekana!Wan aweza kuiba kura na kushinda,lakini hawezi kuiba utu na fikra za Wana mapinduzi. Kuna waliowahi kudhani kuwa utumwa hatakuwa na mwisho, lakini utumwa wa kimwili umeisha bado na kiakili unaoenezwa na CCM. Kuna watu wazima, wakisimama mbele ya Wazungu wanao ni Miungu. Wamepoteza dira na kuua utu wao. Tujiulize kwa nini mboni ya jicho ni nyeusi na ni weusi, ni kwa kuwa ndani yetu kuna ushujaa wa kuona mbinu mpya za kimaendeleo, ila CCM wanafurahia u[NENO BAYA] na u[NENO BAYA] wa wananchi wa nchi hii.

Tunapenda starehe kuliko maendeleo, tuko kama watoto wadogo wanaochezea mchanga. Nchi inakupa vyandarua na wewe unadhani ni hisani ya maana. Ni kweli hatuna uwezo wa kujitengenezea vyandarua, nini utu wetu basi, ubinadamu na matumizi ya ubungo wetu ni kwa ajili ya nini? Wao wanachukua zawadi gani wakikupa chandarua? Kuna tofauti ipi na wale waliokuwa wanapewa shanga na wao kutoa dhahabu, ni aibu CCM.
 
Matatizo ya Watanzania wa vijijini;
maji,
nishati(umeme),
soko la mazao yao,
miundombinu(barabara na usafiri wa reli usioaminika,
huduma mbovu za afya,
elimu duni(majengo yanaitwa shule!),
usalama(watu wanauawa kwa imani za kishirikina),
mimba mashuleni(oh,hili alisema wana kiherehere)
mawasiliano(mpaka wapande juu ya mti ndo wapate network).
Now,Kinana's of this world...Niambie kuwa JK halifahamu lipi kati ya haya??Yalikuwepo alipopita 2005 na bado yapo mpaka leo_Oh,nilisahau kuwa CCM pia ni tatizo kwa wananchi!
 
Mpaka sasa waajiriwa wa kusafisha hawajafika kuwatawaza mabosi wao? Wako wapi leo au ndo mambo ya long weekend?
 
yalaaaaaaa Munguu yupo bwana ccm itatoweka kama utawala wa rumi ulivyotoweka KULA NA USAFIRI,PESA TUNAPATA CCM BUREEE,KURA NI CHADEMA KWA DR.SLAAAAA NA WABUNGE WAKE PIA MADIWANI
 
yalaaaaaaa Munguu yupo bwana ccm itatoweka kama utawala wa rumi ulivyotoweka KULA NA USAFIRI,PESA TUNAPATA CCM BUREEE,KURA NI CHADEMA KWA DR.SLAAAAA NA WABUNGE WAKE PIA MADIWANI

taratibu aisee, nasikia wakazi wa Moshi Mjini wanalalamika kwamba safari hii pesa za CCM hazitoshi ati!!!
 
Back
Top Bottom